Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Rais wa Kenya, William Ruto amekutana na viongozi wakuu wa shirika la ndege la kimarekani la Delta katika mpango wa kuwauzia hisa zote 48.9% zinazomilikiwa na Serikali ya Kenya kwenye shirika hilo.
Kenya Airways imekuwa ikitegemea hazina ya Kenya kuweza kujiendesha huku kipindi cha Januari-Juni ikiwa imerekodi hasara ya dola milioni 82 na kipindi kama hicho 2021 kikitoa hasara dola milioni 95.8.
Kwa upande wa Tanzania, ripoti ya mwisho inayopatikana inasema ATCL imepata hasara ya TZS bilioni 36 mwaka 2020/21 kutoka bilioni 60 mwaka 2019/20. Kwasasa shirika hilo ndege zake kubwa inazoziendesha zimepumzishwa huku moja ikishikiliwa kwa madeni.
Serikali chini ya Rais Magufuli iliamua kulifufua shirika la ndege la Tanzania lililokuwa hoi bin taaban kwa kununua ndege mpya na kuliazima shirika hilo.