Mkuu 'Proved', na mleta mada mkuu 'Mag3, jibu langu kwenu ni hili: kwamba Zanzibar ni mnufaika, awemo au asiwemo ndani ya mkataba huo.
Mavuno yote yanayotokana na shamba la bibi Tanganyika, kama hayo mkuu Mag3 aliyoyanukuu toka ndani ya maandishi ya makubaliano yataingia Zanzibar, bila ya Zanzibar kuwa mshiriki katika mkataba huo, hili lipo wazi kabisa.
Sasa basi, kama kuna athari zozote zinazoambatana na masharti ya mkataba huo, ya nini Zanzibar ajitumbukize kwenye 'risk' hiyo isiyokuwa na lazima yoyote?
Zanzibar na washirika wake, akina UAE na makampuni yao haya, sasa wanaimarisha kuitawala vizuri zaidi Tanganyika. Zanzibar ni mbia, au tuseme ni mwezeshaji wa mpango huo wa kuitawala Tanganyika na kuvuna wanavyotaka.
Muungano ulio assisiwa haukuwa na lengo hili, lakini bila ya kujitambua, CCM sasa wametufikisha huko kwa lazima.