Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Ushauri mzuri lakini umechelewa, umeutoa wakati tayari maamuzi yameshafanywa na mikataba imeshaingiwa nadhani. Km bado, better wazingatie ushauri wako mtoa Post
Mkuu naomba muiamini selikari yenu. Selikarini kuna wataalamu zaidi ya huyu mleta maada. Kwa kawaida kila mtu na mawazo yake na siwezi kuyapinga ya mleta maada maana ni mawazo yake. Wahusika hawakukurupuka na naomba tusiwakatishe tamaa. Wanafahamu wanafanya nini. Mkuu keshasema wanataka ndwge ya masafa marefu ili watalii waje moja kwa moja anamaanisha na yuko sahihi sana. Seatback and relax waacheni waturekebishie nchi.
Umeandika vizuri sana..lakini tununue ndege Kwanza... Tuwe nazo km kumi na tano. Kachumbali ni nzuri pia
 
Umesema lakini tujenge nyumba ndo tutafute wapangi tusitafute wapangaji wakati hata kiwanja hatuna
Ndo ukweli halisi....tunajenga kwa vision ya ndani na nje.....watu wanaogopa kukua....usipowaza globally utabaki locally
 
kiufupi,naona kama trilioni moja na nusu au mbili zikizikwa katika huu mradi,mafanikio yake ni kudra tu.

mradi umepikwa kisiasa na wataalam wanaletewa tu
 
watalii watavutiwa na ndege moja ambayo ikiondoka new york haijulikani itarudi lini?

kuna mashirika kila siku ya mungu yanapishana angani mara nne tano.

hiyo ndege inachukua abiria wangapi (hawazidi 600)na nchi inapokea watalii wangapi kwa mwaka? kama watalii milioni mbili,je ndege hiyo moja itakuwa suluhu?

tumeboresha mazingira ya vivutio vya utalii?

naamini mazingira yakiwa bora katika vivutio vya utalii,watavutwa kuja.

Mbuga kama katavi,gombe,selous nani anazijali?

nani anajali kuhusu ujangili?
 
Mawazo mazuri sana japo huenda ukaitwa mchochezi.
 
Hili ndege ni mzigo tu kwa sasa na tusipokuwa makini utakuwa ni mzigo wa muda mrefu.

Hivi waTanzania tufanyiwe nini?

tukigeuka huku watu wanalia uchumi hoi...tukigeuka kule....ufisadi umetamalaki...Bwana Yule ndo anajitahidi angalau aweke mambo mstarini..kila mwananchi anakuja na yake. Sasa afanye nini? Ukitokea ukaona jema la Bwana Yule utaambiwa wewe ni sehemu ya CCM au unataka cheo.

Ila nilichogundua waTanzania wengi tumezoea na tunapenda siasa za kudanganyana (no wonder watu wanamkumbuka Kikwete humu). Tunapenda michakato kwa sababu ndo inatupa nafasi za kupiga hela. Ni mara ngapi bajeti zimepangwa na hela imeliwa? leo Magufuli anahukumiwa eti ananunua ndege bila bajeti ya Bunge! Wonders shall never cease!

Au atukusanye waTanzania wote pale uwanja wa taifa tujadili vipaumbele vya taifa kwa kunyoosha mikono?
 
Watanzania tumekuwa wanasiasa zaidi kuliko, uzelendo umepotea kuanzia mizizi hadi matawi. Swala la msingi tunalijadili kisiasa. Mtoa maada ana hoja ya msingi. Ni muda muafaka kwa sasa kutrain watalaam wetu kwa ajili long term. Nadhani mkuu wa nchi anania mzuri tu, Ila ushauri kama huu ni vizuri kuzingatia. Nyumba ni yetu sote, mwenye kuleta kuti, fito, udongo wa kukandika, end of the day tuwe na nyumba yetu. Nyumba ya kupanga ina masimango.
 

Thegame si busara kwa mtu kama huyu barafu ambae ametoa ufafanuzi kama huu kumwita mtabiri. Ameeleza vizuri tu hatari iliyopo pindi tukikosa kitu kinaitwa "Fleet Commonality" kwenye shirika letu, kumbuka fedha iliyonunua na itayonunua hizo ndege ni fedha zetu mimi na wewe na Watanzania wengine wote na wala sio fedha ya mtukufu Rais ama CCM. Kwa mfano mimi kama ningeulizwa maoni yangu kabla ya ununuzi huu wa ndege ningependekeza kwanza tukodi kwa mkata wa ACIM (Aircraft Crew Insurance and Maintenance) katika kipengele cha Dry lease kabla hatujaanza kununua. Kurusha ndege sio issue sana kwa upande wa gharama, gharama kubwa utaziona wakati wa matengenezo (C check) ambapo ndege zinatakiwa zichunguzwe kila baada ya miezi 20 ama 24, sidhani kama ATC wapo na hanger na wataalamu wanaoweza ku accommodate matengenezo haya kwa sasa. Mkuu barafu tuendeleee tu kutoa maoni yetu kuhusu shirika letu hili kila mara inavyowezekana na sina shaka kuwa wahusika wa ATC wanapita hapa na kujifunza kitu.
 
Watanzania tusipatiane woga wa kuthubutu.
Usipovua viatu na kuingia mtoni huwezi kujua kina cha maji.

Magufuli ana entepreneurial spirit pamoja na ule moyo wa kuthubutu.

Mtoa mada,mpeleke mwanao mafunzo ya urubani ufaidike na fursa.
Think positive.
 
Watanzania tusipatiane woga wa kuthubutu.
Usipovua viatu na kuingia mtoni huwezi kujua kina cha maji.

Magufuli ana entepreneurial spirit pamoja na ule moyo wa kuthubutu.

Mtoa mada,mpeleke mwanao mafunzo ya urubani ufaidike na fursa.
Think positive.
Mkuu masopakyindi mimi nimekuwa positive sana kwa ATCL...nifuatile humu vizuri,toka enzi bimbadia inaletwa na kukashfiwa mimi nilikuwa pamoja nayo,nifuatile utaelewa ninaongea kwa nia njema.
Hilo la kumpeleka mwanangu,naamini umeandika kama dhihaka na kashfa kwangu;siwezi kukurudishia,nitaondoa maana ya kuwa na mjadala wa kistaarabu
 
Kawaida ya tz. Study haifaywi kabla ya uamuzi. Ona mifano. ndege ya rais, meli ya Bagamoyo, mabehewa rada na madudu mengine ambayo hayasemwi
 
Mkuu Thegame RwandAir hawana Dreamliner,na kwa sbb ya hiyohiyo "Fleet Commonality",Rwanda wameingia mkataba na Ethiopia wa miaka saba,ambapo marubani na mainjinia wa Ethiopia ndio wanaoziemdesha na kuzi-repair ndege zao huku wakiwafundisha Warwanda.

Hii inaongeza ghalama kubwa kwa shirika,hata hao Ethiopia na ubishi wao,bado Dreamliner marubani wake na wageni pamoja na wahandisi ni kutoka nje.Rating ya DREAMLINER kwa marubani na wahandisi sio ya mchezo.

Mimi sijaitabilia kushindwa ATCL,nimekuwa mstari wa mbele kuitakia mema na kuitia moyo.Fuatilia utaelewa humuhumu Jf
 
Wakati sisi tunakomaa na bombardier....iran wameagiza boeing 787 dreamliner ndege 80......

Kiukweli kwenye soko la airline sasa hivi ukiacha kutoa service nzuri lakini pia ndege zinazopendwa ni boeing na airbus.....

Ila ukiongea tu unawekwa ndani
 


Ushauri mzuri tatizo wahusika watataka mpaka ushauri utoke kwa mzungu, kutoka kwa mzalendo mwenzetu ni UCHOCHEZI na kuisimanga ATCL!
 
Mkuu sikuandika dhihaka hata kidogo.
Nia yangu ni kuonyesha kuwa katika kila challenging situation, mtu unaweza kufaidika.
Sorry kwa misunderstanding.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…