Kwanini Wazungu walivamia Bara la Amerika kabla ya Afrika?

Kwanini Wazungu walivamia Bara la Amerika kabla ya Afrika?

Ila hili la kuitafuta Asia kidogo linanichanganya.

Ilikuwaje hao wazungu wa ulaya wajue kwamba huko Asia na India kulikuwa na biashara na viungo, bila kujua mahali kwenyewe palipo na jinsi ya kufika.

Coz hao walioleta taarifa hizo nilitaraji wawe na ufahamu wa eneo husika lllipo na njia za kufika.

Ulaya na Asia zimeungana hakuna hata bahari, sasa iweje wavuke maji kwenda America ambako ni uelekeo tofauti kabisa.

Mm nadhani hao wazungu walikuwa washafika hiko India na asia tayari, ndio wakaanza kupuyanga kwingine wakikata maji waone hayo maji yatawafikisha wapi, ndio wakajikuta huko America.

Ni fikra zangu kulingana na jinsi nionavyo,
Ni kweli kuwa ulaya na Asia vimeungana Kwa nchi kavu,lakin ukumbuke katikati ya mabara haya kuna safu za milima Himalaya ambazo zimakava kama nchi tano kama siyo sita au saba ambazo baadhi zipo ulaya na nyingine zipo Asia,Kwa hiyo hizo safar za kutoka ulaya na kwenda Asia moja Kwa moja ziliwachukua mda mrefu na walikumbana na kashi kashi nyingi njiani Kwa sababu ya milima Himalaya
Kwa hiyo ili kuepuka ugumu huo iliwabidi waopt kutumia bara la Africa ili wafike Asia,
Lakin kupitia Africa pia nilikuwa na vikwazo vingi sana vikiwemo uwepo wa dola imara za waafrika,pia baada ya kumaliza kutembea kupitia nchi kavu ya afrika,iliwabidi tena watumie usafir mwingine wa majini kuwapeleka hiyo Asia mashariki,hapo garama ikawa kubwa sana

Sasa suluhisho LA yote hayo ni kutafuta njia ya majini ya kutoka ulaya na kufika moja Kwa moja huko Asia mashariki bila kikwazo kutoka jamii yoyote,so the Atlantic ocean ikawa ndiyo suluhisho

Sasa kupatikana Kwa America ilikuwa ni accidentally, na walipofahamu pale siyo Asia,iliwabidi wafanye america kuwa kituo chao cha kupumzikia wakat wanatoka ulaya kwenda Asia mashariki na baadhi yao wakaweka makaz
 
Lkn kwa nini Wazungu hawakuhamia Afrika kama walivyohamia wote Bara la Amerika? Ndiyo swali langu, kwani Ukoloni wa Kizungu huku kwetu umekuja baadaye sana ingawaje Wazungu walilijua Bara la Afrika kabla hata ya kulijua Bara la Amerika, sasa kwa nini ukoloni ukachelewa na kuamua kuja baadaye?
Mkuu wazungu walishahamia africa especialy north miaka mingi sana kabla na baada ya yesu kuanzia Wagiriki,Warumi,Vandals na phoenicians.Alexander the great wa wa wagiriki wa macodon empire alianzisha mji mpya pale egypt mji wa Alexandria kwenye mwaka 331BC ambao upo mpaka leo.Ukoloni wa bara africa na wazungu uligawanyika awamu mbili hyo unayoifahamu wewe ni awamu ya pili.
 
Labda namba 2 naweza kukubaliana nayo lkn siyo namba 1, kwani Bara la Amerika lilikuwa na advanced civilization klk kwetu Afrika, kama ulishawahi kusikia kuhusu Maya Civilization ambapo walikuwa na kila kitu hata kuna mapiramidi walijenga kama ya Misri, hivyo siwezi kuamini kwamba sisi tulikuwa na Jeshi imara klk la Maya people kuweza kuwatisha Wazungu waliokuwa na vifaa vya kisasa vya kivita!

Piramidi za Maya Civilization

walijenga haya Majengo kwenye karne ya 7

Hii ilikuwa nyumba ya Kiongozi wao au Ikulu karne ya 7 huko kabla Muzungu hajatia mguu, waliweza kujenga majengo kama haya
Uxmal_38.jpg

1920px-Templo_de_las_inscripciones.jpg

Chichen_Itza_pyramid.jpg

Angalia hilo jengo na hizo ngazi, watu wa Maya walijenga kwenye karne ya 6/7 huko, sasa sidhani kama waliweza kujenga haya majengo karne ya 6/7 walishindwa kuwa na Jeshi imara klk sisi!
1920px-Zacuelu2.jpg
Kilichowamaliza mayans pamoja na civilizations nyengine zilizokuwako katika mabara ya amerika ni Magonjwa ya mlipuko,yaliyoletwa na wageni,magonjwa ambayo hayakuwapo kwao na hawakuwa na immunity nayo,pia silaha ziluzotumiwa na wavamizi wa kizungu zilikuwa more advanced kuliko za kwao
 
Nasoma comment tu ila ubishi huu uwe na trusted source tu
 
Mkuu wazungu walishahamia africa especialy north miaka mingi sana kabla na baada ya yesu kuanzia Wagiriki,Warumi,Vandals na phoenicians.Alexander the great wa wa wagiriki wa macodon empire alianzisha mji mpya pale egypt mji wa Alexandria kwenye mwaka 331BC ambao upo mpaka leo.Ukoloni wa bara africa na wazungu uligawanyika awamu mbili hyo unayoifahamu wewe ni awamu ya pili.

Labda sikuweza kuelezea vizuri, nilichomaanisha ni Afrika ya kwetu huku yaani Kusini mwa Sahara, nafahamu khs Afrika ya Kaskazini lkn nilikuwa naongelea Ukoloni wa Wazungu Afrika ya kwetu kwamba kwa nini ilichelewa sana?
 
Kwasababu ngozi yao ilitaka barid sio africa walibabuka kwa joto na kula vumbi

Swissme
Bara la Amerika yaani Latin America kutokea Mexico (na hata Kusini mwa Marekani - New Mexico, Texas, California, Louisiana na Florida) hadi Argentina kuna joto kali kama ilivyo Bara la Afrika. Kinachotofautisha ni kwamba: Wa-Iberians (Spaniards na Portuguese) ambayo yalikuwa Mataifa makubwa Ulaya kuanzia Karne ya 15 - 17, walikuwa wakichimba silver barani Amerika ambayo ilikuwa na thamani kubwa kama exchange currency barani Ulaya. Vilevile, walihitaji sana sugar hivyo walianzisha mashamba ya miwa Caribbean na Brazil.
Aidha, America hakukuwepo magonjwa hatari kwao kama malaria, yellow fever na trypanosomiasis (sleeping sickness), ambayo ni endemic kwetu sisi waafrika. Kwa Amerika, wazungu walipokuwa wakienda huko, Red Indians wengi walikufa na hivyo kuwalazimu wazungu kuanza kuja Afrika kuchukua watumwa kwa ajili ya kureplace wahindi waliokufa kwa magonjwa ya wazungu na kazi ngumu za sulubu.
Hivyo mtaona kwamba wakati wazungu walipokuja Afrika, wao ndio walikufa lakini walipikwenda America, waliwawaua wahindi wekundu, so kukawepo vacuum kubwa na maeneo kuwa empty. Hivyo wakati wazungu wa kilatini (Wareno na Wahispania) wanahamia Latin Amerika Karne ya 16 - 17 na kufuatiwa na uhamiaji mkubwa wa Teutonic races - whites (Waingereza, Wafaransa, Wajerumani na Nordic) katika Karne ya 18 - 19, ulipelekea Wazungu wengi kuvutika na kwenda kwenye Bara hilo. Hizo stage ndizo ziliitwa Mercantilism - commercial capitalism (Walatino) na Industrial - Competitive capitalism (Whites - Teutons).
Hata hivyo, wazungu walipohamua kukomesha biashara ya utumwa, tayari Uingereza ilikuwa imeshakomaa kwenye industrial revolution tangu 1780s na kufuatiwa na Ufaransa na Ubelgiji in 1840s na Ujerumani na Marekani in 1860s, ndipo waliamua kuja Afrika kutafuta raw materials - refer Monopoly Capitalism (imperialism & colonialism).
 
Ingawaje Wazungu waliijua Afrika kwa miaka mingi kabla ya Columbus kugundua Bara la Amerika, lkn Wazungu hawakuja Afrika kwanza mpaka baadaye sana badala yake wakaenda Bara la Amerika (Leo hii USA, Kanada, Mexiko, Argentina, Venezuela, Brazili, Chile n.k.)sasa kwa nini hawakuja Afrika kwanza?
Kwa sababu za kiintelijensia yao kipindi hicho.

(explorers)
 
Wazungu walianza kuja Afrika kabla ya America rejea utawala wa wagiriki Egypt baadae utawala wa waroma Egypt hapo ni kabla ya kristo
 
Wazungu walianza kuja Afrika kabla ya America rejea utawala wa wagiriki Egypt baadae utawala wa waroma Egypt hapo ni kabla ya kristo

Sikumaanisha Afrika ya Kaskazini bali Afrika ya kwetu huku Kusini mwa Sahara!
 
Lengo lilikuwa kufika india na east asia kiujumla.

Chukua atlas hapo utanielewa kwa jinsi gani ingekuwa ni mbali sana kupitia nchi kavu, ukizingatia usafiri ulikuwa ni mgumu, pia njiani kulikuwa na maadui wengi wa kiutawala kutoka falme na nchi zingine.

Proposal hiyo ya Columbus ilikuwa ni kuzunguka kupitia atlantic ili kutokea upande wa pili (hapa ni baada ya watu kuwa na uelewa wa kwamba dunia ni duara).

Tatizo hapa ilikuwa hakuna ajuaye kuwa kuna bara jingine upande huo, hivyo wali-assume wangefika asia ya mashariki moja kwa moja.

Ila ndo hivyo, baada ya muda mrefu wa safari, wakatia nanga katika bara wasiolijua (america).
Waliwakuta wenyeji, i.e. wahindi wekundu wakawaua kibao. Kiufupi ni kwamba wakatwaa ni kwao. Baada ya feedback kurudi ulaya, na mataifa mengine yakafuata. Hivyo america ikawa ni territory ya watu weupe.

Additionally, kwa nini east asia? - ni kwa sababu kulikuwa na biashara 'iliyochangamka' zaidi ukizingatia kulikuwa falme/mataifa tajiri, civilized yenye maendeleo.

Cha kukumbuka tu, ni kwamba origin ya watu weupe kiujumla ni ulaya. Huko kwingine ni kwa sababu walivamia tu.

Hivyo, kama afrika ilivyofanywa, ndivyo amerika ilifanywa hivyo hivyo.

Nchi za asia ilishindikana kwa sababu tayari wenyeji walikuwa na maendeleo yao binafsi including silaha.
Lakini, bado waliziweza nchi kadhaa kuzitawala, ingawa mwisho wa siku walipinduliwa tena.
Hii ndio maana asia wanajiamini na tamaduni zao.

Kwa hiyo, simply, Amerika ilipatikana by accident. Lakini mwisho wa siku walifanya scrambling na patition kama Afrika.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app

The dark father maelezo mazuri ahsante
Ni hivi kuna explorer mmoja alikuwa anaitwa Amerigo Vespucci alizaliwa katika mji wa Florence Italy tarehe 9 March 1450.Alifanya safari yake ya kwanza tarehe 10 May 1494 kwenda kujaribu kutafuta njia ya kwenda bara la Asia.Safari yake ya tatu alifanya akafanikiwa kufika Rio de Jeneiro nchi ya Argentina ya sasa.
Alipokuta nchi hii akagundua sio nchi ya Asia akaipa jina la dunia mpya habari za bara hili akizirudisha kwa mfalme wa Ureno wakati huo ambayo ndio alikuwa mfadhili wa safari yake hiyo.
Mnamo mwaka 1507 hiyo dunia mpya ikapewa heshima yake na kuitwa AMERICA kulingana na jina lake Amerigo.Hata hivo ilikuja kugundulika baadaye na Christopher Columbus au Cristobal Columbus kuwa kumbe kuna bara lingine liko kaskazini ambalo ndio bara la Amerika kaskazini
Bahati wenyeji waliowakuta kule hawakuwa wakorofi walikuwa ni wahindi wekundu ambao kiasili walikuwa ni wafugaji na wavivu.Ikumbukwe lengo lao kuu lilikuwa kutafuta njia ya kwenda India kununua viungo maana tawala za nchi za Asia zilikuwa simeendelea sana kibiashara na zilikuwa na tawala zenye nguvu.Walivoona mabara hayo mapya waliyoyakuta yalikuwa na rutuba sana na hali ya hewa ilikuwa sawa na kwao ndio mkakati wa kuhamia Amerika ukaanza taratibu.
Wahindi wekundu wa Amerika wanavoitwa vile kiukweli sio wahindi ila kwasababu shida yao ilikuwa kufika India kwa mara ya kwanza walidhani wamefika wakawapachika jina hilo kwa makosa na walikuwa ni wekundu na ni wekundu hadi leo
Amerigo Vespucci alifariki tarehe 22 feb 1552 katika mji wa Seville katika nchi ya Uhispani
Majibu mazuri
 
Mtoa mada swali lako hauko sahihi wazungu walianza afrika kwanza ndiyo wakaenda Amerika na Asia

Biashara za waafrika na wazungu zilianza toka kuanguka Kwa roman empire karne ya 4 hapa kila taifa lilitafuta malighafi kivyake mfano Chao jukua alikuwa ni mchina aliyefanya biashara za nje ya China kupitia bahari ya Hindi mwaka 859 karne ya 8

Waarubu walianza kuingia afrika kupitia ukanda wa bahari ya Hindi na kufanya biashara na wenyeji wa mwambao wa bahari ya Hindi ,hii ilikuwa ni karne ya 6 na baadae wakafuatiwa na wareno karne ya 8

Spain walifanya biashara na mataifa ya north afrika kama Morocco Egypt karne ya 5 kipindi cha ngome ya fitamids na hapa Egypt walipitia slavery mode of production ,system ya uzalishaji Mali ambayo ilikuwa hata ulaya kipindi cha roman empire kabla ya kuanguka karne ya 4

Portuguese hawa watu waliingia mapema sana south afrika na wakasettle cape town wakifuatiwa na Dutch 1456s

Wazungu hawakulivamia bara LA america sehemu walizokuwa wanafikia hazikuwa zikikaliwa na watu na red indies wakazi wa america walikuwa ni wachache sana wengi walikuwa ni wavivu !.katika historia hakuna sehemu inayo onyesha resistance Kwa walowezi Kwa wazawa wa america hii ni kutokana kwamba hata neno amerika ni limetajwa na navigator wa kipindi hicho

The discovery of new word by Christopher Columbus ,Christoforo Colombo ,Cristobal colon 1492

Hayo yote ni majina ya navigator cristo katika kuligundua bara LA amerika sasa tukiangalia mwaka lilipogunduliwa hilo bara utaona kwamba afrika ndo bara pekee ambalo wageni walipata kulitembelea Kwa muda mrefu kuliko amerika
Aliyegundua Amerika aliitwa Amerigo Vespuci na ndio jina Amerika likapatikana
 
Back
Top Bottom