Suala la kujiuzulu au kutokujiuzulu kwa Waziri Kawambwa si utatuzi wa matatizo makubwa katika sekta ya elimu. Watanzania tuwe na utamaduni wa kutumia muda kutafakari pale jambo baya au zuri linapotokea. jambo lolote linapotokea ni vema kila mmoja wetu akajiuliza mambo yafuatayo;
- Tatizo ni nini?
- Nini chanzo cha tatizo?
- Je tatizo linatokea kwa mara ya kwanza au linatokea mara kwa mara?
- mazingira ya kutokea tatizo yapoje?
- nini ufumbuzi wa muda mfupi na mrefu (ni9ni kifanyike)