Kwanini Yanga icheze kesho na Simba keshokutwa?

Kwanini Yanga icheze kesho na Simba keshokutwa?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ni sawa hatukatai #TFF ni Simba 100% sio ajabu nao utakuta wamefunga ofisi kuomboleza kichapo cha goli tano, kati ya Tff zote hii ndio imeshindwa kuficha mapenzi kwa kitoto chao kipenzi Simba.

Simple calculation timu zote zimecheza Jumapili ila ajabu Yanga inayoenda kucheza ugenini wanacheza kesho wakati Simba wakiwa nyumbani wanacheza keshokutwa ukiangalia Yanga ndio walikua na gemu ngumu zaidi kuliko Simba kwa hapa Tff imembeba Simba, ratiba hii inamtengenezea Simba mazingira mazuri sana ya kiupendeleo kuibuka na ushindi huku wakitaka Yanga ipoteze gemu zake.

Chini ya Tff hii wamekua wakiifanyia Yanga figisu za kila aina ili ishindwe bahati nzuri sana Yanga imekua na viongozi shupavu chini ya Rais kijana Eng Hersi na mashabiki shupavu hili limesaidia kuruka vikwazo na viunzi vyote vya Tff kama Yanga angekua legelege hakika angetema pointi zote.

Hata siku moja giza halijawahi kuishinda Nuru.

Roma ikisema imesema
 
Ni sawa hatukatai #TFF ni Simba 100% sio ajabu nao utakuta wamefunga ofisi kuomboleza kichapo cha goli tano, kati ya Tff zote hii ndio imeshindwa kuficha mapenzi kwa kitoto chao kipenzi Simba...
Vitu vingine viache vipite Mkuu,
 
Ni sawa hatukatai #TFF ni Simba 100% sio ajabu nao utakuta wamefunga ofisi kuomboleza kichapo cha goli tano, kati ya Tff zote hii ndio imeshindwa kuficha mapenzi kwa kitoto chao kipenzi Simba...
Kwa hiyo unataka kila siku inapocheza Yanga na Simba icheze?
 
Dec

15 na 16 ni mbali sana ni zaidi ya mwezi. Ukweli Simba anabebwa sana na TFF na marefa wao akina Tatu mwalogo.
Hiyo ni kwa mujibu wa google japo hapa kati wanacheza mechi za caf
 
Back
Top Bottom