Kwanini wauaji wa MO29 walitaka wagawane dhambi za mauti na wahudumu wa hospitali?

Kwanini wauaji wa MO29 walitaka wagawane dhambi za mauti na wahudumu wa hospitali?

Huo ni mwanzo tu. Wanaenda kupachika na kujaza madaktari na manesi wa mchongo na watendaji mahospitalini na kusambaza uchawa katika kada ya afya.

Itafika wakati hata wagonjwa wataangaliwa ni wa mlengo gani wa kisiasa. Ukiwa wa upande ule, haupewi huduma au ndiyo wahudumu wanaambiwa "mpelekeni mochwari akaponee huko".

Tayari sekta ilikuwa kwenye hali mbaya, sasa imagine wakifanya hayo yote itakuwaje?
Tunahitaji ukombozi wa haraka,nchi hii kumbe haijawahi kupata uhuru.

Nashauri nchi ikikombolewa,bendera ya Tanganyika iongezewe rangi nyekundi kama ishara ya kuwaenzi mashujaa waliomwaga damu MO29
na kwamba nchi imekombolewa kwa damu,si kwa mdomo kama tulivyoaminishwa
 
Hata vitani unyama kama huu haufanyiki, mateka wa kivita hutendewa vyema kwa mujibu wa sheria. Hawa majini subiani wa Tanzania ni level ya juu kabisa ya ushetani
Kweli mkuu, mateka wa vita kati ya nchi na nchi hawatendei hivi , na ni makosa makubwa mateka wa vita amejisalimisha then bado unamminia risasi, hebu fikili kwenye vita bado zipo sheria za kiamataifa za kuwalinda mateka ila kwenye maandamano ya nyie kwa nyie ndani ya nchi , hakuna , mnauana wenyewe kwa wenyewe kisa tu uchaguzi.

Chadema Mungu awalinde sana , huu mtego kweli viongozi mliopo mmewekwa na Mungu, kupitia wanadamu.
 
Tunahitaji ukombozi wa haraka,nchi hii kumbe haijawahi kupata uhuru.

Nashauri nchi ikikombolewa,bendera ya Tanganyika iongezewe rangi nyekundi kama ishara ya kuwaenzi mashujaa waliomwaga damu MO29
na kwamba nchi imekombolewa kwa damu,si kwa mdomo kama tulivyoaminishwa
Muhimu sana!
 
Mkuu hapa watumishi wa afya wanaweza kuwa wanalaumiwa bure ,watu wapo chini ya mtutu wa bunduki ,ulitaka wafanyeje, na mbaya zaidi aya mahospitali ,ukisikia mkurugenzi , mara Rmo ,Dmo , ni machawa pindukia wa ccm,

Swala sio kusumbua watumishi wa hospital bali walio juu yao , watumishi wa chini ni kuwaonea katika hili
Hapana ndugu..! hata chini ya mtutu haiwezekani kutoa ushirikiano kuwezesha uovu kufanyika, lazima kama taifa/jamii tukubaliane kwenye mambo yanayojenga haki na uwajibikaji kwa watu na taifa..bora itokee awapige risasi wote lkn si kumpa ushirikiano wa uovu anaofanya! wauguzi na madaktari wana viapo, ni vya nini sasa km wanakuwa sehemu ya uhalifu kwa wale wamekuja kwao kutaka msaada..? hapana hatuwezi kuwa jamii ya hivyo! mbona masista waliwakatalia hao polisi na hawakuwafanya chochote?
 
Back
Top Bottom