Nimebatizwa moroviani nikiwa mtoto,then nikaja batizwa tena Catholic nikiwa primary usiku Wa kuamkia pasaka,
Yan nimebatizwa mala mbili Lisa tu chet changu cha moroviani hakikupatikana
But mpk sasa nasubiri ubatizo Wa ATHEISM nishaaachana huko toka nimalize seminary
Hongereni na kila kher wakuuu
Mpendwa zinginary pamoja nanyi nyote mnaonisikiliza hivi sasa, napenda mjue kuwa hamwezi kamwe kukiishi kitu ambacho hukijui. Hivyo kwasababu hiyo itakupasa kufanya mafundisho ya kanisa Katoliki, na kanisa linapaswa kuhakikisha kuwa umeyafahamu vyema. Kanisa linatuhoji kama tmekubali mafundisho hayo, nasi tunakiri kanuni ya Imani mbele ya waumini wenzetu wote; na huo ndiyo muhtasari wa mafundisho ya kanisa Katoliki; na hapo utapokelewa rasmi.
Lakini ikumbukwe kwamba, kama hukubatizwa kadiri ya utaratibu wa Kanisa Katoliki yaani, kama unavyo batizwa maneno haya, Fulani na kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu ambayo yataambatana na kumwagiwa au kuzamishwa kwenye maji kutokana na mazingira na tamaduni husika hapa nazungumzia maji siyo kimiminika kingine chochote hayakusikika wala kutumiwa basi utakapoamua kujiunga na kanisa Katoliki basi utabatizwa. Nakama ulikwisha batizwa kwa namna sahihi basi kanisa litakamilisha ubatizo wako kwa kukupaka mafuta matakatifu ya krisma ambayo kwa uhakika katika adhehebu mengine hayapo.
Wapendwa mnaonisikiliza hivi sasa, haya ni mafuta yaliyotiwa manukato na kuwekwa wakfu na Askofu. Mafutahayo huashiria paji la Roho Mtakatifu kwa mbatizwa mpya. Hapo mbatizwa anakuwa Mkristo , yaani “mpakwa” na Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu nafsi ya tatu. Huyu mpakwa anaingizwa katika Kristo, na hivyo anashiriki ukuhani, unabii na ufalme pamoja na Kristo.
Mpendwa zinginary e, baada ya kupokelewa hivyo basi utapewa mafundisho mengine zaidi kwa ajili ya kipaimara ili uweze kuwa askari hodari wa Yesu Kristo kwa maneno na matendo.
Mpendwa zinginary nasisitiza tena mafundisho ni lazima na tena ujue kuwa mafundisho mengi ya dhehebu ulilokuwepo hayalingani na yale ya Kanisa Katoliki.. Na ukisema kufanya tena kama ulivyouliza haupo sahihi, hata kidogo kwani mafundisho uliyofanya ni sawa na ya Kanisa Katoliki? Mfano mzuri umesema unashiriki meza ya Bwana kumbe Kanisa Katoliki lina Ekaristi Takatifu na siyo meza ya Bwana kwani tunaamini kabisa katika maumbo ya mkate na divai padre ambaye ni mwanadamu kama sisi kwa uwezo alio nao yafanya maumbo hayo kuwa mwili na damu yake Mwokozi Kristo. Usiogope, amini.
Kwa mantiki hiyo kanisa Katoliki haliwezi kamwe kumpokea mtu kutoka nje na kisha bila mafundisho kumfanya muumini wake haiwezekani. Katika Kanisa Katoliki ni lazama upate mafundisho tena mafundisho ya kina kwa utaratibu kabisa likiisharidhika kweli umeiva katika mafundisho basi litakupokea; kinyume chake halitakubali kumpa mtu kitu asicho kijua. Mpendwa Amelye, pamoja nanyi nyote mnaonisikiliza hivi sasa, mzazi hawezi kumpa mtoto mdogo kitu chenye thamani kubwa akichezee la hasha! Mpendwa mafundisho ya imani yetu sisi Wakatoliki ni kitu cha thamani sana na hivyo Kanisa linapenda kila anayejiunga nasi ajue thamani hiyo kwanza.
Moja kati ya mafundisho muhimu utakayofundishwa mpendwa AMALYE ni kuhusu misingi ya Imani yetu, sakramenti za kanisa Katoliki ambazo zipo saba. Utafundishwa Imani yetu Juu ya Mungu Utatu Mtakatifu, mafundisho kuhusu Bikira Maria na mengine mengi yatakayo kuimarisha katika maisha yako ya kila siku kama Mkatoliki. Mpendwa Amalye ni muhimu kujua pia Kanisa likisha kukupokea siyo ndiyo mwisho wa mafundisho, la hasha! bali utaendelea kufundishwa zaidi na zaidi kuhusu imani hiyo. Zaidi ya hayo Kanisa litapenda kuona unaiishi hiyo imani kwa matendo. Mfano kanisa litapenda likuone ukihudhuria kwenye jumuiya ndogo ndogo kwani kutoka huko tunaimarishana; litataka likuone unalipa zaka kwani ndiyo shukrani yako kwa Mungu; na tena utapaswa kulihudumia Kanisa na huko ndiyo hasa kutafsiri mafundisho ya kanisa na kuyaweka katika maisha ya kila siku.
Mpendwa zinginary, tunaamini, ndani ya jumuiya ndogondogo utawafahamu wa Kristo wenzako, utapata nafasi za kuwahudumia wagonjwa na wenye shida mbalimbali na utasali pamoja na wanakanisa. Kwani walipo wawili watatu Mungu yupo pale.
Mpendwa Amelye, kwa uhakika kanisa Katoliki litakukaribisha lakini ni lazima ukubali masharti ambayo kanisa hilo limejiwekea. Kanisa lenyewe linasema: “Ili kuingia katika nyumba ya Mungu, yampasa mtu kuvuka kizingiti, alama ya kupita kutoka ulimwengu uliojeruhiwa na dhambi kuuendea ulimwengu wa uzima mpya ambako watu wote wameitwa. Kanisa linalo onekana ni alama ya nyumba ya Baba ambako taifa la Mungu huelekea na ambako Baba “atafuta kila chozi katika macho yao.” Kwa sababu hiyo kanisa ni pia nyumba iliyo wazi na tayari kukaribisha watoto wote wa Mungu. (Kat.ya Kanisa Katoliki namba 1186)