Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Nimebahatika kuishi na kufanya kazi na wazungu. Kwa kweli licha ya neema ya chakula waliyo nayo wazungu ni wachoyo mno wa chakula.
Nilijifunza kusema hapana asante hata kwa kikombe cha chai. Hasa uingie ndani ya nyumba uwakute wanakula ilhali hawajakualika kwa chakula.
Huku kwetu Kwamtogole mgeni akiingia wakati mnakula atakaribishwa mezani. Kama ugali hautoshi, mama ataenda jikoni kimya kimya kupika ugali mwingine.
Hii issue ilikuwa inanikera kama jiko ni la kuni na kuni si kavu kivile. Moto utakusumbua sana kuivisha ugali wa ziada.
Haya nimeyaona sana Ulaya sifahamu tabia za Wamarekani.