Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Bandugu,
Wahenga walisema, "Aombae hupewa". Juzi tu viongozi wetu wa juu kabisa waliiombea Tanzania ugaidi kwa kusingizia wapinzani wao wa kisiasa kuwa ni magaidi. Na kuwakamata na kuwasweka jela. Na kweli maneno yana nguvu ya kuumba. Uongo na ufedhuli wao umemuumba gaidi wa kweli. Bahati nzuri huyo gaidi wa kweli alikuwa hana hamu ya kuua raia wa kawaida. Leo wanausalama 4 wamepoteza maisha yao na wengine 6 kujeruhiwa katika tukio la ugaidi ambao hauna ubishi kabisa. Viongozi wetu na polisi hawataki kabisa kutamka neno ugaidi katika kile kilichotokea leo mbele ya Ubalozi wa Ufaransa. Badala yake ugaidi ni mpinzani kumtumia mtu shilingi laki 6 na kudai katiba mpya! Kwa kile kilichotokea leo, eti kinaitwa uhalifu tu!
Tujihadhari sana na kile tunachoomba. Solomon alipoambiwa aombe chochote alichotaka, hakuomba utajiri. Aliomba hekima. Na alipewa hekima na Mungu.
Usiku mwema wana-JF.