Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Nimefikiria sana mpaka nimekosea majibu, tulizaliwa watoto saba nyumbani, na ndugu waliokuja kuishi nyumbani kipindi tunakua wanafika 6, hao waliosomeshwa na mzee, japo wengine walikua wanakuja na kuondoka, mabinti wengine walikua wanakuja kujifunza cherehani na kuondoka, na sio kwamba mzee alikua na maisha mazuri hapana ya kawaida tu wala hakua mtumishi wa serikali, japo ndugu kutoka kijijini walikua hawakatiki pale nyumbani kiukweli tulikua na familia kubwa yenye upendo, mpaka sasa mzee ameshazeeka na tumeshakua watu wazima, lakini bado ndugu wapo huko nyumbani pamoja na wajukuu kutoka sehemu mbalimbali.
Nikipiga mahesabu yangu na nina watoto wawili wako primary lakini maisha yananiendesha, yaani nawaza hapa wakiongezeka ndugu wengine nitaweza kuiendesha hii familia? Sasahivi vijana wengi wanavipato lakini ni ngumu sana kumsomesha ndugu yake ukiachana na ndugu wadamu, lakini mtoto wa baba mkubwa sijui mama mkubwa upendo haupo kabisa.
Hapa nawaza wazazi walikua na upendo sana au walikua na uwezo? Au maisha yalikua cheap miaka hiyo?