Kware: Ufugaji bora wa Kware, Na faida ya bidhaa zitokanazo na Kware

Ndugu Deo Benjamin ni kware wa muda(umri) gani anafaa kuliwa kama nyama?
 

Bwana deo ni kware wa umri gani wanafaa kuliwa kama nyama?
 
Wa prorini wanatoa wapi vyakula vya ivo?
 
Ndugu Deo Benjamin ni kware wa muda(umri) gani anafaa kuliwa kama nyama?

Mkuu kwale kuanzia week saba anafaa kuliwa kama nyama, kwa kuwa anakuwa mature na kwa majike wanakuwa wanataga tayari.
 
Wa prorini wanatoa wapi vyakula vya ivo?

Mkuu Protein na madini vinapatikana kwenye chakula na udogo na hata baadhi ya mimea. mfano ganda la yai wa kuku wa kienyeji au kwale lina calcium kwa kiasi kikubwa sana.
 
Mkuu Deo Benjamini naomba unipatie msaada wa kimawazo march 14 nilifanikiwa kununua kware kwa mujibu wa muuzaji alidai wana wiki 3 niliwapa chakula cha kutosha na maji ila walipitiliza hadi mwez wa 5 bila kutaga nilikuwa nikimpigia simu ila hakunipa mbinu mbadala ila walau sasa mefarijika kidogo wametaga mayai 2 ila hawajataga tena. Sasa mkuu hawa watakuwa na tatizo gani? Huwa nawapa chakula cha vifaranga chenye mchanganyiko mbalimbali
 
Last edited by a moderator:

Mr. Mangi kuwa makini sana biashara hii imeingiliwa na makanjanja wengi sana, nunua kwale wako kwa watu wanaojulikana, nimenunua kwale kwa Deo Benjamini - Kwale Bora na kwale wangu walianza kutaga siku ya 45, yaani week sita na siku tatu, nadhani ni matunzo ya utotoni, chanjo na chakula...ngoja tumsubiri Deo

NOTE: Deo alinishauri ninunue Kwale wa week tatu kwa kuwa sikuwa na utaalamu wa ufugaji, na kipindi hicho kwale wale alikuwa ameshawapa chanjo zote.
 

nilinunua kwa mtu anaefahamika ambae ni suzan aliyerushwa ktk kipindi cha amka na badilika ila pamoja na umaarufu wake kuna mambo hayakwenda sawa alinishauri ninunue wa wiki 3 nilimtumia hela na mzigo akanitumia, ila mzigo hakufunga yeye niligundua hilo ktk maongezi kupitia simu baada ya kutaka kujua uwiano wa madume na majike akashindwa nijibu wale kware walikuwa wadogo sana nilitilia shaka umri wao ila nikajitahidi kupuuzia uchakachuaji? Sasa sijui nifanyeje hapa moshi mjini hawapogi kabisa karibia mtaa mzima habari zimeenea nafuga kware watu wanakuja kuwaona na wanatamani niwauzie ila kila siku nawaahidi wasubiri watage nitawapa mbegu, sasa sijui niwape nini ili watage
 

Mangi heshima mbele mfugaji mwenzangu.

Moja kuna uwezekano kwale uliouziwa hawakuwa wa week tatu, kuna wafugaji hawana imani na kwa kuwa ufugaji huu ni mgeni anaweza kukupatia kwale wa week moja akakwambia ni wa week tatu, na kwa kuwa wewe ni mgeni hutaweza kugundua, Sasa twende kwenye issue ya msingi:-
1. Je walipata chanjo zote, yaani newcastle siku ya saba, Gumboro siku ya 14 na newcastle tena siku ya 21?
2. Je toka week ya kwanza mpaka ya tano uliwalisha chakula gani na uliwanywesha nini, je unaweza kunipa mchanganyiko wa chakula ulichokuwa unawalisha, na nini uliweka kwenye maji? na vile vile baada ya week ya tano?..kumbuka kwale wakiwa wazito na wenye mafuta mengi huwa hawatagi, ni kama ndege wengine
3. Je uliweka nini kwenye chakula kama chanzo cha zink kwenye chakula chako, fahamu kwale wanahitaji zink ya kutosha kwenye chakula chao.
4. Je ratio ya madume na majike ikoje?.

Tuanzie hapo kwanza
 

swali namba
1. Hapo sijui maana alidai wana wiki 3
2. Kwa mujibu wa muuzaji alidai wana wiki tatu hivyo kuanzia hapo niliwanunulia chakula cha vifaranga wa kuku upande wa maji alinishauri niwachanganyie glucose na nilifanya hivyo ila kuna wakati fulani nilichanganya aloe vera na mwarobaini nikawapa
3. Kwa kweli hapa sikuweka chochote zaidi ya hicho chakula
4. Hapa pia sijui hata yeye hajui pia kwani inaonekana mzigo hakuuandaa yeye ila kuna njia alinipa ya kuwakagua nyeti zao nilifanya hivyo ila sikuona tofauti nilidhamiri kumjulisha hilo ila kutokana na mihangaiko ya kila siku sijamjulisha hadi sasa. Asante
 

Deo Benjamin
 
Last edited by a moderator:

1. Boss nataka kujua kwenye huo mchanganyiko wa chakula kulikuwa na nini vipi uliwapa chakula cha layers or broilers cha dukani au ulipewa formula ya mchanganyiko maalum wa chakula cha kwale?

2. Ulishauriwa uwape glucose mara baada ya kuwapokea, kwa kuwa kwenye usafirishaji kwale hupata uchovu kwa hiyo hushauriwa kuwapa glucose for 8hrs na baada ya hapo una switch back kwenye vitamins, inaonekana kwale wako hawakupata vitamins za kutosha na hii husababisha kwale wapate shida kwenye utagaji.

Mwisho: Kwale wako hukuwapa chakula bora chenye formula nzuri kwa ajili ya kwale, probably ulikuwa unawalisha broiler mash na vilevile hawakupata vitamins kabisa, nitakuPM formula ya Quail Feed ambayo iko kwenye stages tatu
 

nitashukuru mkuu, chakula nilikuwa nanunua kilichotengenezwa tayari sikuzingatia ni kwa ajili ya broilers au layers naona tatizo kubwa litakuwa kwenye lishe na vitamini kwani hata sasa asubuhi wanakuwa kama vile wanawika kama kuku, nitashukuru kwa msaada wako niweze kuwakomboa
 

Worry out kaka, nitakutumia kwa DM
 
Naomba mtitiriko mzuri na sahihi ya wa kuwapa Chonjo kuku wa nyama yani broilers. Kuanzia siku ya kwanza kuingia bandani. Nahitaji mtiririko huo. Pls Kwa mwenye ufahamu tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…