Kwanini wenzetu wameweza kujenga uchumi wa nchi zao nchi za Afrika zimefeli wapi?

Kwanini wenzetu wameweza kujenga uchumi wa nchi zao nchi za Afrika zimefeli wapi?

astranaut

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
1,276
Reaction score
1,024
hivi ni kwanini mpaka leo bajeti zetu zinategemea misaada ya nje? kwanini mpaka leo tumeshindwa angalau kucopy kwa wenzetu wao wamefanyeje kujenga uchumi wao?
mbali na kwamba sisi hatuna technolojia kama wao lakini kwanini tumeshindwa japo kuweka mifumo sahihi ya ukusanyaji kodi ili kwamba kila mtu anaepaswa kulipa kodi alipe bila kukwepa na kodi iwe rafiki kwa mlipaji?

Mapendekezo yangu kuhusu ukusanyaji kodi ambayo itasaidia kuboost mambo flani flani mbali na raslimari zingine zilizopo nchini:-
serikali iweke mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi kwa wafanya biashara wote kama ilivo kwa watumishi wa umma ambapo imeweza kuwakata moja kwa moja kutoka kwenye salary zao,hapa kwanza kabisa ihakikishe biashara zote zinakua scientifically registered(biashara na wafanya biashara wote wasajiliwe kielekronic) tofauti na sasa ambapo mtu anaanzisha biashara hakuna anaejua kama unaduka/kibanda sehem flani.

Hii itarahisisha kuzitambua biashara zote na wafanya biashara sehemu waliko,mkoa,kata,mtaa n.k japo hadi sasa leseni zinatolewa kwa njia hiyo lakini mkazo uongezwe kila anaetaka kuanzisha duka/ kibanda sehemu yoyote lazima asajiliwe kielectronic na apewe control number ya kulipia kodi.

Hapa asikubaliwe kufungua chochote bila kusajiliwa katika mfumo wa ulipaji kodi.Hii itawarahisishia TRA kukusanya kwa usahihi kwasababu watu wote watakua computerized hivyo yule ambae hajalipa wataweza kumfahamu aliko na kumuface moja kwa moja.

b) majengo yote na wamiliki wote wawe computerized mtaa kwa mtaa kwa sababu hapa napo ni sehemu nyingine inayoongoza katika ukwepaji kodi, watu wanamiliki nyumba hadi 10 lakini kodi hawalipi,hivyo basi kama nchi nzima nyumba zote zitakua compurized zikawekwa kwenye mfumo kila nyumba itakua inaonekana katika mfumo hakuna atakae kwepa kodi lakini pia lazima kodi iwe rafiki kwa kila mtanzania.

Nyumba za kulala wageni lazima kodi yake tena kwa mwezi iwe juu kidogo sababu wao wanaingiza kila siku,vivyo hivyo nyumba za biashara na nyumba za kawaida za kuishi lazima zipangiwe kodi stahiki.Hii kama kweli ikifanyika nchi nzima mapato yatapaa kwa namna moja ama nyingine.Sababu hata kama kila nyumba ikilipiwa sh 500 kwa mwezi nchi nzima pata picha makusanyo yatakuaje.

Nchi lazima ijengwe na watanzania wenyewe kwanza wengine wataendeleza,na katika haya yote lazima viongozi kidogo wawe wazalendo,pia kodi itakayo kua inakusanywa nchini lazima itumike effectivelly tofauti na kwenda kufanya shughuli za kisiasa zisizo na tija kwa taifa na watanzania.Kitu kingine mimi kwa upande wangu sioni sababu ya kuendelea kulipia lesseni za biashara na lesseni nyingine zozote badala yake watu wawe wanapewa bule kama ilivo kwa TIN number. Hivyo basi ulipaji ubaki tu kwenye kodi TRA badala ya kulipia vyote.kama mambo yote hayo yatasimamiwa kikamilifu ukusanyaji tra lazima kwa mwezi watusomee tr 5.

Kuendelea kuziachia halmashauri zikusanye kodi katika mukitadha huu tunao utumia ni kuendelea kupoteza mapato ambayo kama mfumo mpya wa computerized ungetumika basi kila mmoja angeweza kufikiwa kwa urahisi na yule ambae hajalipa angeweza kuonekana mara moja katika mfumo.Data base ya pamoja itengenezwe kwa kila halmashauri lakini zote ziwe centralized BOT.Kuna halmashauri zingine ni zembe,fisadi n.k katika ukusanyaji kodi kama mifumo sahihi ikiwekwa lazima mapato yapae,Tusijidanganye kwamba kutumia EFD machine eti wafanyabiashara wanalipa kodi lahasha hapa watu wengi hawana hizo mashine na wala list hawatoi kwahiyo kuna mianya mingi sana ya upotevu wa mapato.

Lakini pia yote hayo inafaa yaende sambamba na katiba mpya kwa sababu kama katiba isipo badilika awamu flani inaweza ikatekeleza nyingne ikaja kuharibu kwa kuanzisha mifumo mipya.Pia katika masirahi mapana ya nchi lazima itikadi za vyama ziwekwe pembeni wabunge wajadili msitakabali wa nchi kuliko kujali vyama vyao.Pia lazima bunge likae chini kwa pamoja litunge mpango mkakati wa maendeleo wa taifa kwa aidha kwa kipindi cha miaka kadhaa pamoja tofauti na kutegemea ilani za uchaguzi za vyama pekee

yangu ni hayo mwenye nyongeza,masahihisho aongezee
 
Mikataba mibovu ,ufisadi , elimu mbovu, urafiki na undugu ,katiba ,tume ya uchaguzi,majungu na uchawi kwa viongozi wetu .hivyo ndivyo vinavyotukwamisha afrika
 
Hao mabeberu mnaowatetea Ndio wanaharibu uchumi wa Africa
 
Kwanza tunatakiwa kujua historia. Hii historia ambayo waliokuwa wavivu kujisomea shuleni, siku hizi wanajiuliza imewasaidia nini, ndio itakusaidia kujua mambo mengi.
Cha kwanza katika maendeleo ya himaya ni civilization. Ukiona bado hujastaarabika, ni ngumu sana kupata maendeleo na kujenga uchumi. Sisi bado hatujafika kwenye civilization. Sisi bado tupo kwenye class struggle.
Pili: Modernization. Baada ya civilization kinachokuja ni modernization. Modernization maanake ni kila kitu kuendeshwa katika mfumo wa kisasa. Mfano ufugaji, kilimo, biashara, utawala, jeshi, magereza, polisi, malezi, elimu, afya nk.
Tatu; Baada ya modernization, kinachokuja ni uzalishaji wa ziada. Kwa sababu njia za kisasa hutumika katika shughuli za kila siku, afya Safi ipo, elimu safi ipo, utawala wa kisasa upo, jeshi la kisasa lipo, magereza ya kisasa yapo, basi uzalishaji unakuwa mwingi wa kutosha na kusaza. Sisi bado kwa 85% tunazalisha kwa ajili ya kujikimu. Angalia wafanyakazi, wakulima na wafugaji. Hata wafanyabiashara wengi; bado tunafanya kwa ajili ya kujikimu.
Nne: Biashara; baada ya kuzalisha ya ziada katika nyanja zote, kinachokuja sasa ni biashara ili kuweza kubadilishana vule ambavyo tumevizalisha katika maeneo yetu kwa ziada. Mfugaji atahitaji daktari ya mifugo, Mkulima atauza mazao, ataanzisha hospitali na kuhitaji daktari na madawa. Madawa yatauzwana kodi kulipwa na serikali kupata Fedha za kujenga barabara.
Tano; Viwanda. Baada ya kuzalisha kwa ziada tutahitaji Viwanda kwa ajili ya kusindika na kuongeza shelf life ya vitu vinavyozalishwa kwenye kilimo na mifugo.
Sio kujenga Viwanda wakati hakuna malighafi. Viwanda vya madawa, magari kutokana na civilization na uzalishaji wa ziada vitahitajika.
Sita; Market Development. Yaani maendeleo ya masoko. Maendeleo ya masoko ni hivi vitu vyote vinajiintegrate na kutengeza muendelezo kwa njia ya masoko katika mfumo wa demand and supply. Kupanda na kushuka.
Saba; Investment. Baada ya maendeleo ya masoko, kinachokuja sasa ni uwekezaji. Yaani ni zaidi ya biashara. Baada ya kuonekana Kuna masoko ya nguvu, basi watu humwaga mitaji wanayopata kwenye biashara na kuweka kwenye uwekezaji. Hapa mitaji mikubwa hutumika kuweka vitu vya maana kama vile mashine za uchimbaji madini, uchimbaji wa gesi na uyeyushaji wa chuma.
Nane! Uporaji wa rasilimali za nchi nyingine au exploitation. Hii hufanyika either kwa nguvu au wizi wa chinichini au kwa kupeleka mitaji na kuwekeza na kurudisha faida nchini.
Nchi za Ulaya na America Kaskazini hazinaruka hata moja katika hatua hizi.
Sisi hatukamilisha hata moja. Tunarukaruka tu au tunarushwarushwa tu.
 
kama hayo yote wasomi tunayajua na sisi hao hao wasomi ndo washauri na maimplementer wa mipango kwanini tumeshindwa kuchukua hatua japo tukae chini tutafakari upya wapi tumeruka, kwani tunakmbilia wapi ili hali kila hatua ni muhimu ili kufikia maendekeleo endelevu?
 
Hawezi kukujibu
hapa kuna mwingine atakuja na hoja eti kwa sababu tulitawaliwa hivyo walitunyonya sana,na kusahau kua hata vile vitu walivyotuachia vya kuweza kuboost uchumi tumeshindwa kuviendeleza na vingine aidha kwa makusudi kabisa tuliviua wenyewe.Hapa kuna mifano lukuki kabisa
 
kwa sababu mimi wakati mwingine hoja ya kutawaliwa hua sikubaliani nayo kua sababu ya kuchelewa kufika huko kwenye asali na maziwa,mbona kuna nchi huko huko ulaya zilitawaliwa lakini zimeweza kufanya vizuri pamoja na kutawaliwa kwao
 
Sisi tumeshindwa kuwa wastaarabu. Tumeshindwa kujitawala. Tunatumia akili za waliotuwala zamani au wanaotutawala sasa. Nchi zilizoamua kujitawala kiakili zimepiga hatua kwa mfano nchi za Mashariki ya Mbali. China iliendelea toka zamani. Ni dola yenye nguvu toka enzi. Naongelea nchi kama Malaysia. Sisi hatujitawali kwa fikra zetu.
 
Pole sana..kama unawaza kuongozwa na CCM halafu hapohapo upate maendeleo unajidanganya. CCM imepewa nchi miaka 60 imeshindwa katika kila eneo. Ilichoweza ni kuendesha siasa za kuwahadaa wananchi basi.
 
Kingine tunapuuza sana maarifa. Knowledge na yote haya husababishwa na kukosa ustaarabu.
 
Sisi bado tunapiga mawazo nyundo kwa sababu hatuna civilization.
 
Kodi sio tatizo tatizo zikishakusanywa zinatumikaje? Unaweza ukakusanya ukawekeza kwenye white elephant project, au miradi ya kisiasa, au ukazitumia kupambana na upinzani badala ya maendeleo.

Kwann wengine wao wanaendelea moja wana siasa safi wanachagua viongozi bora,tofauti na Africa haina mfumo bora wa uongozi uliopo Unazalisha miungu watu yaani watawala Na sio viongozi. Mtawala anaruhusiwa kufanya chochote akipendacho hata akitaka kuuwa uchumi, kuuwa watu,wizi,ufisadi,nk huku akipewa kinga ya uhalifu wote aliofanya,tofauti na wenzetu mifumo yao haiwarusu kuiba,kufilisi au kufanya uhalifu wowote.

Africa nchi mawazo ya MTU mmoja ndio mawazo ya wengi vipaumbele vya watawala si vipaumbele vya wananchi kila ajae kiongozi uja na yake mipango na haimalizi uachia njiani mwingine hivo hivo lengo ni kupiga 10%.vikwazo vingine ni ufisadi,wizi,rushwa,uvivu,uchawi,ubinafsi ndivo kikwazo cha kuendelea
 
hapa kuna mwingine atakuja na hoja eti kwa sababu tulitawaliwa hivyo walitunyonya sana,na kusahau kua hata vile vitu walivyotuachia vya kuweza kuboost uchumi tumeshindwa kuviendeleza na vingine aidha kwa makusudi kabisa tuliviua wenyewe.Hapa kuna mifano lukuki kabisa
Hizi ni ideology mfu za wajamaa kama Walter Rodney, Nyerere, Lumumba nk ndo uamini kutawalia ndio kikwazo utadhani China,USA ,India, brazili awakutawaliwa
 
hivi ni kwanini mpaka leo bajeti zetu zinategemea misaada ya nje? kwanini mpaka leo tumeshindwa angalau kucopy kwa wenzetu wao wamefanyeje kujenga uchumi wao?
mbali na kwamba sisi hatuna technolojia kama wao lakini kwanini tumeshindwa japo kuweka mifumo sahihi ya ukusanyaji kodi ili kwamba kila mtu anaepaswa kulipa kodi alipe bila kukwepa na kodi iwe rafiki kwa mlipaji?

Mapendekezo yangu kuhusu ukusanyaji kodi ambayo itasaidia kuboost mambo flani flani mbali na raslimari zingine zilizopo nchini:-
serikali iweke mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi kwa wafanya biashara wote kama ilivo kwa watumishi wa umma ambapo imeweza kuwakata moja kwa moja kutoka kwenye salary zao,hapa kwanza kabisa ihakikishe biashara zote zinakua scientifically registered(biashara na wafanya biashara wote wasajiliwe kielekronic) tofauti na sasa ambapo mtu naanzisha biashara hakuna anaejua kama unaduka/kibanda sehem flani.

Hii itarahisisha kuzitambua biashara zote na wafanya biashara sehemu waliko,mkoa,kata,mtaa n.k japo hadi sasa leseni zinatolea kwa njia hiyo lakini mkazo uongezwe kila anaetaka kuanzisha duka/ kibanda sehemu yoyote lazima asajiliwe kielectronic na apewe control number ya kulipia kodi.

Hapa asikubaliwe kufungua chochote bila kusajiliwa katika mfumo wa ulipaji kodi.Hii itawarahisishia TRA kukusanya kwa usahihi kwasababu watu wote watakua computerized hivyo yule ambae hajalipa wataweza kumfahamu aliko na kumuface moja kwa moja.

b) majengo yote na wamiliki wote wawe computerized mtaa kwa mtaa kwa sababu hapa napo ni sehemu nyingine inayoongoza katika ukwepaji kodi, watu wanamiliki nyumba hadi 10 lakni kodi hawalipi,hivyo basi kama nchi nzima nyumba zote zitakua compurized zikawekwa kwenye mfumo kila nyumba itakua inaonekana katika mfumo hakuna atakae kwepa kodi lakini pia lazima kodi iwe rafiki kwa kila manzania.

Nyumba za kulala wageni lazima kodi yake tena kwa mwezi iwe juu kidogo sababu wao wanaingiza kila siku,vivyo hivyo nyumba za biashara na nyumba za kawaida za kuishi lazima zipangiwe kodi stahiki.Hii kama kweli ikifanyika nchi nzima mapato yatapaa kwa namna moja ama nyingine.

Nchi lazima ijengwe na watanzania wenyewe kwanza wengine wataendeleza,na katika haya yote lazima viongozi kidogo wawe wazalendo,pia kodi itakayo kua inakusanywa nchini lazima itumike effectivelly tofauti na kwenda kufanya shughuli za kisiasa zisizo na tija kwa taifa na watanzania.Kitu kingine mimi kwa upande wangu sioni sababu ya kuendelea kulipia lesseni za biashara na lesseni nyingine zozote badala yake watu wawe wanapewa bule kama ilivo kwa TIN number. Hivyo basi ulipaji ubaki tu kwenye kodi TRA badala ya kulipia vyote.kama mambo yote hayo yatasimamiwa kikamilifu ukusanyaji tra lazima kwa mwezi watusomee tr 5.

Kuendelea kuziachia halmashauri zikusanye kodi katika mukitadha huu tunao utumia ni kuendelea kupoteza mapato ambayo kama mfumo mpya wa computerized ungetumika basi kila mmoja angeweza kufikiwa kwa urahisi na yule ambae hajalipa angeweza kuonekana mara moja katika mfumo.

Lakini pia yote hayo inafaa yaende sambamba na katiba mpya kwa sababu kama katiba isipo badiika awamu flani inaweza ikatekeleza nyingne ikaja kuharibu kwa kuanzisha mifumo mipya.Pia katika masirahi mapana ya nchi lazima itikadi za vyama ziwekwe pembeni wabunge wajadili mstakabali wa nchi kuliko kujali vyama vyao.

yangu ni hayo mwenye nyongeza,masahihisho aongezee
Nchi haina vyanzo vya pesa vya kuaminika, CCM waliua viwanda vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tumemaliza kila kitu hapa. Lakini uvivu inayopelekea hata akili zetu kutokupambanua changamoto kwa haraka.

Nitoe mfano wa mfanyakazi wangu akipata mshahara tuu lazima aisje kazini akituma ujumbe amefiwa Mara kaenda Tanga kuzika na Corona hii. Mara kaenda kuogelea baharini kachomwa na mwiba yaani watanzania wengi wetu hatupendi kuwajibika. Kazi unaomva mwenyewe excuses kibao ukifukuzwa unalalamika

Back
Top Bottom