Nakushuru Mkuu wa kuleta mada hii. Mungu akubariki sana ndugu yangu kwa kuamsha vichwa vya wazalendo wenzako.
Mimi kusema ule ukweli sina imani kabisaa na huyu waziri. Sioni kama ni mzalendo wa kweli kama vile alivyokuwa Prof. Kabudi na naona yeye ni ile jamii ya watu ambao wanapenda sana kuwatukuza wazungu na kuwaona wao ni bora kuliko sisi (wao ni miungu mtu), I am sorry kwa kuwaza hivyo. Naomba hapa nikufafanulie kidoogo. Kama kuta kuwa na watu wenye mtazamo mwingine mbali na wangu mnaweza mkanisahihisha, kwani mimi ni siku hiyo moja tu ndiyo niliyokutana na Prof. Kabudi.
Prof. Kabudi kachukua PhD yake Ujerumani na kwa jinsi nilivyo mwona inawezekana akawa anazungumza vizuri sana kijerumani kuliko hata kiingereza. Wakati akiwa huko masomoni nina uhakika amewasoma vizuri sana wazungu na anawaelewa vizuri sana. Kwa jinsi nilivyo msoma naweza sema kuwa yeye ni kati ya watanzania wachache ambao wanaweza wakamsikiliza mzungu kwenye mazungumzo na kujua au kutambua moja kwa moja kuwa huyu ni mzungu wa aina gani na lengo lake ni lipi? Ama kweli ni watu wenye uelewa mpana sana wa binadam.
Mimi nashukuru kupata bahati ya kuketi naye kwenye mazungumzo na wasomi wengine huko Berlin nchini Ujerumani, kwangu ilikuwa ni mara ya kwanza kumsikia na kumwona, wakati huo bado akiwa Prof. wa Chuo kikuu cha DSM, akitusimulia kuhusu mambo ya muungano wetu na muungano wa wajerumani na akifafanua tofauti za faida na hasara za hizo systems mbili za muungano. Mimi sikumjua kabisaa! Na kusema kweli nilifarijika sana na darasa lake siku hiyo kiasi kwamba niliuona uzalendo wake kwa nchi yetu. Katika mazungumzo hayo nami sikuwa domant, nilihoji sana kiasi kwamba ikafika wakati akatambua kuwa mimi ni mtu wa aina gani na kwa hali hiyo naweza sema niliamsha interest katika nafsi yake kiasi kwamba ikafika wakati kila nilichokuwa nikihoji nilipata jibu ambalo nilifarijika nalo. Kuanzia hapo nilitambua uwezo wake katika kuutambua ulimwengu, kwani nami kidogo historia ya ulimwengu naipata.
Kutokana na mazungumzo yale mimi sikujisikia amani moyoni, nilijiuliza sana, kwanini watu kama hawa hawapewi madaraka makubwa ya uongozi serikalini? Namshukuru mungu alisikia kilio changu, kwani hatimaye Hayati Rais wa wanyonge Dr. JPM alimteua kuwa waziri wa sheria na katiba. Binafsi nilifarijika sana na uteuzi ule na baadae faraja ikaongezeka zaidi baada ya kusikia amekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, kwani nilitambua kuwa sasa yuko kwenye element yake. Na nafikiri hiyo ndiyo sababu iliyo mfanya hata Hayati Rais wetu mpendwa JPM kumpa uwaziri wa nchi za nje.
Prof. Kabudi ni thawabu ya watanzania kutoka kwa mungu. Watakao mkebei yeye ni kwamba kwa vile hawamjui yeye na hali halisi ya ulimwengu na mwenendo wa wazungu. Na kwa hali hiyo naweza sema tena kwamba sina uhakika kama Rais wetu wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan kweli huyu jamaa anamjua vizuri. Angemjua vizuri sidhani kama angechukua maamuzi kama hayo aliyo yachukua. Simpigii debe, ila ningewaomba kaane naye na jaribuni kumhoji maswali mazito yanayo husu ulimwengu na tabia za watu tofauti. Mtafarijika sana na kupata darasa ambalo hamtalisahau.