Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
1. Ushahidi wa Kibiblia
Yohana 1:1 – "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Tito 2:13 – "Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo."

Yesu mwenyewe alikiri kuwa ni Mungu:
Yohana 10:30 – "Mimi na Baba tu umoja."
Yohana 8:58 – "Amini, amini, nawaambia, Kabla Abrahamu hajakuwako, Mimi niko."

2. Sifa za Kimungu alizo nazo Yesu
Uwepo wake wa milele – Mika 5:2
Uwezo wa kusamehe dhambi – Marko 2:5-7
Uwezo wa kutoa uzima wa milele – Yohana 10:28
Uwezo wa kuhukumu ulimwengu – 2 Wakorintho 5:10

3. Miujiza inayodhihirisha Uungu wa Yesu
Kubadili maji kuwa divai (Yohana 2:1-11) –
Kutembea juu ya maji (Mathayo 14:25-27)
Kutuliza dhoruba (Marko 4:39)
Kufufua wafu (Yohana 11:43-44)
Kupaa mbinguni (Matendo 1:9-11)

4. Unabii wa Agano la Kale ulitimia kuhusu Uungu wa Yesu
Katika Isaya 9:6 – Yesu anaitwa "Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele."
Katika Mathayo 1:22-23, tunasoma jinsi unabii huo ulivyotimia:
"Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, Naye watamwita jina lake Imanueli; yaani, Mungu pamoja nasi."

5. Watu Walimwabudu Yesu na kukiri kuwa ni Mungu
Mathayo 28:9,17 – Wanafunzi wake walimsujudia.
Yohana 20:28 – Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu alipoambiwa na Tomaso kuwa ni Mungu, hakukanusha.

Kama unadai Yesu sio Mungu, toa sababu zako hapa
 
Kwa nn Yesu Hakuoa, na Je kwa Nini Shetani alingea na mwanamke ktk Bustani ya Edeni
 
Uhusiano wa Neno na Mungu: Yohana 1:1 inaonyesha kuwa Neno alikuwa "kwa Mungu," na si kwamba Neno alikua Mungu mwenyewe. Hii inaweza kueleweka kama kuwepo kwa tofauti kati ya Mungu na Neno, huku Neno likiwa na uhusiano wa karibu na Mungu lakini si Mungu mwenyewe.
 
Kutoka 3:14 Mungu anamwambia Mussa kuwa MIMI NIKO AMBAYE NIKO, amwambie Farao NIKO amenituma, na ukisoma Yohana 8:58 Yesu anasema kabla ya Ibrahimu hajakuwepo, MIMI NIKO, tayari kaweka wazi kuwa yule NIKO ni yeye
 
Uhusiano wa Neno na Mungu: Yohana 1:1 inaonyesha kuwa Neno alikuwa "kwa Mungu," na si kwamba Neno alikua Mungu mwenyewe. Hii inaweza kueleweka kama kuwepo kwa tofauti kati ya Mungu na Neno, huku Neno likiwa na uhusiano wa karibu na Mungu lakini si Mungu mwenyewe.
Karudie Tena kisoma umalize mistari yote halafu njoo uSome ulichokiandika hapa
 
Yesu anaitwa Mungu kwa sababu mbalimbali zinazotokana na mafundisho ya Biblia na imani ya Kikristo. Sababu kuu ni:

1. Uungu Wake Katika Maandiko

Biblia inamrejelea Yesu kama Mungu katika maandiko kadhaa, kama vile:

• Yohana 1:1 – “Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Hapa, “Neno” linamrejelea Yesu.

• Yohana 20:28 – Mtume Tomaso alipomwona Yesu baada ya kufufuka, alisema: “Bwana wangu na Mungu wangu!”

• Tito 2:13 – “Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.”

2. Yesu Mwenyewe Alidai Uungu

• Yohana 10:30 – Yesu alisema: “Mimi na Baba tu umoja.”

• Yohana 8:58 – Yesu alisema: “Kweli nawaambia, kabla Ibrahimu hajazaliwa, Mimi niko.” Hili lilionekana kama dai la Uungu, kwani “Mimi Niko” (Ego Eimi kwa Kiyunani) linarejelea jina la Mungu lililotolewa kwa Musa (Kutoka 3:14).

3. Matendo Yake Yanaonyesha Uungu

• Yesu alisamehe dhambi (Marko 2:5-7), jambo ambalo Wayahudi walijua ni haki ya Mungu pekee.

• Yesu alituliza dhoruba (Mathayo 8:26), akifufua wafu (Yohana 11:43-44), na kutenda miujiza mingi iliyothibitisha mamlaka yake ya Kimungu.

4. Kuitwa Bwana (Kyrios) katika Agano Jipya

Katika lugha ya Kigiriki ya Agano Jipya, Yesu mara nyingi anaitwa Kyrios (Bwana), neno lililotumika kwa Mungu katika Agano la Kale.

5. Ibada Ilitolewa Kwake

• Katika Ufunuo 5:12-14, Yesu anapokea sifa na ibada kutoka kwa viumbe wote, jambo linalomaanisha kuwa ana nafasi ya Mungu.

Kwa msingi huu, Wakristo wanaamini kuwa Yesu ni Mungu katika mwili, sehemu ya Utatu Mtakatifu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu).
 
Uhusiano wa Neno na Mungu: Yohana 1:1 inaonyesha kuwa Neno alikuwa "kwa Mungu," na si kwamba Neno alikua Mungu mwenyewe. Hii inaweza kueleweka kama kuwepo kwa tofauti kati ya Mungu na Neno, huku Neno likiwa na uhusiano wa karibu na Mungu lakini si Mungu mwenyewe.
Tafsiri sahihi ya aya hiyo inasisitiza kuwa Neno (ambaye ni Yesu Kristo, kama inavyobainishwa katika Yohana 1:14) alikuwa pamoja na Mungu lakini pia alikuwa Mungu. Maneno "Neno alikuwa kwa Mungu" yanaonyesha tofauti ya nafsi ya Baba na Mwana, lakini sehemu ya mwisho "Neno alikuwa Mungu" inathibitisha uungu wa Yesu.

Kwahiyo, Yohana 1:1 haitoi tafsiri kwamba Neno si Mungu, bali inaonyesha uhusiano wa Utatu Mtakatifu—Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Hivyo hapo ni kwamba Neno (Yesu) alikuwa na Mungu Baba lakini wakati huohuo alikuwa Mungu. Ndio maana katika Yohana 10:30 Yesu anasema: "Mimi na Baba tu Umoja."
 
Mwanzo unaozungumzwa ni wa mbingu na nchi. Kabla ya mwanzo huo Mungu alikuwepo, maana Yeye hana mwanzo
Kulingana na yohana "hapo mwanzo"alikuwa anaongelea kuhusu mbigu na nchi?
au alikuwa anaongelea mwanzo wa neno na mungu!?
 
Wanaomuita yesu ni Mungu hao wote ni katika watu waliokufuru, na ibada za watu hao waliokufuru huomba kwa jina la mwanadamu huyo anaeitwa yesu badala ya kuomba kwa jina la Mungu mmoja aliemuumba huyo yesu.
Nimekueleza mambo makuu matano kwanini Yesu anaitwa Mungu. Kama kuna eneo hujaelewa vizuri uliza swali.
 
Mbona kama alishawahi kufa msalabani sasa inakuwaje anakuwa wa milele
Alikufa akafufuka. Wakati anakufa alikuwa ameuvaa mwili wa kibinadamu ili damu imwagike tupate ondoleo na msamaha wa dhambi.
 
Back
Top Bottom