Kwaresma 2018 Special thread...

Kwaresma 2018 Special thread...

Ndugu yangu huu uzi sio kwa ajili ya mabishano

Mabishano au tunahoji, misingi ya hii funga: mchangiaji hapo juu amesema kufunga kwenu ni kuacha unachopenda tu...kama kununua nguo, kunywa bia, kujamiiana..sasa utuelimishe na yesu naye alifunga KIULAINI HIVYO?
 
Mbona hujajibu swali unazunguka zunguka kama feni.

Swali limeulizwa je na Yesu alifunga kama mnavyofunga nyie wakristo nyakati hizi?

Yaani Yesu nae katika zile siku zake 40 za kufunga alikua anakula kwa kujinyima kama nyie?
sijazunguka nimeshajibu na ndiyo maana aliyeniuliza karidhika na jibu. Na cha msingi si kufunga kula kama unavyotaka nikujibu halafu yaonyesha na wewe ni kama JPM anti kiingereza ama hukielewi kama ungekielewa usingeuliza tena swali maana jibu limejitosheleza. Cha msingi ungeomba wanaolewa kiingereza wakutafsirie mkuu.
 
Mabishano au tunahoji, misingi ya hii funga: mchangiaji hapo juu amesema kufunga kwenu ni kuacha unachopenda tu...kama kununua nguo, kunywa bia, kujamiiana..sasa utuelimishe na yesu naye alifunga KIULAINI HIVYO?
Unaelewa maana ya self denial? ndiyo maana kuu ya mfungo wa wakristu unaweza kuamua kuto kula. self denial ni kitu muhimu sana katika mfungo hata wa waislamu ila tatizo wafungaji hawajui maana kufunga wanadhani kuacha kula, Hujaona watu wanafunga kuanzia alfajiri mpaka jioni kula na kufuta sigara lakini ikifika wakati wa futuru wanakimbilia kuvuta sigara sasa sijui kama kweli huo nimfungo.

Sasa wakristu wakatoliki walilijua hilo ndiyo maana wamewafundisha watu wao kuwa maana ya kufunga siku tu kuacha kula bali ni kujikana mwenyewe na matendo uliyoyazoea na kuyaacha kwa siku hizi 40 huku ukisali na kufanya toba. Na kile kitu ulichkiokoa katika kujikana basi wapatie wale ambao hawana uwezo. Sasa sijui ueleweshwe vipi kuhusu hili ili uelewe. Ni kiswahili rahisi kabisa,

Yesu alifunga kwa Imana za kiyahudi ambazo baada ya hapo hakuna mahala popote pale katika Biblia panaonyesha kuwa alifunga siku arobaini, zaidi tunaonyeshwa kuwa alifanya party badala ya kufunga siku ile alipokamatwa na kusurubiwa ilikuwa wakati wa mfungo lakini alifanya sherehe na wafuasi wake. Usipende kufananisha kwaresma na Ramadhani ya waarabu.
 
a881de1d0c0ea2b567371d338a965b01.jpg
 
Wapendwa katika Kristo
Tumsifu yesu Kristo...

Nawakaribisha waumini wote wa kanisa Catholic na wengine wote wanaoshiriki mateso ya bwana Yesu kristo kwa kufunga na kujielekeza mbele zake MUNGU kipindi hichi cha KWARESMA.
Nawaalika sasa tuweze kutiana moyo, kukumbushana, kufundishana kupitia uzi huu.
Kama una document za kidini weka hapa, nyimbo, picha, sala, miatari ya biblia weka hapa...

Wako katika kristo Da'Vinci..

Tunakimbilia..........
Mkuu inaonekana watu wengi humu hawajui kabisa nini maana ya kufunga kwa wakristu labda ungewafahamisha na kuwaeleza kuwa kufunga kwa wakristu hakumaanishi kuacha kula tu kwa siku hizi 40 bali zaidi zaidi ni kitu kwa kiingereza kinaitwa Self denial na hapa ni maelezo kidogo kwa kiingereza.

Self-denial can constitute an important element of religious practice in various belief systems. An exemplification is the self-denial advocated by several Christian confessions where it is believed to be a mean of reaching happiness and a deeper religious understanding, sometimes described as 'becoming a true follower of Christ'. The foundation of self-denial in the Christian context is based the recognition of a higher God-given will, which the Christian practicer choose to adhere to, and prioritize over his or her own will or desires. This can in daily life be expressed by renunciation of certain physically pleasureable, yet from a religious stand-point inappropriate activities, sometimes referred to as 'desires of the flesh', which e.g. could entail certain sexual practices and over-indulgant eating or drinking. In the Christian faith Jesus is often mentioned as a positive example of self-denial, both in relation to the deeds performed during his life, as well as the sacrifice attributed to his death.
 
Ubatizo ni moja kati ya sakramenti saba alizotuachia Bwana wetu Yesu kristo. Sakramenti nyingine ni pamoja na Kipaimara, Ekaristi Kitubio,Mpako wa Wagonjwa,Daraja Takatifu na Ndoa. Sakramenti zote 7 zinagusa hatua zote na nyakati zote muhimu za maisha ya mkristo. Zinayajalia maisha ya imani ya mkristo, kuzaliwa kukua,kupona na utume.Sakramenti ya Ubatizo ni msingi wa maisha yote ya kikristo, lango la kuingilia uzima katika roho na mlango unaowezesha kupata sakramenti zingine. Kwa njia ya ubatizo tunafanywa huru katoka dhambi na kuzaliwa upya kama watoto wa Mungu. Sakramenti hii huitwa ubatizo kutokana na madhehebu ya msingi ambayo kwayo hufanyika. Kubatiza kwa Kigiriki (Baptaizein) humaanisha “kutumbukiza” au “kuzamisha” ndani ya maji alama ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo ili uwe kiumbe kipya.

Yeyote anayepokea ubatizo bila kuwa na imani hapati neema za sakramenti hiyo. Ndiyo maana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kwenda duniani alisema “aaminiye na kuokoka atabatizwa na asiyeamini atahukumiwa” Mk16:16. Pia anawaeleza mitume wajibu wa kuhakikisha watu wote wanahubiriwa na neno la Mungu na kubatizwa akisema “nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Mt 28:19. Swali la kujiuliza na kuangaliwa hapa ni lini ubatizo ufanyike, je, mtoto mdogo asiyeweza kuamini anaweza kubatizwa au tusubiri hadi awe mkubwa?
Katika suala hili ni kweli kwamba ubatizo ni sakramenti ya imani lakini lazima tukumbuke kuwa imani ina lazima ya jumuia ya waamini, ni katika imani ya kanisa tu kila mwamini aweze kusadiki. Imani inayodaiwa kwa ubatizo si imani kamili na komavu bali ni mwanzo tu ambao lazima ukue. Ndiyo maana mwenye kubatizwa huulizwa “unataka nini katika kanisa la Mungu?” naye hujibu “Imani”. Kwa hiyo iwe amebatizwa akiwa mtoto au mkubwa imani lazima ikue baada ya ubatizo. Na ili neema ya ubatizo iweze kukua, msaada wa mzazi ni wa lazima. Hapo pia ni kazi ya wasimamizi wa kiume na wa kike ambao lazima wawe waamini imara, wenye uwezo na walio tayari kumsaidia mbatizwa katika safari ya maisha ya kikristo. Wajibu wao ni kweli kazi ya kanisa. Jamii yote ya kanisa ina sehemu na wajibu katika maendeleo na katika kutunza neema iliyopokewa kwa ubatizo.
Nimebatizwa moroviani nikiwa mtoto,then nikaja batizwa tena Catholic nikiwa primary usiku Wa kuamkia pasaka,

Yan nimebatizwa mala mbili Lisa tu chet changu cha moroviani hakikupatikana

But mpk sasa nasubiri ubatizo Wa ATHEISM nishaaachana huko toka nimalize seminary

Hongereni na kila kher wakuuu
 
Lengo la ujio wa Yesu duniani lilikuwa si kuja kutuonesha staili za kufunga...hilo halikuwa lengo la ujuo wake
 
Nimebatizwa moroviani nikiwa mtoto,then nikaja batizwa tena Catholic nikiwa primary usiku Wa kuamkia pasaka,

Yan nimebatizwa mala mbili Lisa tu chet changu cha moroviani hakikupatikana

But mpk sasa nasubiri ubatizo Wa ATHEISM nishaaachana huko toka nimalize seminary

Hongereni na kila kher wakuuu
Mpendwa zinginary pamoja nanyi nyote mnaonisikiliza hivi sasa, napenda mjue kuwa hamwezi kamwe kukiishi kitu ambacho hukijui. Hivyo kwasababu hiyo itakupasa kufanya mafundisho ya kanisa Katoliki, na kanisa linapaswa kuhakikisha kuwa umeyafahamu vyema. Kanisa linatuhoji kama tmekubali mafundisho hayo, nasi tunakiri kanuni ya Imani mbele ya waumini wenzetu wote; na huo ndiyo muhtasari wa mafundisho ya kanisa Katoliki; na hapo utapokelewa rasmi.
Lakini ikumbukwe kwamba, kama hukubatizwa kadiri ya utaratibu wa Kanisa Katoliki yaani, kama unavyo batizwa maneno haya, Fulani na kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu ambayo yataambatana na kumwagiwa au kuzamishwa kwenye maji kutokana na mazingira na tamaduni husika hapa nazungumzia maji siyo kimiminika kingine chochote hayakusikika wala kutumiwa basi utakapoamua kujiunga na kanisa Katoliki basi utabatizwa. Nakama ulikwisha batizwa kwa namna sahihi basi kanisa litakamilisha ubatizo wako kwa kukupaka mafuta matakatifu ya krisma ambayo kwa uhakika katika adhehebu mengine hayapo.
Wapendwa mnaonisikiliza hivi sasa, haya ni mafuta yaliyotiwa manukato na kuwekwa wakfu na Askofu. Mafutahayo huashiria paji la Roho Mtakatifu kwa mbatizwa mpya. Hapo mbatizwa anakuwa Mkristo , yaani “mpakwa” na Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu nafsi ya tatu. Huyu mpakwa anaingizwa katika Kristo, na hivyo anashiriki ukuhani, unabii na ufalme pamoja na Kristo.
Mpendwa zinginary e, baada ya kupokelewa hivyo basi utapewa mafundisho mengine zaidi kwa ajili ya kipaimara ili uweze kuwa askari hodari wa Yesu Kristo kwa maneno na matendo.
Mpendwa zinginary nasisitiza tena mafundisho ni lazima na tena ujue kuwa mafundisho mengi ya dhehebu ulilokuwepo hayalingani na yale ya Kanisa Katoliki.. Na ukisema kufanya tena kama ulivyouliza haupo sahihi, hata kidogo kwani mafundisho uliyofanya ni sawa na ya Kanisa Katoliki? Mfano mzuri umesema unashiriki meza ya Bwana kumbe Kanisa Katoliki lina Ekaristi Takatifu na siyo meza ya Bwana kwani tunaamini kabisa katika maumbo ya mkate na divai padre ambaye ni mwanadamu kama sisi kwa uwezo alio nao yafanya maumbo hayo kuwa mwili na damu yake Mwokozi Kristo. Usiogope, amini.
Kwa mantiki hiyo kanisa Katoliki haliwezi kamwe kumpokea mtu kutoka nje na kisha bila mafundisho kumfanya muumini wake haiwezekani. Katika Kanisa Katoliki ni lazama upate mafundisho tena mafundisho ya kina kwa utaratibu kabisa likiisharidhika kweli umeiva katika mafundisho basi litakupokea; kinyume chake halitakubali kumpa mtu kitu asicho kijua. Mpendwa Amelye, pamoja nanyi nyote mnaonisikiliza hivi sasa, mzazi hawezi kumpa mtoto mdogo kitu chenye thamani kubwa akichezee la hasha! Mpendwa mafundisho ya imani yetu sisi Wakatoliki ni kitu cha thamani sana na hivyo Kanisa linapenda kila anayejiunga nasi ajue thamani hiyo kwanza.
Moja kati ya mafundisho muhimu utakayofundishwa mpendwa AMALYE ni kuhusu misingi ya Imani yetu, sakramenti za kanisa Katoliki ambazo zipo saba. Utafundishwa Imani yetu Juu ya Mungu Utatu Mtakatifu, mafundisho kuhusu Bikira Maria na mengine mengi yatakayo kuimarisha katika maisha yako ya kila siku kama Mkatoliki. Mpendwa Amalye ni muhimu kujua pia Kanisa likisha kukupokea siyo ndiyo mwisho wa mafundisho, la hasha! bali utaendelea kufundishwa zaidi na zaidi kuhusu imani hiyo. Zaidi ya hayo Kanisa litapenda kuona unaiishi hiyo imani kwa matendo. Mfano kanisa litapenda likuone ukihudhuria kwenye jumuiya ndogo ndogo kwani kutoka huko tunaimarishana; litataka likuone unalipa zaka kwani ndiyo shukrani yako kwa Mungu; na tena utapaswa kulihudumia Kanisa na huko ndiyo hasa kutafsiri mafundisho ya kanisa na kuyaweka katika maisha ya kila siku.
Mpendwa zinginary, tunaamini, ndani ya jumuiya ndogondogo utawafahamu wa Kristo wenzako, utapata nafasi za kuwahudumia wagonjwa na wenye shida mbalimbali na utasali pamoja na wanakanisa. Kwani walipo wawili watatu Mungu yupo pale.
Mpendwa Amelye, kwa uhakika kanisa Katoliki litakukaribisha lakini ni lazima ukubali masharti ambayo kanisa hilo limejiwekea. Kanisa lenyewe linasema: “Ili kuingia katika nyumba ya Mungu, yampasa mtu kuvuka kizingiti, alama ya kupita kutoka ulimwengu uliojeruhiwa na dhambi kuuendea ulimwengu wa uzima mpya ambako watu wote wameitwa. Kanisa linalo onekana ni alama ya nyumba ya Baba ambako taifa la Mungu huelekea na ambako Baba “atafuta kila chozi katika macho yao.” Kwa sababu hiyo kanisa ni pia nyumba iliyo wazi na tayari kukaribisha watoto wote wa Mungu. (Kat.ya Kanisa Katoliki namba 1186)
 
Umejuaje kama hawajafunga? Kufunga kwa wakristu siyo kama ramadhani bali kujinyima kile kitu ukipendacho kwa siku arobaini na kama ulikua unapenda kunua nguo moya kila wiki unaacha kufanya hivyo kwa siku arobaini na ile hela uliyoiokoa unatoa kama sadaka yako kwa wale wasiokuwa na uwezo. Pili umaweza kufunga baada ya kula milo miwili unakula mulo moja iwe mchana ama usiku lakini zile gharama za lazima ukazitoe kama sadaka. Kufunga kwa wakristu siyo kupiga mbiu bali ni juu yako mfungaji na Mungu wako aliyesirini.

Matthew 16: 16-18
“And when you fast, do not look gloomy like the hypocrites, for they disfigure their faces that their fasting may be seen by others. Truly, I say to you, they have received their reward. But when you fast, anoint your head and wash your face, that your fasting may not be seen by others but by your Father who is in secret. And your Father who sees in secret will reward you.
Ufafanuzi wako ni mzuri mkuu. Wengi wanadhani na wamekaririshwa kuwa kufunga ni kula tuu. Bali kufunga ni kujizuia kufanya kile kitu unakipenda au umekua ukikifanya mara kwa mara. Kufunga ni sala na toba na kujitahidi kumrudia mungu.

Huu uzi udumu unatupa elimu kubwa sana.
Kristu.. Tumaini letu !!
 
JE, KWARESMA NI KWELI SIKU 40? MBONA ZIPO SIKU 46?

Ukijaribu kuhesabu kwa umakini kuanzia Siku ya JUMATANO YA MAJIVU hadi SIKU YA PASAKA utakuta zipo jumla ya Siku 46.
SWALI: JE, KWARESMA NI KWELI SIKU 40?
JIBU: NDIYO.
SWALI: KIVIPI?
JIBU: Jumla ya siku ni kweli zipo 46 kama ifuatavyo:
Jumatatu = 6
Jumanne = 6
Jumatano = 7
Alhamisi = 7
Ijumaa = 7
Jumamosi = 7
Jumapili = 6
JUMLA = 46

Katika kuhesabu Siku za Mfungo, siku zote za Jumapili huwa zinatolewa katika Mfungo yaani Jumapili zote 6. Kwahiyo katika zile siku 46 ukizitoa Siku 6 za Jumapili, zinabaki siku 40 za Kufunga.

SWALI: Kwanini hizo siku za Jumapili zitolewe?
JIBU: Ni kwasababu Siku ya Jumapili yoyote ile tunaadhimisha PASAKA NDOGO yaani tunasherehekea na kukumbuka Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyefufuka Siku ya Kwanza ya Juma yaani Jumapili baada ya Sabato kwisha,(Rejea Mt. 28:1-15). Hivo basi, hatuwezi kufunga siku za Jumapili kwasababu ni Pasaka Ndogo na Pasaka huwa tunasherehekea. Kwenye sherehe siku zote hakuna kufunga maana Bwana Harusi tunakuwa naye tukiukumbuka Ufufuko wake ambao ndio Kilele cha Ukombozi wetu sisi Wakristo.

"BASI ENENDENI MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI WANGU" (Mt. 28:19).
Asante sana na ubarikiwe
 
Nimebatizwa moroviani nikiwa mtoto,then nikaja batizwa tena Catholic nikiwa primary usiku Wa kuamkia pasaka,

Yan nimebatizwa mala mbili Lisa tu chet changu cha moroviani hakikupatikana

But mpk sasa nasubiri ubatizo Wa ATHEISM nishaaachana huko toka nimalize seminary

Hongereni na kila kher wakuuu
Kisheria ukishabatizwa kama mkristu hutakiwi tena kubatizwa labda hukuwaeleza RC kama ulibatizwa.
 
Ndugu yangu huu uzi sio kwa ajili ya mabishano
Nani kaleta mabishano?

Kuuliza ndiyo mabishano

Au ulitaka kila unachoandika uungwe mkono na kila mchangiaji na wala tusiulize maswali?

By the way this is a public forum.

Huwezi kuzuia kupingwa wala kuhojiwa kwa Yale yasiyoeleweka.

Hope you got that right.
 
Back
Top Bottom