Mwigamba son
Member
- Jan 11, 2012
- 27
- 6
Ama kweli mwenye nacho ataongezewa na asiyenacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho hivi karibuni mh Pinda wakati akisoma bajeti ya wizara yake alisema zoezi la sensa litafanywa na walim pamoja na watumishi wengine wa umma.Jambo hili naona kama ni mwiba mkali kwa vijana waliotoka vyuoni wasio na ajira. kwani wangepewa fursa hiyo pengine wangejipatia mitaji kupitia zoezi hilo la sensa. Kitendo cha kuwapa walim na watumish wengine wa umma ajira hii wakati tayari wao wana ajira ni tusi kwangu mie kijana nisiye na ajira. Sasa nimeamini ccm haina sera yoyote ya kuongeza ajira kwa vijana.
Kama ukosefu wa ajira kwa vijana ungekuwa uko kwenye vichwa vya watawala basi vijana wangekuwa wa kwanza kufikiliwa panapo fursa kama hizi. hivyo serikali iliyopo madarakani nadiliki kusema haina nia ya dhati ya kutatua taizo la ajira kwa vijana.Kweli Mh Pinda unatunyima vijana wa kitanzania tusio na kazi zoezi la sensa na kuwapa watumishi wa umma ambao tayari wana ajira na mpaka mmewalazimisha walimu kubadili mihula mashuleni.hivi kweli vijana hatuwezi kulifanya zoezi hili kikamilifu mbona mnatupuuza mheshimiwa