Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma inaendelea kutufundisha kuwa

Kuteseka kwetu Kuna maana

Hakuna mateso yasiyo na maana , tuendelee kujitaabisha katika wakati huu wa kwaresma huku kujiwajali masikin na wahitaji

MUNGU MWENYEZI anawapenda sana
 
Zaburi ya 110
1 MWENYEZI MUNGU amwambia bwana wangu keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke adui zako chini ya miguu yako
2 MWENYEZI MUNGU ataeneza enzi yako kutoka siyoni, utatawala juu ya adui zako wote
3 watu wako watakuijia kwa hiari, siku utakapokwenda kuwapiga maadui, juu ya milima mitakatifu watakuijia vijana wako, kama umande unatokeza alfajiri mapema
4, MWENYEZI MUNGU amekuapia wala hatabadili nia yake, wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa melkisedeki
5, BWANA yuko upande wako wa kulia, atawaponda wafalme atakapokasirika
6, Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi, atawaponda viongozi kila mahali duniani
7 mfalme atakunywa maji ya kijito njian, naye atainua kichwa chake juu kwa ushindi.

AMINA
 
YESU KRISTO ni kuhani wa milele mfano wa kuhani melkisedeki

Kuhani melkisedeki alikuwa ni kuhani na mfalme wa mji wa Salem kwa sasa yerusalem
Ndiye kuhani aliye mbariki Ibrahim

Mwanzo 14:17-24
 
Uzi ulikuwa vizuri tu sasa hayo mabishano yenu ya Bibilia na Quran yanaharibu Uzi. Kila mtu Yuko sahihi kwa Imani Yake na mafundisho Yake acheni kubishana waku
Shida jamaa wanakuja na maswali ina bidi tu tuwajibu mtumish
 
Je ukiachana na chakula kwaresma tunafunga kitu gani?

Je kwaresma tunafunga nini?

1 funga dhambi upate utakatifu
2 funga huzuni upate furaha
3 funga uchoyo upate Neema
4 funga majivuno upate utukufu
5 funga kinyongo upate faraja
6 funga wivu upate baraka
 
Tukiwa tunajiandaa na ijumaa ya njia ya msalaba

Ujumbe wa kwaresma
Unasema SIMANENI IMARA KATIKA IMANI 1 WAKORINTHO 16:13
 
Safari ya kwaresma itufundishe kuvumilia na kumjua MWENYEZI MUNGU
 
Safari ya kwaresma itufundishe kujitathimin kiroho
 
Safari ya kwaresma itundufundishe
Kuachana na dhambi kama tumeweza kufunga dhambi katika kipindi cha kwaresma kumbe basi tunaweza kuacha kabisa dhambi
 
Safari ya kwaresma itufundishe kushilia Imani yetu kwa MWENYEZI MUNGU
 
Msalaba wa KRISTO unatufundisha upendo wa hari juu, uliomfanya ajitoe kwa ajili yetu
 
Mwaliko wa kwaresma utufundishe kuokoka na kujipatanisha na MWENYEZI MUNGU
 
Tunapaswa kufanya nini wakati wa kwaresma sisi kama wakristo

1 kusali sana kushiriki misa mara nyingi zaid
2 kutubu zetu mara nyingi
3 kusali kwa bidii rozary, njia ya msalaba na novena mbali mbali
4 kujali na kusaidi wahitaji na masikin
 
Back
Top Bottom