Kweli huyu dada alitaka kunitanguliza mbinguni

Kweli huyu dada alitaka kunitanguliza mbinguni

Ungepumzika kidogo boss🙏🏼
Hizi nyuzi ni chai ila kisaikolojia zinafichua mengi kukuhusu
 
Kweli mkuu, nikimuacha nitaumia sana, natafuta nguvu hapa niurudishe uhusiano kwa spidi kubwa
Mapenzi nd'ouwaga yako ivo.
Jishushe umfuate ukambembeleze.
Hata mimi kwa sifa ulizozitaja huwaga nakosa namna, hata nikimtimua leo, kesho hupata pressure yakumfuata.
Kwa kweli ni mtihani.
 
Nilipata mwaliko wa kwenda huko mkoani kwenye tukio la rafiki yangu mmoja, nikaona si vibaya nikaongozana na bibie.

Bibie akanipa bajeti yake kuanzia mavazi pamoja na vitu vidogo vidogo, ikabidi nimuwezeshe ili tu tutoke wote.

Siku ya tukio, tukawa tunakula pamoja na kupiga maji, tulipiga sana na kulewa sana; katika mazungumzo tukajikuta tumekwazana, nikajikuta nimemfinya mkononi.

Bibie akaamua kutoka nje kwa hasira, akakaa huko zaidi ya lisaa; baada ya muda namuona amerudi na mimi niko chakari kweli, baada ya kunifikia, akavua kiatu chake cha mchuchumio na kunianza kunipiga kichwani, damu ilitoka nyingi sana, ilibidi tuamuliwe na kuwahishwa kituo kidogo cha afya.

Bahati nzuri kwa sasa naendelea vizuri ingawa kuna dawa natumia; sasa najiuliza nimpige chini mazima au niendelee naye kiaina, ingawa katika mawasiliano naye anasema yuko tayari tuachane ila akihitaji matumizi na malezi ya zaigoti niwe tayari kugharamia.

Na sababu ya yeye kunifanyia hizo fujo, anasema nilimuabisha mbele za watu, akaamua na yeye asiwe mnyonge.

Kweli huyu dada alitaka kunitanguliza mbinguni.​


Kesi ya vichaa inaumuliwa na kushauriwa na vichaa wenzao!
 
Back
Top Bottom