Kweli mke wa mtu ni sumu

Kweli mke wa mtu ni sumu

Kaka uliyo ongea yote hakuna hata moja limenistua...😂😂😂
Kiufupi mi siachi haka katabia dadek zangu....
Dogo utakuja upakwe Kimbo 🤣🤣🤣
Na ukitembea na mke wa mtu unakuwa unaharibu future yako. Chukulia Mke wa Farao na Nabii Yusuf AS. Yusufu angekula mke wa Farao kuna mangapi yangeharibika ?
 
Nakuunga mkono. Mimi mwenyewe siku nikimfumania mke wangu suruhisho ni kuachana nae tu. Ksbb itakuwa yeye kamchagua huyo ndio anaeridhika nae
Ni kweli kabisa , kwa sababu hata ukiua au kufanya uhalifu ni kujiweka kwenye matata tu kwa mke ambae hakuheshimu .
 
Dogo utakuja upakwe Kimbo 🤣🤣🤣
Na ukitembea na mke wako unakuwa unaharibu future yako. Chukulia Mke wa Farao na Nabii Yusuf AS. Yusufu angekula mke wa Farao kuna mangapi yangeharibika ?
Mkuu tabia kama ngozi...
Alafu mpaka kushikwa hiyo ni kama ajari kazini tuu..

Mimi mkuu nikuambie sijawahi dakwa hata na bado napeleka show show...
😂😂😂😂
 
Wakuu !
Habari za majukumu na mishemishe za maisha ya kila siku ?

Huu msemo wa Mke wa mtu ni sumu hakika ni kweli na ni sumu kweli pale utakapo ingia kwenye 18 za mwenye mke wake.

Kuna visa kama vitatu hivi nitavielezea hapa, viwili nimevishuhudia kwa macho yangu na kimoja nilisimuliwa na Mshikaji wangu ambaye ni fundi umeme.

Kisa cha kwanza nilicho kishuhudia kwa macho kilitokea maeneo ya Buguruni kama miaka 8 iliyopita. Ilikuwa hivi kuna Kijana alikuwa ni Mwalimu alikuwa akiwafundisha watoto wa Jamaa Tuition, kila siku jioni alikuwa anaenda kuwafundisha wale watoto, sasa baada ya muda kidogo jamaa akajenga mazoea na mke wa Jamaa na Jamaa mwenye mke alikuwa ni mfanyabiashara mwenye ishu zake Kariakoo. Katika mazoea ya hapa na pale Teacher akaanza kumla mke wa jamaa tena mle mle ndani na alikuwa na mazoea ya kwenda kujilia tunda muda wowote hata pale Watoto wanapokuwa wapo shule yeye amachukua bodaboda anaenda kushusha mzigo.

Siku zilienda mpaka majirani wakawa wameshitukia ule mchezo ikabidi wamtonye mwenye mke. Mwenye mke kwa sababu alikuwa anampenda sana Mke wake ikabidi ampige marufuku Mwalimu kuja kuwafundisha watoto tuition pale nyumbani.

Mawasiliano kati ya Mwanamke na Teacher yaliendelea huku jamaa mwenye mke alikuwa amewapa kazi Vijana ya kufuatilia nyendo za mke wake.

Za mwizi ni 40 tu, siku ya tukio na Mimi siku hiyo nilikuwa maeneo ya Buguruni kwa sababu nilikuwa na mshikaji wangu maeneo yale. Ilikuwa ni jumamosi mida ya saa 7 mchana wakati fumanizi linatokea tupo Bar na Mshikaji wangu mara kelele na vurugu za hapa na pale zikatokea.

Hiyo Bar ilikuwa na Guest House mle mle, ghafla upande wa guest house tukasikia kelele na vurugu, jamaa mwenye mke alikuwa ameweka mtego na akawa amewakamata mgoni wake na mke wake, Jamaa alikuwa analia sana kwa sababu baada ya kumfumania mke wake wake alipovamia alilizwa na ule mkuyenge wa ticha 🤣🤣🤣

Ticha alikuwa na mguu wa mtoto na jamaa aliuona live aliishia kulia kwa hasira sana. Kama mnavyojua fumanizi la Uswazi watu huwa wanajaa kama kuna harusi ghafla difenda la polisi likaja pale likawabeba Mwanamke na yule jamaa mpaka kituoni, baada ya hapo sikufuatilia tena.

Tukio la pili hili nilisimuliwa na jamaa yangu Fundi umeme hili lilitokea maeneo ya Mbezi Msumi. Kuna Kijana alikuwa anamla mke wa mtu yaani mwenye mali akitoka tu na mwizi wa mali anaenda kujipakulia mke wa mtu. Kuna siku jamaa kama bahati tu aliongea na mlinzi wake Mmasai akampa na hela na Mmasai akaropoka kuna njemba huwa inakuja hapa mapema tu saa moja au saa mbili asubuhi ukiondoka kwenda kwenye mishe zako, Jamaa akamwambia Masai chukua hii 5000 weka vocha akitokea tu huyo mwizi wangu nipigie.

Kumbe jamaa baada ya kuambiwa vile akawa amewapanga wale Majamaa ya Naccoz Camp Gym pale Mabibo kwa Mfaume Mfaume yule Bondia. Siku ya tukio la kukamatwa mwizi ilikuwa mida ya saa 6 mchana, Masai alimpigia Bosi wake na Bosi akawasiliana na wale jamaa wa Naccoz Camp wakavamia walimkuta Mgoni yupo na taulo tu sebuleni anasubiri kunywa mchemsho wa Kuku.

Jamaa alipovamia na wale Mabaunsa hawakuwa na stoy nyingi sana wale Mabaunsa walitengewa ule msosi na wakanywa na bia safari lager za kutosha.

Baada ya kushiba walimkamata yule mgoni walimshughulikia haswaa mpaka aliacha kinyesi na wakaambiwa Mke na Jamaa wapige deki. ( Hii ni story niliambiwa na jamaa yangu )

Tukio la tatu nililoshuhudia ni juzi mechi ya Simba na Yanga.

Kuna Mshikaji ambaye ki umri ni age-mate wangu tu (34, 35, 36) alikuwa na mazoea sana na Dada mmoja hivi ambaye ni mke wa mtu huyo Dada ni muuza duka la mumewe. Mshikaji alijenga naye mazoea yaliyopitiliza mpaka wakati mwingine alikuwa anamkumbatia hadharani.

Aisee vile vitendo tulikuwa tunamwambia sana achana na haya mambo hata kama unakula huo mzigo usijionyeshe hivyo. Siku ya Jumamosi (Simba na Yanga Day) ndio walikuwa wamepanga wakapeane utamu. Kwa sababu yule Dada ni Msabato alikuwa hafungui duka.

Walipanga wakutane lodge na jamaa alikuwa na kimuhe muhe sana.

Demu alitangulia lodge na jamaa akamfuata yule Demu. Kufika lodge akampigia yule demu na demu akamwambia nipo room no fulani. Jamaa naye akaenda mpaka ile room akafungua mlango na kuingia ndani, ile anafunga mlango tu nyuma ya mlango alikuwa amesimama Mwenye mke na Chooni kulikuwa na Jamaa mwingine. Na Mwanamke alikuwa amekaa kitandani.

Lakini mpaka sasa huyu Mshikaji haonekani hapa mtaani na sijui ilikuwaje huko lodge, na Mwanamke yupo dukani anaendelea na kazi zake poa kabisa na yuko happy as usual.

Hitimisho:
Wake za watu hawafai Vijana wenzangu tuachane nao na tusiwe tunatengeneza mazoea nao hata kidogo. Unaona Mwanaume mwenzako anatunza na kuhudumia na wewe unataka mserereko acha kabisa mazoea na Mke au Mpenzi wa mtu ni hatari, fedheha na aibu.
Kwani mkuu ulishasikia wapi kuna mme wa mbwa?
 
Kuna wanaume wengine ndio chanzo chawake zao kuliwa hovyo.
Jamaa maisha yamemchapa kidogo tu kaikimbia Familia,Kahama na mkoa kabisa,Dada wawatu ako na watoto 4 ajue wanakula nini wana vaa nini,..Dada ndio yupo mwanzoni mwa 40s ndio anautaka balaaa...Wacha mafala wengine wagongewe tu.
Hahaha
 
Gentleman,
elezea vizur kwa kina kifupi kidogo kwa faida ya wadau tafadhali 🐒
Manyaunyau SC ni Makolokolo SC, 2020 kabla ya mechi dhidi ya Watani zao Yanga SC kuna paka mweusi alikatiza katikati ya uwanja akavuka na kurudi kisha akaelekea langoni mwa Mbumbumbu SC na kupotelea mazingira tata. Si unajua tena Simba SC na imani za kishirikina ni damu na maji hata kwa madiba waliwashaga moto uwanjani hadi walipigwa faini? ndiyomaana huwa nawaita hivyo na hizo nick names hakuna hata jina la bahati mbaya lisilotokana na vimbwanga vyao Simba SC.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Wataalam sikuwahi kuwaza kama nitakuja tembea na mke wa mtu ila kutokana na mazingira tumejikuta tumezama penzini na huyu cheupe na sijuw nitachimokaje.hiki kisa changu kinasisimua sana naomba niishie hapa ila ukweli ni kuwa tupo penzini na penzi ni zitooo
 
Back
Top Bottom