Coz wanakua wamepakumbuka sana uraiani na wamekumbuka kua huru na kufanya mambo wayatakayo bila kusimamiwa na mtu,uhuru wa binadamu ni muhimu na unathamani sana,na thamani yake utaijua siku utakapo nyimwa huo uhuru,
Hata watoto wa shule inapogongwa kengere hutoka nduki darasani wakielekea nje ili wawe huru kufanya watakalo bila kusimamiwa na mtu,
Hata kwenye vyombo vya usafiri kama vile Ndege,mabasi,Meli n.k Kila abiria hutaka awe yeye wa kwanza kutoka nje ya hivyo vyombo! Na sababu kubwa ni kutaka kua huru zaidi coz ndani ya safari ya masaa 6 n.k ndani ya chombo cha usafiri ni kama kifungo tu!
Hata mifugo kama vile Kuku,Bata,Mbuzi n.k unapowafungulia asubuhi ili watoke kwenye mabanda yao,basi hutoka nje kwa spidi na kuruka ruka kwa furaha ili wawe huru zaidi kwenda watakako, usiuchezee uhuru wako mkuu ni kitu chenye thamani kubwa sana.