Kwanini Waziri huyu hakutoa sababu ya watangulizi wake 'kutotukanwa' sana kama anavyotukanwa yeye?

Januari sura yake tuu haifai hata kuwa Waziri,huwezi pandisha bei hovyo kwa watu maskini na magao juu
 
Hauwezi kuwa na akili ya kawaida kuandika haya , wewe ni big thinker
 
Haya madini nimeyakubali kiongozi, hii serikali ilishatuona sisi ni mazombi.
 
Sawa kiongozi, shida yetu kwa sasa sisi wengine si kuendelea kusikia tena na tena hizi taarifa maana zimejaa humu na zinatiririka kila siku na kila saa.........zilezile; mwizi, anatoa rushwa, fisadi, uwezo wake wa kitaaluma mdogo n.k.

Ikiwa tumeshasikia tuhuma hizi vya kutosha tu kuhusu yeye, naomba mtuonee huruma na mtupeleke upande mwimgine wa ushahidi wa hizo tuhuma ili nasi ambao bado hatujapata sababu ya kuwachukia watu bila sababu tupate.
 
Katika hotuba yake ndefu ya kumkaribisha raisi kwenye sherehe ya kujaza maji bwawa la Nyerere, waziri wa nishati alilalamika sana mbele ya raisi kwamba amekuwa akitukanwa sana kutokana na changamoto za wizara hiyo.
Honestly, mimi mpaka sasa sijaelewa mantiki ya waziri januari kulalamikia utukanwaji wakati yuko kwenye international audience!
Hivi mtu na akili yako timamu kweli unawezaje kusimama mbele za watu toka mataifa mbalimbali na kuanza kulalamika kuwa unatukanwa? Sijui ni utoto wa uswahilini? Sijui kujiliza ili uonewe huruma? Sijui ni kukosa hekima tu? Yani hata sielewi!
Mwanaume mzima unawezaje kwenda kulialia mbele za watu?
 
Ka video basi
 
Anajua anatukanwa sana kwa kuwa tunashinda nae hapa JF na insta ndo maana uelewa wake mpana kwenye Kutukanwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…