Watu na bajet zao kimjini zaidi.
Nakumbuka nyumbani kijijini huwezi kwenda ukakuta eti watu wamekula chakula kimeisha? Haijawahi tokea.
Wakipika chakula cha mchana lazima waongeze cha ngeni ambae atajitokeza pia na cha watoto watakachokula mida ya jioni kabla ya chakula cha usiku.
Haya maisha ndo nilikulia mimi. Umenikumbusha mbali.nyumbani chakula hakiishagi.
Ikitokea kikaisha mgeni akiingia tu fasta ashapikiwa.
Nirudi kwenye mada waafrika tuna tamaduni tofauti na wenzetu.
Wakati tunakuwa mama alinifundisha hivi, kamwe nisimyime mtu chakula hata kama hajaniomba.
Pili mgeni asitoke ndani bila kula chochote, yaan mlazimishe hata maji au chai.
Wazungu ndivyo walivyo.inabidi kuwazoea tu hakuna namna.najua sio wote wengine wakarim saana
Wakijaga kwetu ni tofauti yaani kama ofisin wakifika tu nawaandalia chai msosi na ni watu wa kushukuru sana, yaan hizo care unazompa, karibu chai ,msosi wanazithamini sana anaweza kushukuru nusu saa. Afu akirudi africa anakuletea mdoliiiiiiii snacks etc.ahaaa
Mm ambao nimekutana nao sio wachoyo.