HOJA Kwanini Wizara ya Afya isibadili utaratibu wa utoaji huduma kwenye vituo vya afya?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Acha Makasiriko Mkuu,Hatupo kwenye Mada Ya Udini๐Ÿ˜ƒ
Kwahiyo Mke wako au Ndugu yako Unaona Ni sahihi Kupimwa Njia Na Daktari wa kiume Ni Sahihi?

Kwanza Unajua Wajawazito Wanapimwaje Njia Au Unaongea Tu,Ukijua Wanapimaje Njia Hata wewe Itakupa ukakasi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Somesheni watoto wenu wa kike, wawe madaktari wengi.

Hamtaki watoto wa kike wasome, na wakati huo huo, hamtaki madaktari wa kiume.

Mbona kwa Waganga mpaka wanafira wake zenu hatujawahi kuona malalamiko??

Suala la matibabu ni suala hiari.

Chagua Daktari wa kike ,kama.m hayupo, chukua mkeo mpeleke palipo na daktari wa kike.

Hakuna mtu timamu huwa analazimisha kutibu mtu.
 
Mimi Sina shida hata wakiingiza mkono wote,huo sio mwili wangu,nakushauri na wee uchunge mwili wako

By the way ni for medical reasons
 
Mpaka leo hii 2026 tuwe bado na uhaba kiasi hicho cha wataalam?Siamini hilo japo kuna upungufu lakini si kiwango hicho
Tembelea vyuo vya afya hasa wakati wa mahafali utaona wahitimu wa kike ni asilimia ndogo sana. Lakini pia sikubishii sana
 
Ufafanuzi Mzuri,Lakini Hoja yangu Ubadilishwe Utaratibu huo Madiktari wa Kiume Wabaki kwenye Upasuaji tu kama Mjamzito atashindwa kujifungua Kwa njia za kawaida.
 
Kama si sawa wewe mbona unaoa mwanamke na kulala naye uchi kwanini usioe mwanaume mwenzio na Mwanamke asiolewe na mwanamke mwenzie huoni huo ndiyo ungekuwa uadilifu
 
Rejea Mkasa Wa yule Mdada wa Tabora aliebakwa na Daktari Kwenye Kituo Cha Afya wakati wa Huduma Mwaka Jana Mwezi 12 Tena alikua ni Mke wa Mtu na Mme wake Alikua nje Mapokezi akimsubili mkewe apatiwe Huduma,

Huyo ni Mmoja aliamua Kutoka Na kusema,Je Ni Wangapi waliofanyiwa vitu vya Hovyo Na wakaona aibu kutoka Kusema Hayo waliotendewa?

Tukisema Wagonjwa wanaohitaji huduma sehemu Zao za Faragha Wahudumiwe na jinsia yao ukiacha fedheha za kuonwa maungo yao sababu zingine ni kama hizo,

Madaktari Wa kiume waliokamilika kihisia kuona Maungo ya Wanawake inatia ukakasi.
 
Ufafanuzi Mzuri,Lakini Hoja yangu Ubadilishwe Utaratibu huo Madiktari wa Kiume Wabaki kwenye Upasuaji tu kama Mjamzito atashindwa kujifungua Kwa njia za kawaida.
Mkuu hemu fuatilia kwanza takwimu za nchi yetu maana ni kama unaongea jambo la kufikirika sana.

Takwimu za nchi yetu, madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi ni wachache mno, na asilimia kubwa ni wanaume. Kwenye wilaya nyingi au mikoani, unakuta kuna daktari bingwa mmoja tu wa kiume anayehudumia hospitali nzima ya rufaa.

Kwa huu uhaba wa madaktari unaona jambo unalolitaka linawezekana kweli?
 
Tabia ya mtu kwa utashi wake haimaanishi kile anayesimamia ni mzinzi. Mpaka amefikia kuhudumiwa na mwanaume maana yake wataalamu wa kike wa hayo magonjwa hamna hapo. Ili kuokoa jahazi wakaletwa wa kiume, utaanzaje kuruhusu jinsia moja ihudumie nyingine wakati hata wataalamu wa kutosha huna.
Unataka watu wakose huduma na maradhi kushamiri?

Haya unataka wa jinsia moja, vipi dokta wa kike akiwa ni upinde wale na ana tabia za kishenzi. Una uhakika atakuwa salama hapo? Hebu hizi tabia za mshenzi mmoja zisifanye mambo yakawa hovyo.

๐Ÿ˜€Mkuu hebu fikiria unachagua kuhudumiwa na mwanaume mwenzio kuepusha mambo ya aibu halafu una tatizo kwenye jicho la chini na Dokta bingwa ni mende. Yaani unatoa nguo kabla hajaanza huduma anajiambia "Ooh Mark usidinde ni mgonjwa huyu". Usalama upo?

Nimeandika mengi ila kiufupi hizi tabia za watu binafsi tu haijalishi jinsia gani kote zipo. Isikatazwe tu na wataalamu wa jinsia husika ni haba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ