Kwanini 'Wazungu' hupambana sana ili Mgonjwa asife, lakini 'Waafrika' hujitahidi mno kufanya 'Maziko' ya Kifahari kwa Marehemu?

Kwanini 'Wazungu' hupambana sana ili Mgonjwa asife, lakini 'Waafrika' hujitahidi mno kufanya 'Maziko' ya Kifahari kwa Marehemu?

Wazungu hawana roho mbaya mkuu..,,wala chuki,,
Mzungu ni kiumbe pekee ambaye anaweza akapanga jambo na kuwaeleza wengine,,
Mfano anataka kusafiri,
Anataka kufanya chochote cha maendeleo ,,
Atakisema hata kabla ya mwaka mzima kufika..wakati huku kwetu Africa mambo ya maendeleo mfano kujenga,,unataka kusafiri ng'ambo nk mtu anafanya siri kuogopa roho mbaya za kichawi..
Mzungu atakusaidia sana ktk kufanya jambo la maendeleo,,wakati mwafrika ukimtajia jambo la wewe kuendelea basi elewa hutofanikiwa kwa kuwategemea wao kukusaidia,..
Mfano...pengine unahitaji msaada wa kifedha ili jambo lako liende,,unaweza kumfata jamaa au ndugu kabisa ambaye uwezo wa kukusaidia anao lakini akishajuwa unahitaji ili upige hatua ktk maisha ,,kusaidiwa ni ngumu sana,,tofauti na mtu mweupe..
Mzungu hukusukuma juu uzidi kupaa wakati mwafrika atakukandamiza uzidi kushindwa..

Mkuu hapa umemaliza kila Kitu na kama yupo Mswahili ( Mwafrika ) ambaye hajakuelewa katika hili basi Mapokezi pale Milembe Hospital ni pake.
 
Mimi huwa 'nawasindikizia' na 'Matusi' ya maana tu Mkuu ambayo najua Siku nikienda 'Mbinguni' ndiyo yatanifanya 'nichomwe' sana tu Moto huko.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani nimecheka kama mazuri, kuna mgonjwa alikuwa ananiambia hao wanavyokazana uwe unakula wameniletea chakula hapa, haaa haaa mpaka mgonjwa kaongea kwa hasira

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Wazungu hawana roho mbaya mkuu..,,wala chuki,,
Mzungu ni kiumbe pekee ambaye anaweza akapanga jambo na kuwaeleza wengine,,
Mfano anataka kusafiri,
Anataka kufanya chochote cha maendeleo ,,
Atakisema hata kabla ya mwaka mzima kufika..wakati huku kwetu Africa mambo ya maendeleo mfano kujenga,,unataka kusafiri ng'ambo nk mtu anafanya siri kuogopa roho mbaya za kichawi..
Mzungu atakusaidia sana ktk kufanya jambo la maendeleo,,wakati mwafrika ukimtajia jambo la wewe kuendelea basi elewa hutofanikiwa kwa kuwategemea wao kukusaidia,..
Mfano...pengine unahitaji msaada wa kifedha ili jambo lako liende,,unaweza kumfata jamaa au ndugu kabisa ambaye uwezo wa kukusaidia anao lakini akishajuwa unahitaji ili upige hatua ktk maisha ,,kusaidiwa ni ngumu sana,,tofauti na mtu mweupe..
Mzungu hukusukuma juu uzidi kupaa wakati mwafrika atakukandamiza uzidi kushindwa..
Yaani sie huku bara giza ukianza kufanya kitu cha maendeleo tu wanaanza kukaa mbele yako kukuziba ili usipite, halafu chakushangaza unakuta ni ndugu au watu wakaribu ambao huwezi tegemea kabisa kukuharibia, Mungu atusaidie sana.

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Mzungu akiwa na Mgonjwa wake Hospitalini atahangaika hata kwa 'Gharama' zake zote tu ili 'ayaokoe' Maisha yake 'asife' lakini kwa Mwafrika ( Mswahili ) Yeye akiwa na Mgonjwa Hospitalini wala 'hajali' kivile na pengine hata kutoa 'Huduma' au 'Msaada' anakuwa mgumu ila pale Mgonjwa 'akifa' tu ndipo utaona 'anavyojitutumua' kwa Kuchangia 'Mazishi' huku akitoa 'ahadi' za kila namna Mazishini.

Je, Ubongo wa Mzungu na Mwafrika ( Mswahili ) ni sawa au si sawa? Kuna Jambo 'nimelishuhudia' leo na Kuthibitisha kuwa Waafrika tuna Majanga.
Hili ni janga!
-mgonjwa utakuta kalalia matambara hana hata Shuka ila akishakata roho shuka zuri litapatikana,suti atavalishwa,mashada ya bei mbaya,jeneza la kifahari n.k.Ninao mfano Bibi kizee mmoja alikataa kufanyiwa mazishi ya mbwembwe baada ya kuona watu wake hawakumjali wakati akiwa hai.Kwa ufupi ulimbukeni,kukosa utu na kutaka sifa ni sababu kubwa hasa.
 
Waafrika hasa Sisi 'Waswahili' tuna matatizo makubwa mno ya 'Akili' yaani Mgonjwa akiumwa hatuchangii ila akifa ndiyo tunatafuta Sifa tu Misibani.
Msiba unaingiza pesa kwa wafiwa kupitia. Rambirambi wakati mgonjwa pesa inaondoka mifukoni mwa waaouguza mtu lazima apende mazishi kuliko kuuguza!!!!!!!
 
Huku africa Kuna ujinga mwingi,huoni wanaojaa hata makanisani ni wachawi,wahuni,husda lakini hawakauki Wala kubadilika kitabia ili waje wazikwe vizuri,hili liko Hadi kwenye kuchangiana harusi nk nk
 
Yaani sie huku bara giza ukianza kufanya kitu cha maendeleo tu wanaanza kukaa mbele yako kukuziba ili usipite, halafu chakushangaza unakuta ni ndugu au watu wakaribu ambao huwezi tegemea kabisa kukuharibia, Mungu atusaidie sana.

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa mkuu,,
Ukitaka jambo lako lisifanikiwe basi litangaze mapema kabla ya kulitimiza,,haliwezi kuwa kamwe.
Wakati wenzetu wazungu mipango yao inakuwa wazi kabisa ktk kila jambo lao.
Kweli Africa ni bara la giza.
 
Africa is the place love the died,they celebrate when you die ,they hate when you live.
 
Huenda waliokuwa sawa walipokuwa wanawachapa mababu zetu. Mf. Unaambiwa nawa mikono kwa sabuni, akikugeuzia kisogo tu hutumii sabuni, sasa usichapwe? Kulingana na swali lako huenda akili za Waafrika zipo chini sana.
 
Mzungu akiwa na Mgonjwa wake Hospitalini atahangaika hata kwa 'Gharama' zake zote tu ili 'ayaokoe' Maisha yake 'asife' lakini kwa Mwafrika ( Mswahili ) Yeye akiwa na Mgonjwa Hospitalini wala 'hajali' kivile na pengine hata kutoa 'Huduma' au 'Msaada' anakuwa mgumu ila pale Mgonjwa 'akifa' tu ndipo utaona 'anavyojitutumua' kwa Kuchangia 'Mazishi' huku akitoa 'ahadi' za kila namna Mazishini.

Je, Ubongo wa Mzungu na Mwafrika ( Mswahili ) ni sawa au si sawa? Kuna Jambo 'nimelishuhudia' leo na Kuthibitisha kuwa Waafrika tuna Majanga.
Kwa sababu Waswahili hatuna akili
 
Swali zuri sana.

mimi huwa nakereka sana watu wanafanya misiba kama bonanza!!
Hapana mkuu. Kila mtu afanye jambo kulingana na hali yake ya uchumi. Watu hatufanani hata siku moja. Mungu ibariki Tanzania.
 
Waafrika hasa Sisi 'Waswahili' tuna matatizo makubwa mno ya 'Akili' yaani Mgonjwa akiumwa hatuchangii ila akifa ndiyo tunatafuta Sifa tu Misibani.
Inawezekana mgonjwa alikuwa anaumwa lakini Kuna baadhi ya ndugu, jamaa au rafiki hawakuwa na taarifa. Wengine wanaumwa ndani ya siku tatu kisha wanafariki.
 
Mkuu tatizo letu ni roho mbaya ,,
Mgonjwa anaweza akafa kwa kukosa Dawa ya malaria ya 3000 ,,lakini siku akifa yule yule aliyemnyima pesa ya kununuwa dawa atagharamia hata millions kwenye mazishi .
Mkuu, vp kama aliyeombwa pesa alikuwa hana kwa wakati huo? Mkuu, hawa watu wa high class kuna kipindi na wao wanakuwa hawana kwa sababu ya majukumu (ada za watoto, projects za ujenzi, kuombwa msaada na watu wengi, etc)
 
Yaani 'hakyanani' isingekuwa ni huu mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 ambapo nimepanga 'Kura' zangu zote niwape John Magufuli na Tundu Lissu kwa 'upamoja' Wao, kuna Mtu angenipeleka Segadansi ( Jela ) kwa 'Kipondo' ambacho ningempa kwa 'Unafiki' wake. Tokea Mgonjwa wao 'augue' huu ni mwaka wa Tano ( 5 ) hajawahi 'Kuchangia' chochote kile na hata alipokuwa akipigiwa Simu na 'Nduguze' kutoa 'Mchago' wake alikuwa hapokei leo 'Mgonjwa' Israeli 'ameshamtwaa' ndiyo 'anajitutumua' Kuchangia 'Pesa' na Kutoa 'Huduma' Msibani Kwao.
Vp kama na yeye alikuwa hana pesa kwa wakati huo? Angechangia nini sasa mkuu?
 
Back
Top Bottom