Kweli ilikidhihiri uongo hujitenga. Ya utumwa yawekwa wazi

Kweli ilikidhihiri uongo hujitenga. Ya utumwa yawekwa wazi

Zawadini

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
3,051
Reaction score
2,269
Waswahili wana msemao wao husema "kweli ikidhihiri uongo hujitenga". Hii inamaanisha kwamba ikiwa kuna uongo unasemwa/unasambazwa, ikitokea siku ukaelezwa ukweli basi hule uongo moja kwa moja utaondoka kwani watu watakuwa wameujua ukweli.

Kumekuwa na simulizi nyingi kuhusu biashara ya utumwa duniani - pamoja na Afrika. Simulizi hizo zilielekeza upande mmoja tu - Waarabu - watu wakisahau au kujisahaulisha kuhusu pande nyengine. - Wazungu na Waafrika wenyewe (machifu na wazee). Kwa bahati tarehe 6 Juni, 2025 Wazungu wenyewe wakatoboa siri kwamba wao walihusika na biashara ya utumwa na wakaomba radhi kwa matendo yao hayo. Bahati iliyoje kwamba hayo yalifanyika wazi, mchana, kuzimu hakuna nyota pale Zanzibar. Sasa, nadhani, hadithi itakuwa nyengine kuhusu jambo hili la utumwa na tutapata simulizi zenye mashiko kuhusu jambo lenyewe.
 

Attachments

  • Utumwa na Wazungu.mp4
    19.7 MB
Back
Top Bottom