Kweli kiswahili kitatufikisha nchi ya ahadi?

Kweli kiswahili kitatufikisha nchi ya ahadi?

wanaotetea kiswahili ni wanafiki, ni swa na wake wanaomsifu mwalimu Nyrerere kila siku bila kutekeleza mawazo yake. ukiwachuguza utagundua wengine wana hizi shule za English Medium au wanasomesha watoto wao huko kwa sababu tu wanaenzi sana Kiingereza. hata majumbani wanawasemesha watoto wao kiingereza lakini hadharani watasifu kiswahili. Jambmbo hili la kukiponda kiingereza limeanza muda mrefu na kuwafanya baadhi ya wanachi kutokipa uzito na hatimaye kimeshuka sana miongoni mwa watanzahia wa kawaida.Janja ya sizitaki mbichi hizi ya wanasiasa kumbe wananufaika
maoni yangu ni kuwa tukienzi kiswahili but not at the expense of English. Uelekeo wa dunia kwa siku zijazo ni kuwa na lingua franka kwa watu wote duniani na kiingereza kina nafasi kubwa sana. tusipokazana vya kutosha kujielimisha lunga ya kiingereza na kung'ang'ania kiswahili pekee itafika siku tatajajuta. mfano kuna maarifa mengi sana yapo kwa kiingereza na hivi kila mtu akitaka kuyafikia kwa njia ya tafsiri sijui!! Mwalimu aliwahisema Kiingereza ni kiswahili cha dunia labda tutafakari hii hoja ya mwalimu
 
Kiswahili tunakijua useme wasomi wa Tanzania ni waoga. Haiingii akilini hata wakenya wanajua hilo kusema Kenya iko juu kwa Kiswahili kuliko Tanzania. Kiswahili kizuri Kenya kiko sehemu moja tu, Mombasa, zaidi ya hapo ni Kiswahili kama cha Kongo.

Kuhusu program za Microsoft, walienda wakenya na watanzania. Kwa ujumla sio kwa Kiswahili tu, watanzania tuko nyuma kwa kila kitu. Kwa ufupi, 'we are passive'. Kiswahili kuhusishwa na Kenya na si Tanzania ni jambo la kawaida kwa watanzania, mbona hata mlima wetu Kilimanjaro imekuwa hivyo mpaka tulivyokuja kushtuka usingizini?

Sasa turudi kwenye mada. Tumefika hapa tulipofika kwa sababu ya viongozi wetu na wanaharakati wachache kutudanganya kwamba Kiswahili ndio mkombozi wetu. Tunabaki kulalamika watoto wa 'vigogo' wanachukua nafasi za juu kwa sababu vigogo wanajua dunia inakoelekea huku wakiacha wadanganyika kuendelea kudanganywa. Sijaona viongozi au hawa watetezi wa Kiswahili wakipeleka watoto wao shule zetu za kata! Watoto wao wanapeleka English Medium na uwezo ukiruhusu wanasomesha wakwao Kenya, Uganda hata Ulaya na Marekani. Je huko wanafuata Kiswahili? Je wanawapenda watanzania baki kuliko watoto wao?

Nafasi za juu katika makampuni makubwa wanachukua wageni..ebu angalia maofisa wa juu kwenye mabenki, makampuni yote ya simu, madini...Asilimia kubwa kama sio wote ni wageni, zaidi sana wengine ni majirani zetu Kenya. Najua wengine watasema kwa sababu mengi ni makapuni yenye umiliki wa nje. Sio kweli, mbona nchi nyingine wakubwa wa makampuni ni wazawa? Pia mbona wakubwa hao hao wanatoka nchi nyingine tofauti na wanaomiliki makampuni hayo? Mfano mmilki wa benki Uingereza, mtendaji mkuu - Mkenya (Barlays na Standard Chartered Banks).

Point ambayo wawekezaji wengi wameweza kuishawishi serikali ni kwamba watanzania hawajiamini na hawawezi kufanya maamuzi. Kutojua lugha ni moja ya sababu ila inawekwa kifasihi zaidi, 'tafsida'.

Watanzania ambao wameshasoma upepo wako kimya, wanasomesha watoto wao kimya kimya, ila mimi inaniuma nitasema ukweli japo watakao pinga watapinga. Kuendelea kujishauri juu ya umuhimu wa kiingereza ni kupotea kwa hali ya juu. Haya yanatokea wakati kiingereza kikifundishwa kuanzia ngazi ya sekondari, je lugha ikibadirika kabisa tukabaki kusoma kiingereza kama somo tu na lugha ya kufundishia ikawa Kiswahili itakuwaje? Kama ningekuwa rais ningechagua mwaka wa kuimiza lugha ya Kiingereza, English Kwanza.

Nchi hata zenye teknolojia ya hali ya juu sasa wanaona umuhimu wa Kiingereza. Angalia China, wako juu kwenye teknolojia na kila kitu kiko kwenye kichina, lakini wameona hii haitoshi. Sasa wanakitafuta Kiingereza ili kuwawezesha kuwasiliana na dunia. Miaka ya hivi karibuni, vyuo vingi hususani Uingereza zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi ni wachina. Yaani ni wengi kuliko hata wazawa!

Tukirogwa au viongozi wetu wakirogwa na kutoa maamuzi ya kijinga kwamba kiingereza kisiwe lugha ya kufundishia, huo ndio utakuwa mlango wa kukaribisha ukoloni wa mtanzania kwa mara nyingine.

Mungu ibariki Tanzania!
 
mm nakubaliana na hoja kuwa endapo kiswahili kitatumika nchi yetu inaweza kupata maendeleo. sababu ziko nyingi la msingi kabisa lazima sote tukubaliane lugha ni njia ya mawasiliano na maelewano. sasa wewe angalia viko vitu vya msingi kama vingeandikwa kwa kiswahili kuhusu masuala ya afya na kilimo hata mwananchi wa kawaida angejua na kuchukua tahadhari

mm nimejaliwa kutembea nchi za ASia kadhaa, ndugu yangu asilimia karibu 97% hawajui Kiingereza, wanajifunza katika lugha zao, na zimewarahisishia kuwasiliana na kuelewana kirahisi, na ndio umekuwa mwanzo wa kufanya vizuri katika maendeleo. kwanini? hata vitabu vinaandikwa ktk lugha yao, vinasomwa na kueleweka hata na wananchi wa kawaida na kisha inakuwa rahisi kutekelezwa. lkn kwetu unakuta hata sera/mikakati/miongozo/sheria zinaandikwa kwa kiingereza wakati mwananchi wa kawaida hajui kiingereza na ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi yaliyoandikwa, unatarajia nini? ataweza kusoma na kuelewa

nashauri tubadilike, tujifunze kwa kiswahili

upungufu mwingine kuhusu walimu wasio na sifa hilo linatekelezeka ikiwa siasa haitaingilia suala la elimu na maslahi ya wahusika. ww fikiria kwasbabu ya upungufu wa ualimu miaka ya 2004-2008 hivi walichukuliwa vijana wengi waliomaliza F4-F6 na kuajiriwa baada ya kufundishwa kwa muda wa miezi mitatu, je unatarajia nn, huu ulikuwa mwanzo wa kuvuruga msingi mzuri wa elimu. vilevile watu waliofeli ndio wanachukuliwa kuwa walimu unatarajia nn? mbona vyuo vikuu havichukui watu wasiopata GPA chini ya upper second na first class. hl litizamwe vizuri na kwa makini

kuhusu wanafunzi kufeli kiswahili mm siwezi kushangaa kwani kile kiswahili kinavyofundishwa kinakuwa kimeacha utaratibu wa kawaida wa kumfanya mtu kuelewa na kisha kumpima uelewa. kimekuwwa too complicated, mm nimesoma kiswahili hadi A-Level, ninajua tatizo kwann watu kiswahili kina washinda kufaulu. mfumo na namna ya ufundishaji wake ni tatizo

suala lingine ni mfumo wa elimu, hauzingatii vipaji vya wananchi, mtu unasoma masomo kibao wakati mwingine bila sababu. vipaji vitambuliwe na viendelezwe, ndipo tutapata walimu bora, wanasayansi bora, wasaikolojia bora, watawala bora, wanasheria bora n.k.

Sidhani kama ni sahihi kuwa tunajilinganisha na nchi za Asia kama China au Japan, wao walishaendelea muda mrefu, na mazingira yao ya maendeleo ni tofauti sana na yetu, wao hawaitaji sana uwekezaji kutoka nje, sisi tunahitaji, wao hawahitaji sana kujitambulisha wao na bidhaa zao duniani kwa sababu walishatambulika, sisi tunahitaji. Kwa ujumla tunahitaji kushindana, siyo na China wala Japani, bali kushindana na majirani zetu ambao wanatupiga bao kila siku kwa sababu ya kujua English.

Swala la sera au miongozo kuandikwa kwa English tunaweza kubadilisha, siyo ishu, kama nilivosema mwanzoni nakubaliana kabisa na kuenzi Kiswahili, ninachosisitiza ni kwamba hii isitufanye tukitupe kiingereza, tuweke umuhimu pia katika kujua English, Kiswahili tayari kina mizizi mirefu hapa kwetu, ni vugumu kupotea, inabidi tuweke juhudi kwenye English kwa sababu tunaipoza, na madhara ya kuipoteza ni makubwa, mtasema msemavyo, mtachimbia vichwa chini, lakini bado umuhimu wa English katika maendeleo utabaki palepale, na bado kutojua kwetu kiingereza kutaendelea kutugarimu. Na sehemu nzuri ya kukuza English ni mashuleni.

Hivi mbona Kenya wanatumia English kutoka primary mpaka chuo kikuu na bado kiswahili chao kinakua? Na angalia jinsi Kagame anavyojitahidi kuingiza kiingereza Rwanda, tutabaki peke yetu na tutakuwa tunapigwa bao na kila nchi.
 
nakushauri fuatilia historia ya maendeleo ya uchumi wa china na korea kusini kuanzia miaka ya 1961, itaelewa na kukubali ninayokueleza
 
baadhi ya watu wadadai kuwa wanafunzi wanafeli kwa sababu ya kusoma kwa kiingereza. sasa mbona watu wengi tu wanapelekwa nje na wanasoma kwa kiingereza na wanafaulu vizuri tu? wengine wanasema kiingereza ni lugha ya mkoloni je, kwani elimu tunayosoma darasani haikuanzishwa na wakoloni? mbona hatuiachi? je wanafunzi wanaofeli somo hasa la hisabati darasa la saba ilhali linafudishwa kwa kiswahili? Na je, mbona wengi wanashindwa hata kusoma na kuandika hapo ni kiingereza? Mimi naona kuwa kushidwa kwa wanafuni hakutokani wala hakukuanzia na kiingereza bali sababu nyingine. kiingereza kianapata matatizo kama masomo mengine kutokana na mfumo uliopo
 
Kichagga ndio kitakufikisha unapopataka.
Tatizo la watu wengine ni kutopenda kujadili hoja mahsusi na hili limetuangusha sana.Hapa tunajadili mustakabali wa Taifa letu na kudai uwajibikaji katika masuala ya elimu na siyo vinginevyo. Pengine mawazo yako mazuri yanaweza kusaidia taifa hili. Hivi wewe umewahi kufikiri Tanzania baada ya miaka hamsini ijayo itakuwaje katika maendeleo ya elimu.
 
Tuache umaimuna. Kubali kataa English language bado ni muhimu na itaendelea kuwa muhimu esp in this era of globalization. Umaimuna utailostisha hii nchi
 
Ahsanteni wana JF,
Maoni yenu yamekuwa ya manufaa sana.
 
Kama nchi inahitaji zaidi wanaojua kiingereza basi msisitizo uwe kwenye kiingereza lakini kama wanahitajika wasomi wenye utaalamu na ujuzi wa mambo basi hapo lugha iliyo rahisi kwa mtanzania itumike(kiswahili)na kiingereza kipewe uzito wake kama lugha ya kimataifa. Hapo tutapata wataalamu wazuri wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani zao na katika lugha(kiingereza). Tuache siasa kujua kiingereza sana hakumfanyi mtu kuwa fundi bora kama hakuyaelewa mafunzo kwa kikwazo cha lugh.
 
Tuache umaimuna. Kubali kataa English language bado ni muhimu na itaendelea kuwa muhimu esp in this era of globalization. Umaimuna utailostisha hii nchi

Kiingereza ni muhimu lakini kwenye kuandaa wataalamu kiswahili ni muhimu zaidi kwa sababu kinaeleweka kwa wengi na kwa urahisi,kumbuka kujua kiingereza hakumfanyi mtu kuielewa mashine kama hakuelewa maelekezo ya mwalimu wake sababu tu ya lugha,hivyo watu wapatiwe maarifa kwa lugha wanayoielewa pia wafundishwe kwa ustadi kiingereza kama lugha ya kimataifa wala kufanya hivyo si kuwa maamuma ndo mana wengine hutumia lugha zao kuandaa wataalamu na pia hujua lugha nyingine kutegemeana na mahusiano.
 
wanaotetea kiswahili ni wanafiki, ni swa na wake wanaomsifu mwalimu Nyrerere kila siku bila kutekeleza mawazo yake. ukiwachuguza utagundua wengine wana hizi shule za English Medium au wanasomesha watoto wao huko kwa sababu tu wanaenzi sana Kiingereza. hata majumbani wanawasemesha watoto wao kiingereza lakini hadharani watasifu kiswahili. Jambmbo hili la kukiponda kiingereza limeanza muda mrefu na kuwafanya baadhi ya wanachi kutokipa uzito na hatimaye kimeshuka sana miongoni mwa watanzahia wa kawaida.Janja ya sizitaki mbichi hizi ya wanasiasa kumbe wananufaika
maoni yangu ni kuwa tukienzi kiswahili but not at the expense of English. Uelekeo wa dunia kwa siku zijazo ni kuwa na lingua franka kwa watu wote duniani na kiingereza kina nafasi kubwa sana. tusipokazana vya kutosha kujielimisha lunga ya kiingereza na kung'ang'ania kiswahili pekee itafika siku tatajajuta. mfano kuna maarifa mengi sana yapo kwa kiingereza na hivi kila mtu akitaka kuyafikia kwa njia ya tafsiri sijui!! Mwalimu aliwahisema Kiingereza ni kiswahili cha dunia labda tutafakari hii hoja ya mwalimu

Wachina,warusi,wajerumani na wengineo ni wataalamu wakubwa duniani je nao hukumbatia kiingereza kama sisi? Hivi ikitokea leo uchumi wa dunia unashikiliwa na uchina na tukalazimika kuwa karibu nao tutafanyaje kuhusu lugha? Wenzetu wanatumia lugha zao kuandaa wataalamu na wanajifunza lugha nyingine nyingi kutegemeana na wapi wanapalenga kwa maslahi yao sisi tunashabikia tu kiingereza.
 
Back
Top Bottom