Kwawamba Hatarini Kujiuzulu

ZigiZaga

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2011
Posts
951
Reaction score
1,072
ni habari za kuaminika kutoka chanzo cha karibu na kawambwa, chanzo hicho kimeendelea kudokeza kwamba, tangu atangaze matokeo ya kdt cha 4 siku chache zilizopita amekuwa akitumiwa ujumbe wa kumtukana na kutishiwa maisha na baadhi ya watu wasio julikana. 'nimekuwa nkitishiwa maisha, hii ni hatari kwangu na kwa familia yangu,hivyo haina budi ning'atuke kwa ajiri ya usalama wangu na familia yangu'kilisikika chanzo hicho kikimunikuu kawambwa.
 
Wanasiasa,elimu imeingizwa siasa,afya siasa na maisha yetu siasa.
 
Ataweka historia ya uungwana, kwani when things go wrong one should feel responsibility.Japo ni kashfa kutokana na uzembe wake ktk ku-handle swala la waalimu lakini atakuwa ameoga.
 
Ila hata kama akiondoka bado matokeo hayata badilika
 
I gues this can not happen in tz! Ngoja tusubiri!
 
"Mchelea mwana kulia hulia yeye"...kawambwa achia ngazi mwanangu itakustahi na kukujengea heshima kubwa sana.huoni heshima aliyonayo mzee wetu el.?
 
Wadau,

Kuna tetesi kutoka katika chungu kikuu kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru J. Kawamba ameitwa na Ikulu. Ikumbukwe kuwa huyu waziri amekuwa akilalamikiwa na jamii jinsi anavyoongoza wizara hii. Watu wengine wamekuwa wakihusisha uteuzi wake wa uwaziri na ukaribu wake na Rais wa nchi.

Lakini cha kujiuliza:

Ni kweli Waziri huyu anaweza kujiuzulu katika serikali ya kulindana?
Rais anaweza kukubali kumtoa waziri kwa sababu ya kukosa kuwajibika
?
 
Mdau mwenye Namba yake huyo waziri tunaomba atupie hapa ili tuweze kuwasiliana moja kwa moja na huyo Kawambwa kuhusu machungu tuliyokuwa nayo kwa vijana wetu kuambulia sifuri za hatari.
 
sitashangaa Le Mutuz akapewa ubunge wa kuteuliwa achukue nafasi ya waziri wa elimu
 
2012 N.Waziri afya aliwaita waandishi ili atangaze kujiuzuru cha ajabu walipofka pale akasema waondoke hana la kusema
 
Uwajibikaji wa aina hiyo sio sera ya fastjet na chama chake hivyo ataambiwa atulie ni upepo utapita tu!
 
Asije naye akasingizia CHADEMA kuwa wamewapa wananchi namba zake wakati yeye tu ndiye alishendwa kazi. Maskini jamaa ataondoka hana kitu hata kimoja cha kujivunia katika wizara zote alizowahi kupewa
 
Mkuu,
Kichwa cha habari yako hakiendani na habari yenyewe!
Kuitwa IKULU haina maana kwamba kunaashiria kwa Waziri kujiuzuru. Inawezekana ameitwa kupongezwa kwa hao wanafunzi waliopata Div 1-3.

Isitoshe hiyo habari yako bado ni"Tetesi" uliyoitoa kwenye Jungu kuu...Sijui ni Jungu kuu la Mama Ntilie au la Break Point!!
JF ni platform ya Wananchi kupata na kutoa taarifa muhimu zinazohusu nchi yetu, Jamii na Ulimwengu kwa ujumla..naomba tuzingatie Hilo wakati tunaleta
" TETESI KUTOKA KWENYE JUNGU KUU"
 
Uwajibikaji wa aina hiyo sio sera ya fastjet na chama chake hivyo ataambiwa atulie ni upepo tu utapita!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…