Kwanini Watumishi tunaungwa katika Vyama vya Wafanyakazi, Chama Cha Wafanyakazi Wa Serikali Na Afya Tanzania (TUGHE)na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) bila kuchagua?
Kuna hivi vyama vya Wafanyakazi TUGHE na TALGWU wanakuunga kilazima bila mfanyakazi kujua, hawakupi hata form ya kujiunga unakuta umeungwa tu na waanaanza kukata kwenye mshahara na ukitaka kujitoa hawataki wanakuwa wakali kama vile ni lazima kisheria kwa mfanyakazi kujiunga.
Ulalamishi mwingine huwa mnapenda kuuanzisha bila hata sababu za msingi ninyi watumishi.Sasa,unataka uende kujiunga TUGHE wakati wewe ni wa TALGWU?Au mwalimu akajiunge kwa wafanyakazi wa viwandani? Changamoto yenu kuu ni kutaka mlumbane tu na waajiri wenu utadhani purukushani za walimu na wanafunzi mmezihamishia kazini.Acheni vurugu.Hapo ni kwenye ajira siyo shuleni mlipodekezwa na kutetewa na wazazi wenu mtaharibu maisha yenu.