Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Zamani (kabla ya smartphone) nilikuwa nikitaka kudownload miziki naingia Waptrick. Simu kubwa zilipokuja nikaona process za kudownload kwenye browser ni ndefu kwanza vitu vyenyewe unakuta vimeongezewa au vimepunguzwa mfano ukidownload kupitia mdundo lazima ukiplay mwanzo yasikike maneno "... mdundo.com" basi nilikuwa sipendi kabisa
Ndipo nikakumbuka Waptrick yangu basi nikawa naingia huko kudownload. Mara kukaja application inaitwa videoder ya wahindi sijui ile nayo ikawa safi sana kudownloadia vitu vya YouTube. Si ndiyo saa ngapi Waptrick nayo isivamiwe na matangazo mpaka ikawa siwezi tena kuitumia mara videoder nayo ikawa inagoma
Nikahamia vidmate napo kumeharibika hatari kwa matangazo halafu kuna lile li Phoenix la wanaijeria basi humo kwenye vidmate kila saa linajipendekeza kujidownload. Kwahiyo mpaka sasa sijaona app bora kwa kudownloadia video na audio.
Hayo yote yalikuwa ni nyongeza tu au ukipenda waweza ita utangulizi, hoja yangu sasa ni kuhusu matangazo ya kubet na mikopo ambayo siku hizi mpaka humu jamii forum naona yameanza kuingia sasa. Hivi kuna mtu angedhani TBC wangekuja kuandaa na kushawishi watu kucheza kamari? Kweli Farhia wa ITV ni wa kukwambia weka buku ujishindie!?
Yaani kwa sasa chaneli za madhehebu ya dini tu ndo hakuna kubet! Huko kwenye internet ndo hakuna cha nini wala nani popote utakapoingia wanakubandikia mtangazo wa kubet au mikopo ya riba pwa utajua mwenyewe. Unakuta wewe upo unasoma uharamu wa kamari na riba kwenye moja ya vyanzo mtandaoni halafu muda huohuo linabandikwa litangazo la vitu hivyo hivyo likikushawishi uiendee haramu hiyo
Wenyewe wanakwambia internet haina mwenyewe kwahiyo tangazo lolote popote usishangae. Tena matangazo mengine mengi yanakuja na hutakiwi/huwezi kukata bali usubiri mpaka lifikie sehemu fulani ambayo wanauhakika mpaka hapo utakuwa umesikiliza au kutazama lengo lao ndipo wanakuwekea alama ya kuondoa. Naona kwenye zinaa ni kama vile lengo lilifikiwa sasa nguvu kubwa inahamishiwa kwenye kubet, ulevi na riba siku hizi
Kuna maneno alizungumza Mtume Muhammad (swallallaahu àlayhi wa sallam) alisema kuwa hakitafika kiyama mpaka kufikie zama pombe na kamari vishamiri na kuonekana ni vitu vya kawaida. Wewe ambae hujanielewa nakuwekea kwa ufupi mada yangu nimesema HAKUNA APP YA KUDOWNLOADIA VIDEO/PICHA/AUDIO AMBAYO UTATUMIA KWA RAHA BILA MATANGAZO YA APP NYINGINEZO AU SITES. VILEVILE HAKUNA SEHEMU UTAINGIA KWENYE INTANETI UKAKOSA TANGAZO LA KAMARI AU LA MIKOPO YA RIBA MFANO MZURI NI HUMU JAMIIFORUMS