Kwanini wazee wanaogopa sana kifo kuliko vijana?

Kwanini wazee wanaogopa sana kifo kuliko vijana?

Sean Paul

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
1,330
Reaction score
3,289
Habari wana JF,

Katika uzoefu wangu na utafiti usio rasmi nimegundua watu wazima hasa wazee waliozeeka haswaaa, ni waoga wa kifo kuliko vijana.

Sisi vijana tunatake risk nyingi sana za kuogopesha na kuweka rehani maisha yetu, wala hatuna woga uliopitiliza wa kifo. Lakini wazee wetu wengi ni waoga sana wa kifo. Nadhani wengi mtakua mmejionea huko kama ikitokea mnauguza wazee hali inavyokuwa.

Inakuwaje mtu aliyeishi miaka 70+ ni mwoga wa kifo namna hiyo? Ana nini cha kupoteza huyu? Ni kawaida hali hii kutokea ama? Wataalamu wa saikolojia mnasemaje hapa kwa uzoefu wenu?
 
Vijana wanaona kifo kipo mbali sana na wazi hukiona kifo kipo karibu na huogopa sana
Kifo ni jambo linajulikana kuwa kipo tu na hakiepukiki. Tena ukiwa mzee ni kama tunda lililoiva, linatarajiwa kuvunwa muda wowote. Nadhani walipaswa waishi wakijua jua limeshazama hapa muda wowote safari na hakuna cha kupoteza. Kifo inatakiwa isiwe habari ya kushtua kabisa kwao.........ajabu iliyoje wao ndio wanakiogopa mno
 
Wazee wanaogopa kwasababu wanataka waendelee kutumia mali walizotafta
 
Habari wana JF,

Katika uzoefu wangu na utafiti usio rasmi nimegundua watu wazima hasa wazee waliozeeka haswaaa, ni waoga wa kifo kuliko vijana...
Hata vijana wana ogopa pia. Kifo hakizoeleki, na hasa mtu anaweza ni wapi huko anapokwenda. Wazee kwa kuwa mwili umechoka kinga za mwili zimepungua na viungo vimechoka wao wanajiona si wa kuishi muda mrefu. Japo kifo ni siri.

Kuhusu wao kuogopa zaidi hili ni jambo jingine
 
Kifo ni jambo linajulikana kuwa kipo tu na hakiepukiki. Tena ukiwa mzee ni kama tunda lililoiva, linatarajiwa kuvunwa muda wowote. Nadhani walipaswa waishi wakijua jua limeshazama hapa muda wowote safari na hakuna cha kupoteza. Kifo inatakiwa isiwe habari ya kushtua kabisa kwao.........ajabu iliyoje wao ndio wanakiogopa mno
 
Hata vijana wana ogopa pia. Kifo hakizoeleki, na hasa mtu anaweza ni wapi huko anapokwenda. Wazee kwa kuwa mwili umechoka kinga za mwili zimepungua na viungo vimechoka wao wanajiona si wa kuishi muda mrefu. Japo kifo ni siri.

Kuhusu wao kuogopa zaidi hili ni jambo jingine
Naam, na hapo ndipo kwenye mada husika. Kwanini wao wanaogopa sana?
 
Subiri ufikishe miaka 70+ uje tena na hii thread ya kipuuzi.

Bila shaka wewe unasubiri urithi
Punguza makasiriko mzee, kwani una umri gani?

Mimi nikifika umri huo sitarajii kuogopa kufa.

Na suala la urithi halipo kichwani mwangu.

Baba yetu ana watoto 8 kwa mama tofauti na hakuwa tajiri. Tunarithi nini? Zile nyumba 3?
 
Jaribu kukaa siti ya mbele kwenye gari ya magazeti inayokwenda mwanza, ukiweza kuvumilia na kurelax ule mwendo then utaweza kuelewa wanachopitia hao wazee na kwann wanakuwa waoga.
 
Jaribu kukaa siti ya mbele kwenye gari ya magazeti inayokwenda mwanza, ukiweza kuvumilia na kurelax ule mwendo then utaweza kuelewa wanachopitia hao wazee na kwann wanakuwa waoga.
It's just a matter of psychology.
Dereva anayeendesha kila siku anawezqje?
Hata kwa wazee tatizo linaanzia vichwani mwao?
 
Kwa sababu wazee wanakuwa tayari walishajiwekeza na kujua utamu wa maisha, kwa kijana bado anakuwa anajitafuta
 
Kwa sababu wazee wanakuwa tayari walishajiwekeza na kujua utamu wa maisha, kwa kijana bado anakuwa anajitafuta
Sasa kama walishajitafuta na kujipata, kwanini wanaogopa sana kifo? Hawa hawana cha kupoteza.
 
ushawahi kukutana na Habari mbaya ya kushtua? Mshtuko wakat mwingine unaua mapema, wengi hufa kwa hofu, hofu ndio unayomuua mtu haraka, wazee wetu umri wao unaposogea picha ama habari inayomjia kichwan ni kifo, hivyo hupatwa na hofu, pengine alikuwa aishi Miaka 150lkn kwa sababu ya hofu anakataa moto
 
Back
Top Bottom