Kwanini waumini wengi wa Dini ya Kikristo wanaamini mkristo aliyefanikiwa ni mchawi au anatumia nguvu za Giza?

Kwanini waumini wengi wa Dini ya Kikristo wanaamini mkristo aliyefanikiwa ni mchawi au anatumia nguvu za Giza?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Wakristo wengi wanamwomba Mungu awape maarifa ya kutafuta Mali.Wengi wanafanikiwa; wakifanikiwa Tu wenzao uacha kumtukuza Mungu Kwa kumpa utajiri mwenzao badala yake umwita freemason.

Wachungaji wote waliofanikiwa nchini wanaitwa freemason. Wafanyabiashara nao freemason.

Je, Mungu wa wakristo hana nguvu yakutoa utajiri Hadi sifa na utukufu tumpelekee freemason? Je, hizi kebehi Kwa Mwenyenzi haziwezi kuwa chanzo cha umaskini Kwa wakristo wengi wanaokwenda kanisani.

Kwanini Mungu wa wakristo asitukuzwe anapowa Mali waja wake? Wakristo mnamkosea Sana Mungu; kila akitoa baraka mnamdhiaki na kumfananisha na miungu.

Jitafakarini Sana msiendelee kumchukuza Sir God

Jumapili njema
 
Bila kuhusisha dini .... Eneo lolote Lile ukifanikiwa kuzidi walivyozoea upeo wao wa akili unakimbilia katika uchawi Kama source ya mafanikio.
Ni ugonjwa wa kurithishana ktk namna ya kufikiri na kulitafakari Jambo ambapo mbele ya chujio ametawala Mganga, Mchawi Kama sio Masonry.
 
Kwa mkristu aliyekamilika, anatafakari jinsi Yesu alivyojaribiwa na shetani pale mlimani. Kwa kutumia logic, Mali yote ni ya shetani. Yesu alikataa mali ya shetani, sasa wewe mkristu uliyetajirika huo utajiri umetoa kwa Yesu??
 
Wewe NI mmoja wa wanaolengwa hapa; matajiri wote Dunian NI Mali ya shetani? Mungu kwako wewe ni wamaskini?
 
Mkuu

Ukweli ni kwamba:-

Wakati unahangaika ilibupate mtaji hakuna anaekuwaza na wewe upo wote wanakuona mhangaikaji tu!

Sasa Basi

Ukiafanikiwa kuupata Huo mtaji ukaanza biashara BADO hakuna anaekuwaza ,Sasa ukianza kupanda kiuchumi na kuanza kumiliki vitu VYA kawaida kama nyumba ya kuishi,nyumba za biashara,Biashara ukaanza kufahamika kwa matajiri na kuaanza kuwa Don:-

Walimwengu macho wanakodoa kodo kodo kazi inaanza rasmi kukuwinda kiroho na kimwili na maadui wanaanza kuibuka tena wanaanzia kwenu kwenye ukoo wako Hadi wa nje!!

Mf; unaanza kuuguliwa, Biashara haitoki kama zamani,wakikopa hawalipi!na pesa haikaliki!

Sasa matokeo ya kushambuliwa unajikuta kwenye madhabahu mojawapo ukitengeneza mfumo,!

Hapo Ndio maana watu wa imani wanaamini waliofanikiwa wanatumia ndumba ku survive kwenye Hali zao na sio kanisani wala ibadani!!

Takwimu zinaonyesha ibada Zina favor watu wasio na makuu maishani yaani wale ambao sio wasaka noti bali wakivaa,kula na kulala inawatosha hao Ndio wanadunda Sana kwenye imani lakini wasaka noti wote wanapigana mno kiroho!! Tambua hilo Mkuu!!
 
Ukipata mtu aliyeshika hii imani kikamilifu ni masikini wa kutupwa. Kwa maneno mengine dini ni umasikini. Pale mlimani Yesu aliambiwa nini na shetani? Usimumunye maneno, sema ukweli. Hawa wanaosema wanafufua watu, mpaka kununua helicopter ni utajiri wa Mungu?
 
Wakristo wengi wanamwomba Mungu awape maarifa ya kutafuta Mali.Wengi wanafanikiwa; wakifanikiwa Tu wenzao uacha kumtukuza Mungu Kwa kumpa utajiri mwenzao badala yake umwita freemason.

Wachungaji wote waliofanikiwa nchini wanaitwa freemason. Wafanyabiashara nao freemason.

Je, Mungu wa wakristo hana nguvu yakutoa utajiri Hadi sifa na utukufu tumpelekee freemason? Je, hizi kebehi Kwa Mwenyenzi haziwezi kuwa chanzo cha umaskini Kwa wakristo wengi wanaokwenda kanisani.

Kwanini Mungu wa wakristo asitukuzwe anapowa Mali waja wake? Wakristo mnamkosea Sana Mungu; kila akitoa baraka mnamdhiaki na kumfananisha na miungu.

Jitafakarini Sana msiendelee kumchukuza Sir God

Jumapili njema
Wanaona wachungaji wao wanavio tumia misukule
 
Shida ya fikra za umaskini na umaskini kwa ujumla ni kufikiri unapendwa sana Mungu,,,kujiona una haki sana kwa Mungu,,,kuliko hao matajiri na kuona matajiri wote ni maadui katika maisha yako,,,,na ukifatilia sasa fikra za kimaskini na maskini wengi ndio wanafki,,wachoyo,,,roho mbaya,,wakudaa,,na wachawi haswa,,,ni wale usoni kama watu lakini rohoni ni hatari tupu!!
 
Back
Top Bottom