Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Mh Barafu katoa ufafanuzi wa kitaalamu ambao wengine tunauona una mshikheri kidogo kwani some issues are not justifiable kama mimi na baadhi ya watu tulivyofafanua. Ninahakika hata Barafu kajifunza mengi tu na mara nyingi amekuwa muelewa na mwepesi kujifunza. Kwako wewe, kinyume na Barafu, uko kisiasa zaidi na hutoi picha ni nini unataka zaidi ya kupinga tu kwa vile CCM inahusika. Kwanini tusiwaze nje ya kuta za vyama na itikadi bali kama watanzania. Najaribu kufikiri kwa upana zaidi. Wewe ni mtanzania na siyo lazima ukubaliane na mimi au Barafu bali uonyeshe uelekeo kitaaluma na siyo mihenuko ya kisiasa katika kila jambo.

barafu finally you are coming to terms na huu upuuzi wa kuifufua ATCL. Ulitetea sana ndege mpya na inaonekana ni mjuzi wa hayo mambo.

Tatizo linakuja kwa kua ni serikali inaendesha na kwakua serikali yetu ni CCMScrow na rais ana kauli ya mwisho kabisa hata kupita wataalamu, it is logical serikali isifanye biashara ya ndege.

Iko siku ndege itaisha mafuta hewani kisa mkuu kasema yatafika na ole wao wasipaishe ndege au wapaishe afu yaishe.

Sasa wewe umeliona hilo la Fleet Commonality maana ndio uwanja wako. Sie wa political economy tunajua ubaya wa serikali kuendesha mabiashara ya kawaida.

Bottomline serikali iachane na hiyo midudu. Wawekeze precision au waache tu hao binafsi wapambane. Iko siku Auric au Coastal watakua na mi dear bomba kibao na midrimlaina km mazingira wezeshi yatakuwepo.

Na siku hiyo ndipo hata sie leo tunaoona ndege ni ya wale nasi tutakua wapandaji maana ya msingi yatakua yametatuliwa.
 
Teh teh teh, mi napita tu, nasikia mkuu Melo yuko sentro na kanyimwa zamana kisa hataki kutuchoma kwa maafande. Ngoja nikae kimya tu, ingawa unaweza shangaa unashitakiwa kwa kukaa kimya wakihisi umefanya uchochezi kimoyomoyo😀😀😀
Hii inji haishindwi kitu ati!!!
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Gharama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege, kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
Ushauri mzuri sana na wakitaalamu, pia umependekeza nini kifanyike. Huu ndio aina ya ukosoaji wa kujenga.
 
Pole ndugu yangu ushauri huu wenye nchi hawawezi kukuelewa sanasana watakuita mpinzani.Subiri baada ya miaka kumi.Kwa sasa kanyaga twende.CCM mbele kwa mbele.Vikao ndani ya Ikulu wanasema wao ni wenye nchi wengine hawana akili,hawajui chochote,wao ni wao tu.
 
Barafu umenena vema tena kizalendo. Hata hivyo usishangae upande ule wa mtaa wa Lumumba wakasema una wivu wa kike ndo uwezo wetu wa kufikiri. Ubarikiwe sana
 
kwani ni za mkopo?sio kila kitu unapinga tu,halafu ndio wa kwanza kuzikimbilia kufanya booking
Unajibu hoja kilumumba pole mahaba yakipitiliza yanapofua bahati wengi wamesha pofuka wana macho lkn hawaoni wana masikio lkn hawasikii wana midomo lkn hasemi.
 
utashindwa na ulegee mojakwamoja....tatizo una roho mbaya kama wachawi kisa aliyeifufua ni raisi kutoka CCM
 
For short run lazima itugharimu tu hilo halina mpinzani but for long run huoni tutakuwa na wataalam wengi wenye ujuzi tofaut tofauti na kupelekea kuwauza hata nje kama nchi zingine wafanyavyo?

Nafikiri hili la kujua mengi halitatulaza njaa, kikubwa tu tushikamane.
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Gharama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege, kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
 
Bombardier: Ni CS300 na Q400 na ndege no Boeing 787-8. Msitudanganye. Sio kachubari. Q400 na CS300 ni Bombardier. Boeing in 787 tu. Au unagopa Q400 pangapoi na CS300 no jet. Lakini no kampuni moja. Tulikuwa F27 pangaboi na 737 jet tulikuwa poa tu
 
Mh Barafu katoa ufafanuzi wa kitaalamu ambao wengine tunauona una mshikheri kidogo kwani some issues are not justifiable kama mimi na baadhi ya watu tulivyofafanua. Ninahakika hata Barafu kajifunza mengi tu na mara nyingi amekuwa muelewa na mwepesi kujifunza. Kwako wewe, kinyume na Barafu, uko kisiasa zaidi na hutoi picha ni nini unataka zaidi ya kupinga tu kwa vile CCM inahusika. Kwanini tusiwaze nje ya kuta za vyama na itikadi bali kama watanzania. Najaribu kufikiri kwa upana zaidi. Wewe ni mtanzania na siyo lazima ukubaliane na mimi au Barafu bali uonyeshe uelekeo kitaaluma na siyo mihenuko ya kisiasa katika kila jambo.
Nimeonyesha vizuri kabisa utaalamu wangu ni siasa. Na ninaheshimu wa kwenu wa ndege na wala sijapinga mambo ya kuwa na shirika la ndege la kitaifa. Napinga serikali kuliendesha. Haijawahi kuweza. Haiwezi na haitaweza. Ni suala la muda.

Nimeelezea kwenye posti mbalimbali kuwa shida kubwa sana ni ufisadi na ile hali ya cha wote hakina mwenyewe. Only way wanaweza kuiendesha ni kuwa na udikteta flani. Na wenyewe huwa haudumu.
 
Mkuu masopakyindi mimi nimekuwa positive sana kwa ATCL...nifuatile humu vizuri,toka enzi bimbadia inaletwa na kukashfiwa mimi nilikuwa pamoja nayo,nifuatile utaelewa ninaongea kwa nia njema.
Hilo la kumpeleka mwanangu,naamini umeandika kama dhihaka na kashfa kwangu;siwezi kukurudishia,nitaondoa maana ya kuwa na mjadala wa kistaarabu
Kiukweli huwa sina shaka na ushauri wako! Sema leo wanaokudhihaki wamesahau kati ya watu waliojenga hoja sana humu ndani na kutetea kwa kila hali kipindi bombadier zinanunuliwa ulikuwa ni wewe!

Usikate tamaa mkuu hii nchi ni yetu sote
 
ATaifufua makapi ya CCM lowasa haya furahi...wewe kenge
Kawaida ukiwa huna hoja matusi na kubwabwaja kunatamalaki. Ishu sio chama gani kiendeshe au kufufua ATCL. Hoja yangu ni kuwa serikali haiwezi na haitaweza maana udhaifu wao unafahamika. Waachie private sector ama waingie ubia nao.

Sasa wewe unaeweza kuongea na kenge we utakua nani? Rudi kwenye hoja twende mdomdo tutafika. Ukitukana hausaidii yyt sanasana unaonekana dhaifu wewe na unayoyashabikia.
 
Bombardier: Ni CS300 na Q400 na ndege no Boeing 787-8. Msitudanganye. Sio kachubari. Q400 na CS300 ni Bombardier. Boeing in 787 tu. Au unagopa Q400 pangapoi na CS300 no jet. Lakini no kampuni moja. Tulikuwa F27 pangaboi na 737 jet tulikuwa poa tu
Mngekua poa msingeua shirika.
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Gharama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege, kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
Tupe na mifano mkuu
Taja mashirika ya ndege yaliyofanikiwa yasiyo na kachumbari ili tuelewe vzuri
 
Kiukweli huwa sina shaka na ushauri wako! Sema leo wanaokudhihaki wamesahau kati ya watu waliojenga hoja sana humu ndani na kutetea kwa kila hali kipindi bombadier zinanunuliwa ulikuwa ni wewe!

Usikate tamaa mkuu hii nchi ni yetu sote
Mkuu ngushi leo nimejifunza kitu,maana kuna watu wamenitukana na kunikashifu;mimi nipo huru,hupongeza na kukosoa pale ninapoona inafaa,na hufanya hivyo kwa staha.

Lkn leo naona kuna member wanaporomosha tu matusi,imenihuzunisha kidogo
 
Back
Top Bottom