Nawasalimu wote. Naibu karibu mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia elimu amekemea vikali tabia ya baadhi ya watumishi kuhama kwa kutumia njia zisizo rasimi huku akihusisha jambo hilo na pesa. Ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa Kuna maafisa Wana barua za uteuzi ambazo hazitoki kwa katibu mkuu utumishi. Hayo ya nafasi na vyeo sitaki kuyasemea kwasababu inafikirisha sana kusikia eti afisa Fulani ngazi ya wilaya ana barua lakini haitoki kwenye mamlaka za uteuzi.Nizungumzie kuhusu uhamisho. Maoni yangu nikwamba urasimu katika kufanikisha uhamisho wa watumishi unachangia kwa kiasi kikubwa watu kutumia njia za mkato. Pia ifahamike kuwa zinaitwa njia za mkato lakini ukweli nikwamba zinahusisha gharama kubwa sana kwa mtumishi anayetaka kuhama. Serikali ijiulize nikwaini mtumishi mwenye mshahara mdogo ashindwe kutumia utaratibu rasimi wakuhama badala yake akope hadi milioni mbili ili atoe kwa watu anaowafahamu kwa ajili ya uhamisho? Nadhani hili swali lakwanini shortcut likifanyiwa kazi hakutakuwa na tatizo kwenye kuhama kwa mtumishi.
Mwisho,kama kweli serikali itawarudisha watu waliohama bila utaratibu kwenye vituo vyao vya zamani itakuwa kilio kikubwa.
Mwisho,kama kweli serikali itawarudisha watu waliohama bila utaratibu kwenye vituo vyao vya zamani itakuwa kilio kikubwa.