Kaka Kwale wako wanasumbuliwa na mafua na si ugonjwa wa macho, Nenda kwenye duka la dawa za mifugo na uwaeleze kuwa kwale wako wanamafua yaliyopelekea kuvimba macho, hatua ya kuvimba macho ni hatua ya juu ya ugonjwa wa mafua na hii itasababisha upungufu katika kutaga, tegemea kukusanya mayai machache kwa muda huu.
Kinga: Jitahidi sana usichanganye kwale wako na mifugo wengine na waepushe kwale wako na Vumbi, mara nyingine vumbi hutokea kwenye chakula (chick mash), jitahidi kisitoe vumbi pindi unapowawekea kwenye vyombo vyao vya chakula.
NOTE: Dawa za mafua ziko nyingi chukua dawa za Holland na ile ya poda na si maji.