Zaburi ya 110
1 MWENYEZI MUNGU amwambia bwana wangu keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke adui zako chini ya miguu yako
2 MWENYEZI MUNGU ataeneza enzi yako kutoka siyoni, utatawala juu ya adui zako wote
3 watu wako watakuijia kwa hiari, siku utakapokwenda kuwapiga maadui, juu ya milima mitakatifu watakuijia vijana wako, kama umande unatokeza alfajiri mapema
4, MWENYEZI MUNGU amekuapia wala hatabadili nia yake, wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa melkisedeki
5, BWANA yuko upande wako wa kulia, atawaponda wafalme atakapokasirika
6, Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi, atawaponda viongozi kila mahali duniani
7 mfalme atakunywa maji ya kijito njian, naye atainua kichwa chake juu kwa ushindi.
AMINA