Leo TCRA wametangaza kuwafungia Kwanza online tv eti kwa kosa la kuripoti tahadhari iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani kwa raia wake kuhusu mwenendo wa COVID 19 nchini. Wamefungiwa miezi 11 kwa kosa hilo walilofanya julai mosi mwaka huu. Kitendo hiki kamwe hakikubaliki.
Taarifa za Kwanza online tv siyo za kigaidi, hazihamasishi chuki wala kumtukana mtu. Kwa TCRA kufanya hivi ni kukosa uadilifu na kushindwa kusimamia misingi yake. Wamegeuka chombo cha kufanya kazi kwa kumuogopa fulani na kuabudu. Huu ni upuuzi wa kiwango chake.
Aidha lipo gazeti ambalo limekuwa likiwatukana wapinzani kila leo na juzi lilienda mbali na kumuita Lissu kuwa ni balozi wa ushoga chini. Hakuna hatua yoyote lililochukuliwa. Habari kama hizi zinahamasisha chuki na hasa ikizingatiwa jinsi TCRA walivyozifumbia macho.
Yapo mambo ambayo mtu au watu kuyafanya waone aibu, wazingatie maadili ya wao kupewa usimamizi na siyo kumuabudu mtu na kuegemea upande!