Kwanini wenzetu wameweza kujenga uchumi wa nchi zao nchi za Afrika zimefeli wapi?

Kitendawili cha kodi Tanzania kitatatuliwa pale tutakapopata serikali itakayokuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu. Ni magumu ndiyo kwani nchi nzima itatikisika na kutakuwa na upinzani mkubwa sana dhidi ya mpango husika. Mwanzoni wadau wataona ngumu kumeza!

Ili ukusanye kodi kirahisi lazima uwe na mfumo mmoja wa malipo nchi nzima yaani Centralized Payment System. Mfano ni ilivyo mifumo ya malipo ya huduma za kifedha (simu na benki). Ukifanya tu muamala papo hapo kila mtu anahesabu chake, TRA, halmashauri,nk.

Sasa hiyo mifumo itawafanya wafanyabiashara wengi ku-give up ukwasi ambao kimsingi siyo wa kwao (hujilimbizia kodi mbalimbali anazolipa mlaji na kuzifanya sehemu ya mtaji). Ukitaka ku-imagine itakuwaje rejea shughuli ya kuviunganisha vituo vya mafuta ilivyokuwa na upinzani mkali.

Hapo wanasiasa (wasio genuine) watakuja na hoja kama 'mfumo huu hautafanya kazi vijijini ambako hakuna mtandao'.

Ni hivi:

Kila biashara itakuwa na akaunti au trace/control namba yake maalumu kwenye huo mfumo wa malipo. Hapo miamala yote ya biashara hiyo ya kutoka na kuingia lazima ifanywe kwenye hiyo account au trace number hivyo mzunguko halisi wa biashara unaweza kuonekana kwa kugusa tu na kidole. Hata kodi hakuna atakayekaa kukadiria. Mfumo utaamua based on formula iliyopo.

Mfumo huu hauhitaji likompyuta la mezani bali unahitaja tule tumachine twa kushika tu mkononi yaani POS aka Point Of Sales. Rejea namna mawakala wa benki, wakatisha ushuru wa halmashauri, EFD, au maduka makubwa yanavyofanya kazi.

Pia huu mfumo hauwezi kuwa na ufanisi bila kuihusisha sekta binafsi (PPP).

Siku serikali inaleta hili pendekezo utasikia kelele kama zote kutoka kila kona. Ndiyo itajua haijui. Unakumbuka mpango wa 2016 wa kufufua sekta ya textiles kwa miaka mitatu (2016-18). Sehemu ya mpango ilikuwa kufuta mitumba kadri ya vile ambavyo viwanda vya ndani vingeongeza uzalishaji wa nguo mpya. Unakumbuka mziki wake? Serikali ikaufyata kama vile hakuna kilichotokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jibu murua kabisa mkuu! Afrika hatuna bado viongozi safi wenye ari. Alikuwepo mmoja tu naye ni Qaddafi lakini kwa tabia zetu za u-cain tulimmaliza. Sasa hapa pengine mpaka mwisho wa dahari au tupate magufuli kama 200 hivi ndiyo tufidie miaka 60 tuliyopoteza takriban baada ya uhuru. Ili tuendelee tunahitaji viongozi ambao wanatakuwa na fikira za kuwa maisha yao bora ni baada ya mtanzania au mwafrika wa mwisho kuwa na maisha bora ndiyo wapate haya maisha wanayoishi sasa na hata tangu baada ya uhuru kama miungu watu. Waje kwenye jamii wavae kikazi wajumuike na wananchi tuchimbe mitaro, tujenge barabara, vyoo bora, nyumba bora, zahanati bora, kilimo cha kisasa, shule bora, mazingira bora, tupande miti, ukoka, paving katika makazi, maji taka yapelekwe sawasawa, sehemu za biashara ziwekwe bora, maeneo ya michezo, bustani za kupumzikia na list ni ndefu! Inawezekana hapa tuna viongozi vibuyu, wabinafsi, uzalendo wa kutamka na walaghai. Nachukia sana wakati mwingine kuwa mtanzania na mwafrika kwa ujumla.
 
Kwa ufupi, Rushwa, Ubadhirifu, Ukabila na Utegemezi ndiyo adui mkubwa wa maendeleo afrika.
 
Kama kila mtanzania akilipa direct tax ya 1800 kila mwezi kwa idadi ya watu milioni 57 basi serikali itakuwa na uhakika wa kuingiza bilioni 102.6 kila mwezi au trilioni 1.231 kwa mwaka. Je, hili linawezekana vipi?
Kwa kupitia current system ya vitambulisho vya nida serikali itatambua status ya wananchi wake kama wqmaeajiriwa, wamejiajiri au hawana ajira. Endapo wameajiriwa basi itakuwa rahisi kulipa kodi kwa vile itakatwa moja kwa moja kwenye mishahara, kama wamejiajiri basi taarifa, zao za benki zitakuwa linked na nida, mobile banking information na kulipa kodi kutokana na mapato yake kupitia GePG system. Kwa hiyo let's say ana biashara na analipwa kupitia mobile transactions basi serikali inakata kodi yake moja kwa moja kama VAT(anayolipa mteja) na direct tax ya mwenye biashara husika. Kama mwananchi hana ajira serikali kupita platform itatakiwa kumwezesha huyo mwananchi kupata ajira au kupata vibarua na tenda mbalimbali ili aweze kupata kipato na serikali ipate kodi yake kupitia kipato hicho. Kwa kupitia mfumo huu serikali itakuwa kama facilitator na wananchi tutaweza kuijenga nchi yetu wenyewe bila kutegemea misaada ya nje.
Na pia mfumo huu utasaidia katika kupambana na uhalifu kwa vile database itatumika pia na vyombo vya usalama. Na pia katika janga kama hili la Covid-19 itakuwa rahisi kujua nani anastahili kulipwa pesa ya kujikimu na nani hastahili.
 
Waafrika wanafikiri,wanaamua kwa HISIA kuliko UHALISIA wa Jambo husika

Hiyo ndio sababu kubwa kwa nchi za Afrika kutoendelea katika kila sekta,.

Pale viongozi wetu watakapo Anza kutoka maamuzi yao kwa Uhalisia wa sio kwa hisi,nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara zitabadilika
 
Hoja ya kutawaliwa napinga coz walio tawaliwa sana ndio wenye angalau leo
 
Hiyo population ya walipakodi umeitoa waoi? Unadhani kila Mkazi anayehesabiwa hata Kama ni mtoto basi anaweza kulipa kodi? Wazee, walemavu na watoto umewaweka wapi? Wanafunzi je?
 
safi sana
 
Hiyo population ya walipakodi umeitoa waoi? Unadhani kila Mkazi anayehesabiwa hata Kama ni mtoto basi anaweza kulipa kodi? Wazee, walemavu na watoto umewaweka wapi? Wanafunzi je?
mi nilisema kwa kila mtanzania anaestahili kulipa kodi na sio kila mtanzania
 
Hiyo population ya walipakodi umeitoa waoi? Unadhani kila Mkazi anayehesabiwa hata Kama ni mtoto basi anaweza kulipa kodi? Wazee, walemavu na watoto umewaweka wapi? Wanafunzi je?
Hiyo ni estimate tu, sio real fact.
Hapo nineainisha endapo kama mtu analipwa elfu kumi kwa mwezi hivyo kodi iwe 18% ya hiyo ten
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…