Kwanini Yanga hawajauchukulia msiba wa Yusuph Manji Kwa ukubwa

Kwanini Yanga hawajauchukulia msiba wa Yusuph Manji Kwa ukubwa

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Sisi mashabiki wa Yanga tumesononeka na kifo cha Yusuph Manji.

Lakini viongozi na taasisi ya Yanga hawajaupa uzito msiba huu wa kiongozi aloyejitoa muda, nguvu na zaidi pesa zake kuijenga na kuipa mafanikio team yetu ya Yanga.

Yanga wameshindwa kuomboleza japo kuamru bendera za team yetu zipepee nusu mlingoti, au kuandaa mchezo wa kumpa heshima.

Au hata kushirikiana na familia yake kumzika Kwa heshima.

Naipenda sana YANGA ila viongozi mmetuangusha Kwa kuonyesha dhahiri kumfifisha Mwenyekiti wetu Manji na kuonyesha hakuwa chochote wala lolote Kwa Yanga

Viongozi wa Yanga Kwa hili mmeteleza, ila Bado hamjachelewa tunaomba japo muandame mcheza mkubwa wa kumuenzi au siku ya mwananchi iitwe ASANTE MANJI au MANJI DAY.

Wasalam

PIA SOMA

- TANZIA - Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani
 
Mambo mengine nikutaka kuyakuzaa kipuuzi tu, wewe ulitaka viongozi wateue watu wakatangulizwe kwenye kaburi lake?. Aliyekufa kafa na kwaapenzi ya mungu... Umhimu wa mtu huwepo akiwa hai na sio akiwa mfu.
 
Kwanza misiba yote inatolewa sabab marehem kafa na nini, ila huyu taarifa imetolewa kibabe, Just Manji kafia Florida Marekani. Wakaona hizo ndio taarifa za kutupa walaji. Basi nasi tukauchukulia msiba kama nothing happened
 
Yaan ulie msiban wa x wako , mbelee ya mumeo anakumiliki ss hv ,ww kuwezaa afsaaa😂
 
Naona kama wanataka legacy ya GSM ndio idumu Yanga, nilisikitika kuona tuna msiba huku watu wanaandamana kushangilia ujio wa Chama.

Lakini, Manji atabaki mioyoni mwetu wanazi wa Yanga. Hatuwezi kusahau alipotutoa, Apumzike kwa amani.
 
Naona kama wanataka legacy ya GSM ndio idumu Yanga, nilisikitika kuona tuna msiba huku watu wanaandamana kushangilia ujio wa Chama.

Lakini, Manji atabaki mioyoni mwetu wanazi wa Yanga. Hatuwezi kusahau alipotutoa, Apumzike kwa amani.
Hakika mkuu
 
Back
Top Bottom