Kwanini website ya Tume/Sekretarieti ya ajira Tanzania (TPSRS) haipo kwenye freebasics.com ili kuwasaidia graduates wenye vipato vidogo?

Kwanini website ya Tume/Sekretarieti ya ajira Tanzania (TPSRS) haipo kwenye freebasics.com ili kuwasaidia graduates wenye vipato vidogo?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini website ya tume/sekretarieti ya ajira Tanzania(TPSRS) haipo kwenye freebasics.com ili kuwasaidia graduates wengi wasio na vipato?

Click here>>> Free Basics

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba kuna kijana mmoja ni jirani yangu (jina simtaji) hapa Mbagala ninapokaa alihitimu chuo kikuu UDSM mwaka jana wa 2019 na hana kipato cha kumuwezesha kwenda internet cafe au hata kuweka bando la data la mara kwa mara ili kuweza kuangalia fursa za ajira mitandaoni.

Kama JamiiForums inawajali watu wa vipato vya hali ya chini na kuamua kuwepo freebasics.com, kwanini tume ya ajira inashindwa kuwajali graduates "fresh from school" ambao ni watoto wa wanyonge/wakulima?

Kwani hii freebasics.com ni nini haswa?
==========
Free Basics provides people with access to useful services on their mobile phones in markets where internet access may be less affordable.

The websites are available for free without data charges, and include content on things like news, employment, health, education and local information.

By introducing people to the benefits of the internet through these websites, we hope to bring more people online and help improve their lives.
==========

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hivi free basics inafungua mafile ya PDF?
 
Hivi free basics inafungua mafile ya PDF?
Graduate akipata clue kupitia freebasics, sasa ndio analipa pesa kidogo anaenda internet cafe akiwa na uhakika kuwa kuna nafasi za kazi zimetangazwa, kuliko kwenda cafe kulipa pesa kisha akakuta hakuna fursa yoyote.
 
Vodacom ni wafanyabiashara ila serikali inatoa huduma kwa watanzania
Wafanyabiashara pia hutoa huduma ambazo serikali haiwezi kuzitoa, na pia hulipa kodi kutokana na mapato ya biashara zao.

Iwe service, merchandising au manufacturing, wote hutoa huduma kwa namna moja kwa watanzania.

Kama kutoza fee kwa huduma zao,hata serikali hutoza fee kwa huduma zao hakuna atoaye bure.

Tofauti, serikali inatoza fee lakini hailipi kodi, private businesses hutoza fee na hulipa kodi, sasa yupi anahitaji kusaidiwa?!
 
Ni wazo zuri sana mkuu.

Nimeona kuna vigezo vinahitajika ili website ipate huduma ya FreeBasics. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kuto_upload files zenye ukubwa zaidi ya KB 200 na "Compliance to technical guidelines" ikiwemo ku_disable JavaScript, iframes, video and large images, na flash and Java applets.

Chukulia kama ilivyo hii JamiiForums, ukiifungua kwa kutumia FreeBasics kuna features zinamiss au zinakuwa slow kutokana na Ku_disable JavaScript na hivyo vitu nilivyoorodhesha hapo juu.

Hivyo, kwa upande wangu naona itapunguza ufanisi wa website kwa wale watakaofungua kupitia FreeBasics.

Technical Guidelines - Free Basics - Documentation - Facebook for Developers

I stand to be corrected.
 
Hivyo, kwa upande wangu naona itapunguza ufanisi wa website kwa wale watakaofungua kupitia FreeBasics.
Graduate akipata clue kupitia freebasics, sasa ndio analipa pesa kidogo anaenda internet cafe akiwa na uhakika kuwa kuna nafasi za kazi zimetangazwa, kuliko kwenda cafe kulipa pesa kisha akakuta hakuna fursa yoyote@
 
Back
Top Bottom