Kwanini wazungu ni wachoyo wa chakula?


Waswahili wenyewe hawa ambao hata ukimkuta kabakisha vijiko viwili vya chakula haoni aibu kujibaraguza karibu chakula?
 
Ulishasema wewe kwenu ni kwa mtogole huko ambako mnaishi ishi tu bila mpangilio wowote lazima uwaone wazungu wachoyo.

Nakumbuka nilipanga sehemu moja uswahilini eti siku wakitembelewa na mgeni wanaenda kukopa kuku na mchele hili wampikie mgeni chakula kizuri, halafu huyo mgeni akiamsha wanabaki wana angaika na madeni,, hahahaha... nafikiri mleta mada utakuwa utatoka kwenye jamii za namna hii.
 
Waswahili wenyewe hawa ambao hata ukimkuta kabakisha vijiko viwili vya chakula haoni aibu kujibaraguza karibu chakula?

So maana yake ni kwamba they don’t really mean it, siyo?

Anasema tu hivyo kama kinga ya kuja kutosemwa baadaye kuwa yeye si mchoyo, siyo? Kwa sababu tu alikukaribisha chakula...

Hahahaaaaa.
 
So maana yake ni kwamba they don’t really mean it, siyo?

Anasema tu hivyo kama kinga ya kuja kutosemwa baadaye kuwa yeye si mchoyo, siyo? Kwa sababu tu alikukaribisha chakula...

Hahahaaaaa.

Hiyo ni zaidi ya uchoyo, imekaa kinafiki zaidi.
Ukiniambia tu umekuja wakati mbaya ndio tunamaliza chakula kuna tatizo?
 
Ni kweli mkuu, tena hata vilema ukiwapisha kwenye foleni hawapendi. Wanataka wasubiri kama wengine
Hata maboss hawanaga makeke kama ya Devid wa bongo, yaani maboss akufokee kama Devi anavyofoka hapana aiseee
 
Si Wazungu tu hata Kenya Hapo tu, mi nadhani ni vile watu wanajali muda bana....sasa we unaacha kula uende kwenye miste zingine unaanza kuhangaika kuwasha kuni/mkaa upike ugali wa mgeni ambae hata hajakwambia anakuja..Tubadirike.
 
Ndio wabongo ata akikukuta bar anataka umnunulie otherwise atakuita mchoyo na mbinafsi na akigundua una pesa benki anataka ukatoe zote mnywe bia mpaka ziishe ndio atakuona mkarim na rafiki wa kweli eti anakuita jamaa yangu

Ila maendeleo yatatufundisha tuu awamu ya tano tumechange kidogo mtu ukienda bar huendi tena na laki mbili ili kuzungusha round unaishi kwa budget unachukua ka elf kumi kako unaenda kwenye ki pub tu tena maeneo ya nyumbani huitaji hata bodaboda bia zako tatu na mishkaki mitatu unarud kulala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijijini? Mi kwangu bora hata watu wa mjini asee!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mzee mama, watu wa kijijini sio wanafiki kama mjini yaaani hapa namaanisha kijijini kule interior kabisa na sio Kyabakali hapo. Watu wa kijijini wakikukaribisha kula ujue wanamaanisha na sio pretense tofauti na mjini ambapo mtu kwanza anakukaribisha baada ya kufahamu kwamba umemuona na anasema karibu huku moyoni amekuja ndita akitamani usije...
 
Mhhhhh, dunia kweli imebadilika sana maana watanzania hatukuwaga hivi kabisa!
 
Ebwanaa eeeh, This is modern Africa!
Hivi una uhakika na unachokisema hapa mkuu ???
Nijuavyo mimi matajiri haswaa huwa siyo wachoyo wa chakula kabisa hata siku moja.
 
Watu na bajet zao kimjini zaidi.

Nakumbuka nyumbani kijijini huwezi kwenda ukakuta eti watu wamekula chakula kimeisha? Haijawahi tokea.
Wakipika chakula cha mchana lazima waongeze cha ngeni ambae atajitokeza pia na cha watoto watakachokula mida ya jioni kabla ya chakula cha usiku.

Haya maisha ndo nilikulia mimi. Umenikumbusha mbali.nyumbani chakula hakiishagi.

Ikitokea kikaisha mgeni akiingia tu fasta ashapikiwa.

Nirudi kwenye mada waafrika tuna tamaduni tofauti na wenzetu.

Wakati tunakuwa mama alinifundisha hivi, kamwe nisimyime mtu chakula hata kama hajaniomba.

Pili mgeni asitoke ndani bila kula chochote, yaan mlazimishe hata maji au chai.
Wazungu ndivyo walivyo.inabidi kuwazoea tu hakuna namna.najua sio wote wengine wakarim saana

Wakijaga kwetu ni tofauti yaani kama ofisin wakifika tu nawaandalia chai msosi na ni watu wa kushukuru sana, yaan hizo care unazompa, karibu chai ,msosi wanazithamini sana anaweza kushukuru nusu saa. Afu akirudi africa anakuletea mdoliiiiiiii snacks etc.ahaaa

Mm ambao nimekutana nao sio wachoyo.
 
Na wanatarajia utakua umeshiba, hauwezi ukawa unazurura bila kujua mambo yako yamekaaje na utajimudu vipi.
hahahaha hii comment imenifanya nijisikie vizuri,kuna mtu mtu natamani apitie hapa aone..
 
Kama wavimba macho tu... Japo wao wana kaunafiki wakibweep karibu ukala utaona watakavyotunisha mashavu

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…