Kweli CCM ina wenyewe, Nape alisema ukweli. Hawa ndio wenye CCM wengine wamevamia!

Kweli CCM ina wenyewe, Nape alisema ukweli. Hawa ndio wenye CCM wengine wamevamia!

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Nape aliposema CCM ina wenyewe wengi hawakumuelewa! Nape alimaanisha kuwa CCM imeshikiliwa na kundi fulani la watu wenye nguvu na ushawishi wao ndio huamua wanamtaka nani ndani ya CCM na nani hawamtaki.

Lakini kwa bahati mbaya kundi hili 2015 lilijichanganya likamkabidhi mshikaji mmoja usukani wakiwa na matumaini tofauti kinyume chake akawageuka na kuleta watu wapya.

Hivyo wenye CCM yao walinyooshwa kweli kweli kwa hiyo hawana jinsi ya kutamba Sasa kwani kupitia Samia wamerudisha udhibiti. Tunaposema wenye CCM tuna maanisha watu wanaosikilizwa na wenye sauti ndani ya CCM na ndio waongoza nchi!

Lakini kwenye hii orodha bahati mbaya Nape nae sio mmoja ya wenye CCM bali ni mpambe tuu kama pole pole!

Hii ndio Orodha ya wenye CCM

1. Jakaya Mrisho kikwete na Familia yake
2. Yusuphu Makamba na Familia yake
3. Mzee Kinana Na familia yake
4. Bulembo na familia yake
5. Dk Shein na Familia yake
6. Ally Hassani mwinyi na Familia yake
7. Samia Suluhu na familia yake
8. Karume na familia yake

Hivyo waliobaki na ambao ni wana CCM na awapo kwenye orodha ya hizo familia wajijue kuwa wao ni wapitaji tuu na sio wana CCM bali ni wavamizi!
 
Wanaobeza Samia & family hamuelewi tu hiyo combi inaaply kwenye Mwinyi family pale juu!

Kuna mdau kasema Nape ni mvamizi kama pole pole nop napinga

Mshua wake marehemu

Mzee Moses Nauye alikua kwenye top chain za CCM na baada ya kufariki familia ya kina Nape akakabidhiwa Mzee Kinana kama father mlezi

Anyway
CCM inawenyewe!
 
Unamaanisha Dada anamiliki Bara na Kaka anamiliki Visiwa???
Za chini chini habari Ndio hiyo na Ndio maana bi mkubwa Jina la mwisho linafanana na Jina la Babu was yule wa visiwani Ili ku mute ubini maana inaonekana senior aliupiga mwingi enzi Hizo Kwa kua na bint outsider the game!
 
Samia hayupo kwenye hiyo orodha ndio mana wanamuona unfit kwenye genge labda wamsajiri kwa makubaliano maalum na hivi ana mtotowanasiasa watamfikiria fikiria
 
Hujui chochote kuhusu CCM, unadhani CCM ni sawa na CHADEMA! Wenye CCM ni wale waliolelewa na kukulia ndani ya CCM. Sio mamluki kama akina Polepole.
 
Familia ya Shein haijawahi kujihusisha na siasa. Afadhali utaje familia ya Salmin Amour, hadi leo yupo mwanafamilia wa Salmini waziri wa makaazi, na alikua waziri wa elimu wakati wa BabuAli Sheni
Nape aliposema CCM ina wenyewe wengi hawakumuelewa! Nape alimaanisha kuwa CCM imeshikiliwa na kundi fulani la watu wenye nguvu na ushawishi wao ndio huamua wanamtaka nani ndani ya CCM na nani hawamtaki...
Familia ya Shein haijawahi kujihusisha na siasa. Babu Ali alikua jeshi la mtu mmoja.

Afadhali utaje familia ya Salmin Amour, hadi leo yupo mwanafamilia wa Salmini waziri wa makaazi, na alikua waziri wa elimu wakati wa BabuAli Sheni..
 
Back
Top Bottom