Kwanini Yanga atapigwa na Simba Oktoba 23

Kwanini Yanga atapigwa na Simba Oktoba 23

Point kubwa ni uwepo wa Babu ONYANGO🤣🤣🤣🤣 Yule ni Dawa Ya yule Boya wao
 
Mikia mtafungwa mtarudi mnalalamika na mimba changa mkitafuna malimao
Mnakufa 3 Bila
Mechi ya mikia lazima kipigo
 
Habari wakuu,

Naimani mu wazima wa afya kabisa, na tunaendelea vyema na harakati zetu za kutafuta ridhki. Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa nini wana Jangwani (maarufu kama Utopolo au Chura) watapigwa kwenye mechi yao itakaowakutanisha na wababe mara nne wa Ligi Kuu Simba SC.

1. Beki mbovu na nzito za wana Jangwani hao. Wana Jangwani wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na beki imara, kwani beki zao asilia Mwamnyeto na Dickson Job zina udhaifu mkubwa sana, hasa kwa kukosa spidi na rahisi sana kupitika na kutoa maboko, huku Bangala akifosiwa kucheza kama namba 4 bandia.

2. Ukosefu wa namba 6 bora itakayosaidia ukabaji na kupandisha mashambulizi. Tatizo hili hata kwenye michuano ya kimataifa limeonekana kugharimu kikosi hicho cha wana Jangwani kwani Bangala hucheza 4, hivyo viungo wenye kasi na akili wa simba kama Okrah na Chama wanaweza kutumia nafasi hii kuwakalishia chuma cha moto Chura.

3.Simba kupania kuwapiga vyura hao wa Jangwani. Vijana wa Simba wamepania kuwanyamazisha Utopolo kwani wanaongea sana na wanaonekana kusahau kuwa angurumapo Simba mcheza nani. Na pia Simba ndiyo baba mwenye nyumba, na watathibitisha hilo.

4. Kutumia faida ya kupigwa na Al Hilal. Ni sawa na mwanamke mwenye maumivu ya kuachwa na bwana wake anavyoliwa mbususu yake kwa urahisi. Hivyo Simba anaweza kula utamu huo wa chura kwani saikolojia ya wachezaji na timu bado haijakaa sawa.

5. Uwepo wa Juma Mgunda a.k.a ( Guardiola Mnene) ambaye amekuwa hapigiki toka ajiunge na wana Msimbazi hao, na pia kuwajua vizuri Yanga ikiwemo na mbinu zao za kizamani kiuchezaji.

6. Kumtegemea Fiston Mayele na si timu. Hili linajidhihirisha hata kwenye mechi ya kwanza kwani Utopolo walishinda kwa uwezo wa Mayele na si timu. Hivyo raundi hii wana Lunyasi watamdhibiti vizuri ili asiteteme bali atetemeke.

Zaidi ya hapo nawapongeza sana Simba kwa badiliko lao la kiuchezaji, kwani wamekuwa bora sana, na nawapa baraka zote kwenye michuano yao yote.

Mungu bariki Simba, na pia didimiza Yanga.
Afu wewe........kweli
20221018_171425.jpg


Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom