Kwanini Wazungu walivamia Bara la Amerika kabla ya Afrika?

Kwasabu amerika kulikua na mali nyingi ukilinganisha na afrika. Ukianzia madini mpaka ardhi yenye rutuba
 
Kwasabu amerika kulikua na mali nyingi ukilinganisha na afrika. Ukianzia madini mpaka ardhi yenye rutuba
 
Historia ya Africa na dunia kwa ujumla sio ile tunayoisoma darasani.Historia ya dunia imefichwa na inaonekana kwa uchache kupitia kivuli kinachoitwa "Conspiracy theories".

Wazungu wameanza kuja Africa miaka mingi kabla ya kristo.Na waafrica wengi wamesafiri sehemu mbalimbali za dunia mfano America ya kusini, kabla ya kinachodaiwa kuja kwa wazungu Africa kupitia wakina Vasco Da Garma, Bathlememew Diaz etc.
 
Maono yako ni kweli.Ni kweli huwezi taka kwenda kufika sehemu mfano eti kununua chumvi na ujue fika kuwa ni sehemu flani bila ya flani kufika.Kihistoria ni hivi kutoka bara la ulaya kwenda India kwa ardhi tu unaweza fika kabisa.Habari za India zilisambaa kirahasi kutokana na dini za ukristo na uslamu zilivoingia katika usambazaji wake ndio baadhi ya sehemu maarufu zikajulikana.Pia vita ni moja ya sababu ya kusambaa kwa habari kutokana na madola mengine miaka hiyo kutaka kujipanua.Mfano mfalme wa Mongolia Geghis Khan pamoja na kwamba Mongolia ni mbali sana lakini majeshi yake yalijaribu kuchukua himaya za nchi nyingi sana za mpaka bara la Ulaya mpaka nchi za Cheksovakia na Norway njia zote hizi zilisababisha habari kusambaa.Sasa je ni kwanini walichagua njia ya maji kutafuta India? Kumbuka hawa walikuwa ni explorers walitumwa na wafalme wa nchi zao kwa ajili ya sababu za kibiashara tu.Hata wewe ndugu yangu ukinunua marobota ya pamba Mwanza ukawa unataka kuyapeleka Dar kwa kupitia njia ya Mwanza-Singida-Dodoma-Morogoro-Dar lakini ukaambiwa kuna uharamia wa kutekwa njia hiyo lakini ukitumia njia ya Mwanza-Singida-Arusha-Moshi-Dar hiyo shida haipo lazima utachagua njia hii japo ni ndefu sana.Sababu ingine zamani walikuwa wanajua kuwa dunia ni kama sahani ukienda kuna mahali utaporomoka sasa uelewa kidogo ulishaanza kuingia taratibu kuwa dunia ni mviringo hivo hata wakienda ndani ya vyombo vya maji kuna uwezekano wa kuizunguka na kutokea sehemu ingine
 


Lkn mbona hatuwaoni? Nilichomaanisha ni kwamba ni kwa nini waliamua kuvamia na kuishi Bara la Amerika kabla ya Afrika ilihali waliijua Afrika kabla? Yaani kwa nini waliamua kuja kuchukuwa Makoloni Afrika baadaye sana baada ya kuwa tayari walishajimilikisha Bara la Amerika?
 


Lkn swali langu ni kwamba kwa nini Wazungu waliamua kutawala na kuhamia Bara la Amerika kabla ya Afrika ingawaje walilijua Bara la Afrika kabla ya Bara la Amerika?
 
Tupo pamoja mzee meko
Msalimie sokomoko, mwambie aache kujificha.

Hahaaaaaa
 
Lkn swali langu ni kwamba kwa nini Wazungu waliamua kutawala na kuhamia Bara la Amerika kabla ya Afrika ingawaje walilijua Bara la Afrika kabla ya Bara la Amerika?
Wajuzi washasema kwamba, Kule america

1. Hakukuwa na resistance kama ilivyokuwa afrika. Huku kwetu tayari kulikuwa na tawala zenye nguvu, so haikuwa rahisi kuingia na kuchukua maeneo kama kule america ambapo kulikuwa na watu wavivu na wasiojitambua

2. Kule america kulikuwa ma ardhi yenye rutuba sana kuliko afrika, na pia Mali zingine nyingi kama madini
 
Aliyevumbua America ni Mtaliano Amerigo Vespucci. Lengo lao ninkuipata njia rahisi kufika India kunako karne ya 15 kwa ajili ya viungo vya chakula spices na dhahabu. Walipofika Amerika wakakuta wenyeji wakidhani ndio wa India na kuwaita Indians wakati siwo.

Ila Afrika walishaijua kitambo kabla.
 


Labda namba 2 naweza kukubaliana nayo lkn siyo namba 1, kwani Bara la Amerika lilikuwa na advanced civilization klk kwetu Afrika, kama ulishawahi kusikia kuhusu Maya Civilization ambapo walikuwa na kila kitu hata kuna mapiramidi walijenga kama ya Misri, hivyo siwezi kuamini kwamba sisi tulikuwa na Jeshi imara klk la Maya people kuweza kuwatisha Wazungu waliokuwa na vifaa vya kisasa vya kivita!

Piramidi za Maya Civilization

walijenga haya Majengo kwenye karne ya 7

Hii ilikuwa nyumba ya Kiongozi wao au Ikulu karne ya 7 huko kabla Muzungu hajatia mguu, waliweza kujenga majengo kama haya











Angalia hilo jengo na hizo ngazi, watu wa Maya walijenga kwenye karne ya 6/7 huko, sasa sidhani kama waliweza kujenga haya majengo karne ya 6/7 walishindwa kuwa na Jeshi imara klk sisi!
 


Lkn kwa nini sasa Wazungu hawakuchagua kuja Afrika badala yake wakaenda Amerika ukichukulia kama ulivyosema walikuwa wanalijua Bara la Afrika tangu zamani sana lkn hawakuja mpaka baadaye sana wakati walikuwa wameshajijenga huko Amerika!

Kwa mfano Wazungu walifika TZ yetu ya leo kwenye miaka 1890 lkn tayari kulikuwa na nchi ya USA, Kanada, Mexiko, Argentina, Brazili n.k. sasa kwa nini ndicho nilichopenda kufahamu!
 
Dark father

Kwa hiyo unamaanisha huko Asia hawakuwa weupe kabla ya hao wa ulaya kuvamia sio.

Walikuwa ni wa rangi gani then
Sijui ntakuwa nimekuelewa?

Kwanza mtu mweupe ni yule mwenye 'original' european descent. Yaan Mweupe wa ulaya. Hivyo ndivyo inavyotambulika kimataifa.

Pili, waliokuwepo asia ni hawa waliopo sasa hivi kwa kiasi kikubwa, i.e. Chinese-like, arabs na indians.
Tukizungumzia east asia wengi ni Chinese-like and indians.

Hivyo weupe hao waliwakuta watu wa aina hiyo huko asia.
 

Ni suala la nyakati tu. Ni kama sasa wanakuja kama ACACIA
 
Kabisa mkuu. You really know history. Naheshimu sana watu wanaotoa maelezo in detail na kwa facts.

Nikiwa na maswali zaidi ntakuchek; coz im always learning.

Shukran
 
Walivamia huko sababu ya Miti, walihitaji sana miti kwa ajili ya ujenzi wa Europe. Afrika haikuwa na miti mikubwa na mingi kama huko.
 
Kabisa mkuu. You really know history. Naheshimu sana watu wanaotoa maelezo in detail na kwa facts.

Nikiwa na maswali zaidi ntakuchek; coz im always learning.

Shukran
Barbosa alitoa mada nzuri na wewe ulijitahidi sana kutoa majibu mazuri ya ukweli kabisa nikaona niingie deep kukupa tough na kukupongeza karibu tuko pamoja
 
Walishafika huko,walichokuwa wanatafuta ni shortcut ya kuweza kwenda na kurudi kwa urahisi.
 
Dunia imeanza zamani sana, hakuna jipya chini ya jua. Kama hujui unaweza kudhani ndio imeanza juzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…