Kwanini Yanga hawajauchukulia msiba wa Yusuph Manji Kwa ukubwa

Kwanini Yanga hawajauchukulia msiba wa Yusuph Manji Kwa ukubwa

Ulitaka wafanye nini ili uone huo uzito?
Wangeweza hata kuahirisha shamra shamra kwa muda. Sasa YM akiwa bado hajazikwa ile Jumatatu, lakini cha ajabu yakafanyika maandamano jijini Dar na sehemu nyingine kushangilia usajili wa Chama

1719989209502.png

1719989226410.png
 
We mkeo akienda kwenye msiba wa ex wake akalia kujigaragaza utajiskiaje?
 
Alitoa pesa Bure?, alikuja kufanya biashara na ya ga na sio kutoa msaada.
Hata kama, bado Yanga inapaswa kumuenzi. Just imagine hao akina Gulamali,Manji,GSM,n.k wasingejitokeza kufanya biashara na Yanga hali ingekuwaje hapo klabuni? Picha utaipata ukirejea ule msimu wa kutembea kapu. Unajizima data sana.
 
Kwahiyo unataka shughuli za timu zisimame?, amekufa kafa. Na kila mmoja ana mchango wake kweny timu zama za Manji zilikuwepo zikapita... Zama za Gsm zipo na zitapita. Usilazimishe kila mtu apokee Jambo kama unavyotaka.

Kama familia hawajaamua kuishirikisha timu kwa ukubwa huo basi hata timu imetoa taarifa kulingana na upatikanaji wake.... Haya mengine ni chokochoko za kiafrika tupu.
Aliyesema wewe ni mtoto kweli hajakosea. Unaweza kujibu hapa ni kwanini Rais Mstaafu akifa (wa nchi yoyote ile) mamlaka zilizopo madarakani hutangaza maombolezo na kushusha bendera japo zama za huyo Hayati zilishapita?
 
Umemjibu vyema
 
Sisi wahenga wa Dar Young African tunautambua na kuheshimu sana mchango wa hayati Yusuph na baba yake( Manji's family) katika soka la Tanzania.
 
Sababu hajazikwa bongo.

Manji angezikwa Tanzania ingekuwa balaa kubwa
 
Kwanza misiba yote inatolewa sabab marehem kafa na nini, ila huyu taarifa imetolewa kibabe, Just Manji kafia Florida Marekani. Wakaona hizo ndio taarifa za kutupa walaji. Basi nasi tukauchukulia msiba kama nothing happened
Sio kwamba ni kwa vile utopolo hawana uwezo wa kwenda Florida kula wali maharage msibani?
 
MLITAKA YANGA WAPITE WANAPIGA KELELE MITAANI ? NDO MJUE WANAOMBOLEZA ????
 
Aliyesema wewe ni mtoto kweli hajakosea. Unaweza kujibu hapa ni kwanini Rais Mstaafu akifa (wa nchi yoyote ile) mamlaka zilizopo madarakani hutangaza maombolezo na kushusha bendera japo zama za huyo Hayati zilishapita?
Una akili ww? Kwahiyo Manji alikuwa Rais wa Nchi gani?.
Hata kama, bado Yanga inapaswa kumuenzi. Just imagine hao akina Gulamali,Manji,GSM,n.k wasingejitokeza kufanya biashara na Yanga hali ingekuwaje hapo klabuni? Picha utaipata ukirejea ule msimu wa kutembea kapu. Unajizima data sana.
Wangepataikana wengine....
 
Back
Top Bottom