Makamba wala asizijali hizi kelele za mende
Yaani wananchi unawaita mende? Hawa wanaopiga kelele ndiyo watakuwa na kichinjio cha 2025.
Kwani hao watangulizi wake waliwekewa watu wa kuwatukana na kuwazushia kama yeye?!!!!
Kwa nini watangulizi wake hawakuwekewa watu wa kuwatukana na kuwazushia? Kwa nini yeye tu, kati ya mawaziri takribani 30 tulionao sasa, ndiye pekee awekewe watu wa kumzushia na kumtukana?
Hata huko nyuma changamoto za umeme hazikuwepo lakini kelele hazikuwa nyingi na zilifanyiwa kazi. Kulikuwa na kelele za mkataba wa Richmond, waziri mkuu akaachia ngazi. Kulikuwa na kelele za gesi ya Mtwara, waziri Mhongo akaachia ngazi. Kulikuwa na kelele ya Escrow account, waziri Ngeleja akaachia ngazi na kurejesha Tsh billioni moja aliyochotewa toka kwenye account hiyo. Kumekuwa na kelele nyingi za aina mbali mbali katika kipindi hiki cha Makamba:
- Alinunua software ya tahama kutoka Mahindra ya mabilioni ya pesa (nje ya bajeti ya serikali) badala ya kutumia watalaamu wetu wa software kama walivyofanya BoT, Mahakama na taasisi zote zingine za serikali. Inaelekea software hiyo ya mahindra ndiyo ikavuruga mfumo wa grid ya taifa. Katika katika ya umeme ikaongezeka. Sababu zilizokuwa zinatolewa kuhusu katikakatika hiyo zikawa hazieleweki na zikawa za kubadilika badilika mara kwa mara.
- Hadi mwishoni mwa mwaka 2021 uzalishaji wa umeme wa mitambo ya gesi na maji ulikuwa MW 1,605 kwa siku. Mahitaji na matumizi yetu yalikuwa hayazidi MW 1,300 kwa siku. Hivyo tulikuwa na bakaa ya zaidi ya MW 300 kila siku. Katika katika ya umeme ilipoanza tukaambiwa mifumo ya usambazaji wote umechakaa kwani ulikuwa haufanyiwi service wala maintanance kipindi chote cha awamu ya tano. Kwamba matrillion ya pesa yanahitajika kubadilisha/ kuweka mpya transformers na lines zote nchi nzima. Pesa hiyo ikatolewa na serikali. Kazi ikaanza. Walianza na Dar es Salaam, wakasema wamekamilisha na wakaendelea na mikoa mingine yote lakini walikuwa hawaonekani. Katika katika ikaongezeka. Wakasema ni ukame huko Pangani na Mji wa Mbu uliosababisha upungufu wa MW 80. Tukabaku tunajiuliza kama upungufu ni MW 80 kwa nini ile bakaa yetu ya MW 300 isitumike, imeenda wapi. Wakasema na huko Kihansi na Mtera ukame huo umefika na kusababisha uhaba wa MW 120 na hivyo jumla ya uhaba ni MW 200. Wakasahau kwamba hata kama ni kweli bado bakaa yetu ya MW 300 haijaisha, imebakia na MW 100. Wakizidi kujichanganya wakasema wamekamilisha expansion pale Kinyerezi ya MW 100. Lakini mgao ukaendelea na walishasema utaendelea hadi 2025. Funga kazi ni pale juzi Mkurugenzi Mkuu wao aliposema mahitaji yetu halisi ya umeme ni MW 60,000 kwa siku, hivyo hata huo mradi wa MW 2,115 wa JNHPP utakapokamilika mwaka 2024, mgao utaendelea hadi tutakapoweza kuzalisha MW 60,000 kwa siku.
- Halfu Januari mwenyewe alipoingia tu kwenye wizara hiyo alisema tanesco wanakusanya TSh 2 trillion kila mwezi kutokana na mauzo ya umeme. Yaani kwa mwaka ni trillion 24, zaidi ya nusu ya bajeti ya serikali. Wanaizidi TRA katika kukusanya pesa lakini matumizi ya pesa hiyo ni wao tu na board yao ndiyo wanaojua. Ilikuwa inatosha sana kugharimia mradi huo wa JNHPP na mingine mikubwa bila wasi wasi. Inatosha sana kugharimia ukarabati wa transmission system bila wasi wasi wala kelele. Lakini wanasema pesa hiyo wanayokusanya jaiwatoshi na wamepanga kuongeza bei ya umeme kuwa TSh 560 kwa unit yaani maradufu. Kwa hivyo watakuwa wanakusanya TSh 48 trillion kwa mwaka na wamepanga ku operate na wafanyabiashara binafsi katika uendeshaji as PPP ie private public partnership. Hapo sasa wananchi wataachaje kupiga kelele na kumsakama hata kumtusi huyo waziri anayewapeleka huko?