Kweli biashara ya ndege ngumu, Kenya Airways na ukubwa wote wamechemka. Ruto kuiuza kwa Wamarekani. ATCL vipi?

Kwani ATCL ipo kweli? Ndege zake watu wanazilia timing zikiruka nje ya Tanzania tu watu wanazirukia
 
Marekani nchi inayoongoza kwa utalii duniani hawana Shirika la ndege la Taifa.
Ufaransa na Uingereza ambayo ni mataifa makubwa kwa utalii na kila aina ya biashara duniani hakuna mashirika ya ndege ya Taifa/serikali.
 
Tulia wewe mkenya mbona unatema moto, umekula isije kuwa ni njaa.
 
Ipi biashara ya serikali iliyosimama.
 
Biashara yoyote haifanywi kwa amri za Serikali(by fiat). Biashara Ina amuliwa na soko, demand and supply, strategy, basi!
 
Huwezi kuendelea kiuchumi bila biashara ya anga, Magufuli alijitahidi sana ila wasioipenda hii nchu wanakuja kuondoa zile juhudi ndani ya dakika 0, huwezi kuwa na uchumi imara bila biashara ya usafirishaji chini na angani, Ethiopia walijitahidi, wanajitahidi, na watazidi kwenda mbele. Pumzika JPM ulifanya kazi usiku na mchana kutuonesha yasiyowezekana kumbe yanawezekana, ila kwa wavivu, wachumia tumbo, wasiopata elimu sahihi wanaturudisha nyuma.
Ahsante JPM.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ndege sio bodaboda, inahitaji investment kubwa sana
 
Ni ngumu kwa serikali kumkopesha kila mwenye shirika la ndege. Na fastjet wamekufa kiuendeshaji wao wenyewe.

Ipo dhana potofu kwamba serikali ililiua shirika lile, ni uongo mkubwa. Walikufa wao wenyewe baada ya kushindwa kuajiri mtaalam wa mambo ya ndege kama kanuni za uendeshaji wa mashirika ya ndege zinavyowataka.
 
Mwenye jukumu la kusimamia hizo sheria ni nani kama sio hao serikali?
 
Moja ya makosa makubwa ya magufuli ni kuingiza mabilioni ya pesa za watanzania kwenye biashara ya ndege, hapo alichemka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…