mdogo wangu
true_diva.....
pole sana kwa yaliyokukuta. napenda tu ujue kuwa siyo mwisho wa dunia. Una maisha yako wewe kama wewe, bila kuwa na mwingine, na hayo maisha yako yana-deserve kuendelea mpaka pale yatakapoishia.
Una muda mfupi sana wa ndoa, na nakuambia niamini kabisa kipindi hiki huwa ni kigumu sana katika ndoa kuliko kipindi chochote, pambana kwa kadiri Mungu atakavyokujalia na utakishinda tu.
umeona dada zako wengi hapo akina
snowhite,
gfsonwin na wengine wengi tu, hapa pia sitataka kabisa kumwacha
Nyamayao, na mimi mwenyewe, naweza kusema tumekuwa kwenye hii tasnia kwa miaka mingi sana, na hakuna kati ya hao ambaye amekiri hapa kuwa imekuwa ni tambarare tu..... lakini look at them now, kila kitu kimekuwa historia.
Mimi ninachotaka kukushauri ni kwamba, kwanza jiangalie unataka nini katika maisha yako........ nimeona umekiri kuwa unampenda sana, jitahidi kupigania penzi lako (kama linastahili) na utapata ujira wako.
Mimi huwa napingana sana na kung'ang'ania kitu ambacho si changu. hapa nataka nikuambie kuwa ongea na huyo mume akupe msimamo wake kuhusu nyie wawili (wewe na huyo x), usiongee naye kwa vitisho, mpe muda wa kujifikiria na kuamua kuwa anataka nini. kama anakuchagua wewe basi akuheshimu (hapa mimi naamini kabisa ni ngumu kumkataza mtu kuwasiliana na watu ambao wewe huwataki, anaweza kukuambia hawasiliani naye kumbe anakudanganya) la maana hapa ni kukuheshimu.
kama unaweza, jitahidi sana hii kitu iwe kati yako, mumeo na Mungu wako, hapa JF umekuja sisi hatukufahamu na tunakupa majibu general tu, lakini kwa watu wanaokufahamu usitegemee hali itakuwa tambarare; kuna ambao watamwagia mafuta ya taa kwenye moto hali ikawa mbaya zaidi......
Kaza Moyo, jua unachotaka, then songa mbele.
Mungu akutangulie katika kila utakalolifanya