Kwanza TV waitwa na TCRA kujieleza kwanini wasifutwe kwa kuchapisha habari ya Ubalozi wa Marekani juu ya COVID 19

Kwanza TV waitwa na TCRA kujieleza kwanini wasifutwe kwa kuchapisha habari ya Ubalozi wa Marekani juu ya COVID 19

Vyombo vya habari Kwa umoja wao havijui nguvu waliyonayo. Kwa bahati mbaya wameamua kukacha majukumu yao kwa ustawi wa taifa
 
Uandishi unatakiwa ku balance hasa kwenye issue sensitive kama hizo.Upande wa serikali haukuulizwa na hizo habari mwandishi ha ku confirm na wizara ya afya

Pia hilo tamko la ubalozi wa marekani lina walakini kisayansi ona unasema kuwa kitisho cha maambukizi ya virusi vya corona jijini Dar es Salaam na maeneo mengine kipo juu mno kwa sababu serikali haijatoa takwimu za ugonjwa wa COVID19 !!!!!!

Hivi kiini cha maambukizi ya Corona kuwa kubwa ni sababu ya takwimu? takwimu ndizo zinasambaza corona? takwimu ndio wadudu wa corona? Na kuwa tiba ya Corona ni takwimu ukizitoa ndipo watu wanapona!!!

Mwandishi alitakiwa ajiridhishe kisayansi kama ni kweli takwimu ndizo zinasambaza Corona kuwa kadri unavyotoa takwimu sanaaaa Corona inapungua!!! Marekani wanatoa takwimu sana kila saa Corona mbona haishuki?

Ni kama vile kusema nchi iko kwenye uchumi wa kati huku wananchi wakiwa masikini wakubwa. Hilo neno uchumi wa kati ndio linaloolndoa umasikini? Kilichopo ni kukamata vyombo vyote vinavyotangaza hilo huku wananchi wakiwa bado masikini sana.
 
Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli risk ya kupata COVID-19 in Tanzania bado ni kubwa,ya wastani au iko chini au haipo kabisa na na ajiridhishe kuwa maambukizi ni kweli yako juu na yanaendelea kuwa juu kama ubalozi wa marekani unavyodai? Sababu tamko lao ubalozi sio la Mungu linahitaji independent verification ya Mwandishi kabla kuchapisha

Pili Alitakiwa ajiridhishe Kupitia wizara ya afya athibitishe ikiwa ni kweli hospitali zetu zina uwezo na mdogo kama ubalozi ulivyosema na kuwa zilizopo zinaweza kulemewa kama zinazodaiwa na ubalozi

Mbona Serikali inatangaza COVID-19 imeisha/imepungua na habari hizi zinatangazwa na vyombo vya habari bila ya scientific prove yoyote na hakuna chombo chochote cha habari kilichopewa adhabu yoyote?
 
Wanazingua wawafate US embassy nasio kuanza kuwaonea madogo
 
Hao kama chombo cha habari wametoa taarifa kutoka kwenye chanzo kinachoeleweka, ni jukumu la mamlaka husika na wao kutoa taarifa zao siyo mamlaka nyingine kukitisha chombo cha habari kwa kutoa taarifa zisizopendwa na serikali.

Huko tuendapo Vyombo vya habari vitatishwa kwa kutangaza ushindi wa timu za nchi nyingine dhidi ya taifa au timu za nchini.

Siyo kazi ya chombo cha habari kutangaza taarifa zipendwazo na serikali, serikali isitafsiri uzalendo kwa mtindo wa muwamba ngoma.

Itoshe tu kusema kwamba ilichokifanya TCRA ni WENDAWaZIMU.
Tuwaonee huruma hao TCRA. Pengine nao wanalinda mikate yao tu. Chanzo cha tatizo sote tunakijua vizuri.
 
Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli risk ya kupata COVID-19 in Tanzania bado ni kubwa,ya wastani au iko chini au haipo kabisa na na ajiridhishe kuwa maambukizi ni kweli yako juu na yanaendelea kuwa juu kama ubalozi wa marekani unavyodai? Sababu tamko lao ubalozi sio la Mungu linahitaji independent verification ya Mwandishi kabla kuchapisha

Pili Alitakiwa ajiridhishe Kupitia wizara ya afya athibitishe ikiwa ni kweli hospitali zetu zina uwezo na mdogo kama ubalozi ulivyosema na kuwa zilizopo zinaweza kulemewa kama zinazodaiwa na ubalozi
Mwandishi aliwasaidia ubalozi kufikisha ujumbe kwa walengwa wao(wafanyakazi wa ubalozi na wamarekani waishio tanzania) kuna ubaya?
 
Hawa jamaa safari hii wanazikwa rasmi
Hilo lingewezekana kama mchakato mzima wa uchaguzi ungekuwa sawa, hapa mshindi ni yule atakayetangazwa na sio atakayepata kura nyingi!!! Ndio maana licha ya majivuno mengi lakini, hawajiamini kama wana nchi wanawaelewa.
 
Uandishi unatakiwa ku balance hasa kwenye issue sensitive kama hizo.Upande wa serikali haukuulizwa na hizo habari mwandishi ha ku confirm na wizara ya afya

Pia hilo tamko la ubalozi wa marekani lina walakini kisayansi ona unasema kuwa kitisho cha maambukizi ya virusi vya corona jijini Dar es Salaam na maeneo mengine kipo juu mno kwa sababu serikali haijatoa takwimu za ugonjwa wa COVID19 !!!!!!

Hivi kiini cha maambukizi ya Corona kuwa kubwa ni sababu ya takwimu? takwimu ndizo zinasambaza corona? takwimu ndio wadudu wa corona? Na kuwa tiba ya Corona ni takwimu ukizitoa ndipo watu wanapona!!!

Mwandishi alitakiwa ajiridhishe kisayansi kama ni kweli takwimu ndizo zinasambaza Corona kuwa kadri unavyotoa takwimu sanaaaa Corona inapungua!!! Marekani wanatoa takwimu sana kila saa Corona mbona haishuki?
Kwaiyo unataka mwandishi ageuke wanasayansi
 
Ingekuwa nchi yoyote hiki chombo cha habari kingepigwa ban.

Yaani hadi serikali inamwita kaimu balozi mwenyewe wa Marekani na kumtaka atoe maelezo halafu ninyi kama chombo cha habari mnaendelea kutoa habari hizo.
Acha kuwa toilet paper ya serikali,badala kuwa mkweli nafsi yako ipone!
 
Tuwaonee huruma hao TCRA. Pengine nao wanalinda mikate yao tu. Chanzo cha tatizo sote tunakijua vizuri.
Ukitaka kudumu kwenye cheo chako ni lazima na wewe uone Kane, unatoa mchango gani wa uonevu,, ili kimfurahisha jamaa!!! Ndio yale yale,mzungu akikusifia uchumi wako unakuwa kwa kasi, sifa kwake, ila akikwambia uchumi wako una sua sua, huyo ni beberu!! Anatumwa!
 
Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli risk ya kupata COVID-19 in Tanzania bado ni kubwa,ya wastani au iko chini au haipo kabisa na na ajiridhishe kuwa maambukizi ni kweli yako juu na yanaendelea kuwa juu kama ubalozi wa marekani unavyodai? Sababu tamko lao ubalozi sio la Mungu linahitaji independent verification ya Mwandishi kabla kuchapisha

Pili Alitakiwa ajiridhishe Kupitia wizara ya afya athibitishe ikiwa ni kweli hospitali zetu zina uwezo na mdogo kama ubalozi ulivyosema na kuwa zilizopo zinaweza kulemewa kama zinazodaiwa na ubalozi
WB wametoa taarifa kuwa Tz imeingia uchumi wa kati,tumeona haraka haraka vyombo vya habari vimeruka na habari hiyo!Najiuliza mbona waandishi hawajaitwa kuhojiwa kwanini wamerusha habari hiyo bila kujiridhisha kama kuna ukweli?Au ruksa kwa habari nzuri ila kwa mbaya ndio inakuwa nongwa kureport?
 
Nafikiri baadhi ya wananchi wa Tanzania wanatakiwa either wasome sana kuelewa baadhi ya utendaji wa taasis za serikali, wajibu wa kila mtanzania katika kupata habari sahihi, kutoa habari sahihi na pia walau kujua kwa juu juu nini hasa serikali lengo Lake katika kuwa na sheria flani flani kama hizi za habari ili kabla ya ku- comment, au tasnia hii ya habari inapoitwa ijieleze, basi tujue kosa Lake, na kama ambavyo TRA Ilivyoweza kutoa makosa ya taarifa ya hao online TV.

Suala la kuhabarishana habari ni takwa la kisheria na kikatiba hivyo sio kosa kutoa habari yoyote ile ilimradi ni sahihi na inashabihiana na mfumo wa matakwa ya kisheria.

Yapo mambo mengi yalishafanywa ya kimtandao na magazeti katika kumchafua ndugu Sumaye na Bila kufuata sheria, Sumaye aliweza kushtaki na akalipwa fidia na pia kuombwa samahani mwanzo mwa gazeti kwa siku 7 . sikumbuki ni gazeti lipi. Kwa Hilo hakuna alieweza kuzungumzia Hilo.

Sheria ya habari inataka usawa katika utoaji wa habari ikiwemo kuhoji na kusikiliza pande zote mbili na kisha kuzishapisha zote Bila mwandishi kuongeza chochote chake. (hyo ndo natural justice, means hearing both parties)

Sasa kwenye hayo maudhui, huyo online TV alihoji upande wa ubalozi wa marekani na pia wizarani na kisha kuchapisha zote mbili taarifa? Hilo ndo kosa na si kuwa katoa hyo taarifa. Ila kama angeitoa baada ya kuhoji tu pande mbili hyo hoja ya online TV kuonekna imepotosha taarifa isingekuwepo. Maana ndo sheria inavyotaka. Ni km mahakamani lazima pande zote mbili zitoe maelezo yake.

Sasa sijui mtu na frustration zake anaongea hoja za kijinga tu Bila kujua taratibu. Nafikiri wasomi wa Tanzania kama mtu anajua tu kiingereza, huo sio usomi, usomi ni kuelewa jambo fulani.

Pia si kila kitu serikali inaonea, jamii ya sasa inapenda uwekezaji katika sector mbali mbali lakini napo wawe wanaajiri wanasheria au taasis ambazo zinaweza kuwa zinasaidia kuwapa ushaur kuanzia wafanyakazi wao, na taasis nzima ili kuepuka masuala ya haya ya either wafanyakazi au mtu mmoja mmoja kuwa na ushabiki wa vyama, au kuwa na chuki na serikali, au kuona kuwa hela ni nzuri kuzidi vyote hata km ni kuiabisha nchi yako sawa tu ilimradi utauza sana uwe billionaire mtoto. Baadae mnasema mnaonewa.

Mi sijaona kenya wakifanya haya nchini kwao, hawawez toa taarifa za uzushi km huu. Tujifunze kuwa WAZALENDO
Kwa kuangalia Press Release iliyotolewa, Mwandishi alitakiwa ajiridhishe nini kwa mfano?!

Alitakiwa ajiridhishe kwanza kwamba Press Realese husika ni kweli imetolewa na US Embassy, au?!

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli US Department of States imetoa a Global Level 4 Advisory for COVID-19?

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli risk ya kupata COVID-19 in Tanzania bado ni kubwa?

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli Ubalozi wameshauri wananchi wao kuendelea kuchukua tahadhari?

Alitakiwa ajiridhishe kwanza kama ni kweli health facilities ZINAWEZA kuelemewa?

Alitakiwa ajiridhe kwanza ikiwa ni kweli uwezo mdogo wa hospitali zilizopo INAWEZA kusababisha kuelemewa?

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli serikali imeondoa vikwazo vya usafiri kwa international flights?

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli US Embassy inafahamu kuna mashirika kadhaa ya ndege yamepanga kufanya safari zake kuingia Tanzania

Alitakiwa ajiridhishe kwanza ikiwa ni kweli mashirika ya ndege yaliyotajwa yanapokea online reservation?!

Or, ni kipi hasa alitakiwa kwanza kujiridhisha kwa kuangalia the said Press Release ambayo ni:-
 
Hii nchi ilipofikia hata kuihurumia ni sawa na kupoteza muda tu .

Zipo taarifa kwamba Channel hii ya mitandaoni imefungiwa kwa kosa la kunakili taarifa ya ubalozi wa Marekani ya kutahadharisha kuhusu uwepo wa corona nchini Tanzania .

Kama hii ndio sababu basi bila shaka chombo pekee cha habari kibaki kuwa TBC , maana hawa ndio mnaoweza kuwatumia mtakavyo , hii ni sababu duni mno kuitumia kufungia chombo cha habari .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sasa kwa nini Polepole anajiona keki kuitwa na TCRA?!
 
Back
Top Bottom