Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Mkuu ngushi leo nimejifunza kitu,maana kuna watu wamenitukana na kunikashifu;mimi nipo huru,hupongeza na kukosoa pale ninapoona inafaa,na hufanya hivyo kwa staha.

Lkn leo naona kuna member wanaporomosha tu matusi,imenihuzunisha kidogo
Pole sana mkuu, wakati napitia comments za watu nimeshangaa sana kama hivi ni kweli tumekuwa wasahaulifu kiasi hiki!
Kiukweli kipindi kile zile nyuzi zako zilitubadilisha sana wengi na kuanza kuwapuuza waliokuwa wanakandia lile swala!
Nakumbuka uzi wako hata ile juzi ilvyotokea ile shoti mwanza sijui arusha bado ulileta ufafanuzi wenye mashiko kabisa!
Usikate tamaa tupo tunathamini michango na fafanuzi mbalimbali ambazo huwa unazileta humu ndani,
 
Serikali inabidi iangalie haraka sana mishahara na allowances za marubani wazawa, locals, mishahara yao ni midogo kabisa kuliko hata makampuni madogo ya watu binafsi..[/B]

Mfano Rubani wa Fastjet au ATCL akiwa mgeni analipwa almost mara mbili ya wazawa.. hili ni kosa kubwa kabisa..

Mishahara ya marubani wazawa walipwe vizuri kama KQ wanavyofanya, wanawalipa mishahara mizuri na allowances nzuri marubani wazawa, hii inawapa motivation kubwa sana..

Hili ni muhimu mno..!!
 
Ngosha akioneshwa tu ndege imepaki ye ananunua...atakuja kuuziwa hadi kiwanja bahari ikikupwa maji!
 
Umeandika vizuri sana..lakini tununue ndege Kwanza... Tuwe nazo km kumi na tano. Kachumbali ni nzuri pia

Mkuu:
Ni vyema ungefafanua ki-utaalam zaidi juu ya uzuri wa kuchanganya aina zaidi ya mbili (Kachumbari) kwenye fleet ya ATCL.
 
ukweli ni kwamba! alieanzisha mjadara nimtaalamu wa haya maswala! amechambua vizuri sana..tukitoa itikadi na tukaweka mbele weledi watu km hawa wanatakiwa wawepo kumshauri JPM kwny haya maswala..japo anasound km na yeye ni mfanyakazi kwny ATCL au TCAA.. yuko full detailed!..
kachumbali itaeza kutucost hasa kwny hatua za mwanzoni.
 
Mleta mada ameongea maneno ya msingi na baadhi ya mifano haiko mbali na sisi. Precision Air ni kampuni ndogo lakini imeweza kusurvive kwa miaka kadhaa pamoja na changamoto zilizopo, wako focused kwenye ATR. Pia kampuni ya Auric Air wamajikita zaidi kwenye safari fupi zakini ziko consistent sana na wanatumia ndege aina moja, CESSNA.
Hata kwa mabasi (mfano kwa kwetu sisi wenye uelewa mdogo), kampuni inakuwa na experience nzuri kama wakiwa focused kwenye brand moja. Mfano Dar Express na Scania na tunaona walivyoweza kudumu miaka mingi.
 
Mleta mada ameongea maneno ya msingi na baadhi ya mifano haiko mbali na sisi. Precision Air ni kampuni ndogo lakini imeweza kusurvive kwa miaka kadhaa pamoja na changamoto zilizopo, wako focused kwenye ATR. Pia kampuni ya Auric Air wamajikita zaidi kwenye safari fupi zakini ziko consistent sana na wanatumia ndege aina moja, CESSNA.
Hata kwa mabasi (mfano kwa kwetu sisi wenye uelewa mdogo), kampuni inakuwa na experience nzuri kama wakiwa focused kwenye brand moja. Mfano Dar Express na Scania na tunaona walivyoweza kudumu miaka mingi.
Mkuu lukindo wewe sasa ndio tumeelewana vizuri sana.Precision na ATR imewafanya wasiwe na ghalama kubwa ktk matengenezo,sababu wana wahandisi ambao wapo hapa hapa Tz,wamejenga na hunger yao hapahapa kiasi matengenezo hata makubwa ya ndege zao wanafanyia hapa hapa Tz.

Si Auric Air tu mkuu,hata Coastal Travel wamejikita kwenye C206,C208 na Pilatus12(PC12).Wana hunger yao hapahapa Tz,na matengenezo yao wanafanyia hapa hapa na marubani wanawafanyia rating hapa hapa.Asante kwa mifano mipya uliyoniongezea Mkuu
 
sasa nyie mnatakaje? tatizo hamkuzoea mambo makubwa mlizoea tanzania iliyo shindwa kila kitu...unataka kuniambia serikali hawajui hayo? unadhani CEO wa ATCL hajui hilo....kwahiyo hasingenunua dreamliner unadhan bombardier wana ndege nyingine za masafa marefu kama boeing....kwahiyo tufanyeje tusilifufue shirika kisa gharama ni kubwa..husione vyaelea vyaundwa...ila katika vitu ambavyo magu hatutamsahau kama taifa ni kufufua ATCL.....ipo siku tutamkumbuka jamaa kafanya kazi kubwa mbona kikwete kwa miaka10 hata Q400 ilimshinda?
Jifunze kuandika vzr HUSI..ndio kitu gani
 
Pilot in command, first officer,engineer.......duuuh sikujua hata km kuna watu hawa kwny ndege.....mi nlijua pilot tu akipaki anafungua toolbox anapiga spanner
 
barafu ushauri muruwa mm naona kuna kutafuta sifa kama nimenunua ndege nzuri instead ya kusimamisha shirika maana atakuja na airbus kutusifia na pia tutanunua hebu tuwe makini madam nia rais kaonyesha aache wataalam wafanye yao
Mkuu BAFA unaweza kupitia hapa tena?
 
Mkuu lukindo wewe sasa ndio tumeelewana vizuri sana.Precision na ATR imewafanya wasiwe na ghalama kubwa ktk matengenezo,sababu wana wahandisi ambao wapo hapa hapa Tz,wamejenga na hunger yao hapahapa kiasi matengenezo hata makubwa ya ndege zao wanafanyia hapa hapa Tz.

Si Auric Air tu mkuu,hata Coastal Travel wamejikita kwenye C206,C208 na Pilatus12(PC12).Wana hunger yao hapahapa Tz,na matengenezo yao wanafanyia hapa hapa na marubani wanawafanyia rating hapa hapa.Asante kwa mifano mipya uliyoniongezea Mkuu
Tatizo mkuu anajua kila kitu
 
ziliponunuliwa panga mlilopoka sana sasa zinakuja mlizotaka mnaleta utaalamu
 
Tunamatizo Watatizo kweli. Kwani ATC Walikuwa Na ndege za ainagani? Kama hivi tu. F27 Boeing 737 Na Ndege ndogondogo toka Canada twinnwater alizouziwa mchanga mmoja Na kuanzisha kampuni yake
 
Commonality ya ndege ni muhimu lkn kwetu tulishindwa kununua 737 sababu zingechelewa sana.labda ungelaumu kwa kuto consider kukodi lkn pia kukodi ni gharama si mchezo.kukodi maintenance engineers ni jambo lisiloepukika kwa sababu wakati wanajenga capacity
 
Wakati tunaendelea kumpongeza Rais JPM kwa juhudi zake za kufufua shirika la ndege Tanzania(ATCL) tujipe na muda wa kutafakari pia mambo mengine na "kuhoji" kwa nia njema ya kutuondoa hapa tulipo kwenda mbele.Kuhoji kwetu ichukuliwe kama changamoto ya kulihuisha shirika letu na si kuliangamiza.Isije ikawa kuna watu hawamshauri vizuri Mzee au wanataka kumuingiza kwenye historia ya walioshindwa kuirudisha ATCL angani kama miaka ya 1980.

Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.Hawa ni uzao wa "Kabila" moja toka Canada.

Baadae tumemsikia Rais akisema ameshaangiza B787(Dreamliner).Hivyo kufikia miaka mitatu toka sasa,ATCL itakuwa na Dash8-Q400,CS300 na B787(Dreamliner).Hii ni "kachumbari" isiyo na viungo...Inaweza kuliletea shirika changamoto na hata hasara huko mbele ya safari,na tukadidimia kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Masharika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality";yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja,zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation,au mkatumia Boeing,Bombardier,ATR,Embrer nk.

Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa same model and Same Generation ya ndege,mfano Boeing 737-700,B737-700ER na B737-700c au Same model na different Generation,mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

Kuna faida nyingi kwa shirika kuamua kuwa na ndege kutoka kampuni/mzalishaji mmoja kuliko kuwa na shirika lenye ndege kama "kachumbari".Yaani shirika l moja kama ATCL lina ndege kutoka Bombardier,Boeing na Airbus.Huu ni mseto unaotishia ukuwaji wa shirika kibiashara na kiutaalamu.Faida kubwa ni kuwa mnapunguza ghalama za ku-train marubani na pia kupunguza ghalama za maintanance.

Mpaka sasa ATCL imeleta ndege aina ya Bombardier,na hatukuwa na marubani wa kurusha aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa darasani,hatukuwa na wahandisi wa aina hiyo ya ndege mpaka pale walipopelekwa pia darasani kufungua modules za Q400.Na hata sasa,bado tumeazima wahandisi toka Zimbabwe na Malawi walio na uzoefu wa kuhudumia ndege hizo.

Hii ni kusema hata sasa shirika kama ATCL linatakiwa lijizatiti lenyewe kwa kuwa na wahandisi wake na si wa kuazima na marubani wake na si wa kuazima,ile ile dhana ya kuongeza faida na kubana matumizi itimie.Kenya na "vurugu" zake katika usafiri wa anga,Dreamliner zimawatia adabu.Hao Ethipia wana Dreamliner kadhaa,lkn mpaka sasa mainnjia na marubani wa ndege hizo ni kutoka nje ya Ethipia;yaani wanakodi kuanzia Pilot in Command,First Officer na Injinia.Hawajwa na mainjinia walio "certfied" kuigusa na kuikarabati Drwmliner...

Kumpata rubani Tanzania hii mwenye masaa(rating) ya kuendesha Dreamliner sio kazi ya mwaka mmoja,na kumpata injinia wa kuihudumia Dreamliner aliyekuwa certified siyo kazi ya mwaka mmoja.Ni safari ndefu.Haiwezekani rubani mwenye rating ya pangaboi aingie moja kwa moja kwenye dreamliner.Inahitaji muda na pesa.

Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

Mashirika mengi yamefanya hivyo,Kenya imezingatia na inamiliki ndege aina moja za E170 na E190 pamoja na Boeing.Hii inawasaidia kuwa na marubani wenye ujuzi wa aina hizo za ndege na hivyo kuepusha ghalama,pia inasaidia sbb wanakuwa na injinia wenye leseni za E190 na hivyo kupunguza ghalama.Ethiopia yeye ameamua kuwa na Bombardier na Boeing tu.Kuanzia B737,735,767,777 na 738.Rwanda alichofanya amenunua Bombardier,Boeing na sasa Airbus na "amekodisha" marubani na wahandisi wote toka Ethiopia ili wamfundishie vijana wake kwa mkataba wa miaka 7.

Kutoka kuwa shirika "mfu" na kuacha kuzingatia "Fleet Commonality" ni kama tunarudi kulekule walikoshindwa waliotangulia.

Uliletwa uzi humu watu "wanalalamika" kuiona Pangaboi ikizunguka Dsm siku nzima badala ya kuanza safari za mikoani.Ile ilikuwa ni "Touches and Goes" ili wale marubani walioenda darasani kufanya kwa vitendo kabla ya kukabidhiwa.Sasa ikumbukwe mafunzo yake sio kama gari,kwamba unajifunza huku ukiwa na chombo.Kwenye ndege ni "Flight Simulator" ambayo baada ya kumaliza,ndio unapewa ndege huku ukiwa na instructor,na kukabidhiwa ndege ni hadi pale utakapoonekana umefudhu kweli(usije kuuwa watu)

Sasa hata kama tulipeleka marubani sita kwa maana ya pair tatu,basi hapo wenye uwezo wa kurusha ni watatu tu,huku hawa wengine wakitumia hata mwaka mzima kupata uzoefu na masaa ya kuwa pilot in command.Gharama hizi zote tunaweza kuziepusha kwa kuzingatia "FLEET COMMONALITY" kwa kuwa na ndege za kampuni moja itakayotusaidia kuzalisha wahandisi namarubani walio certified kwa aina fulani ya ndege, kuliko kukimbilia kwenye "haterogenious fleet" itakayoongeza ghalama zaidi.

Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boieng na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

Kuhama toka kwenye "bombadia" mpaka kwenye "Dreamliner" ambayo ni B787(New Generation) wakati tumeacha wala hatuna wataalamu wa B737,B738,B739,B767 na B777...tumeruka generation yote ya kati mpaka kurukia latest ya B787....

Ni mtazamo tu;hatuisimangi ATCL
Ushauri mzuri wenye kuonyesha unatambua hatari ya mazingira tuliopo usiposifia au unapokuwa sahihi wakati "wenyewe" wamekosea.
 
Back
Top Bottom